Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

Nimeamini TANESCO inatumika kisiasa

Wasalaam Wadau wa JF na GT wote.

Ninapoandika Uzi huu kwasasa Hatuna Umeme hapa Tulipo, tatizo hili hapa kwetu #Kilosa halijaanza wiki iliopita Tarehe 07/09/2015 wakati Tanesco wakitangaza Kujaribu mitambo ya Gesi.

Huku kwetu Tatizo la kukatika Umeme kwa Masaa 16 mpk 18 kwa siku limeanza Tangu mwezi wa Saba (07) Mwanzoni, ni takribani Miezi mitatu sasa hatuna umeme wa Uhakika na Bila Taarifa yeyote kutoka katika Shirika hili la Ugavi wa UMEME.

Wiki iliopita TANESCO walipotangaza mgao utakoma Tarehe 14/09/2015 tulijipa moyo basi nasi tumepona, UMEME uliendelea kukatika, Likaja Tangazo Umeme wa uhakika unapatikana sasa Ijumaa tarehe 18/09/2015 tukaisubiri Iyo jana umeme pia ukakatika kwa masaa 13.

Leo tena nnapoandika sasa Umeme umekatika saa 01:53 asubuhi hii na kurudi bila shaka ni mpk saa 4 usiku.

Sasa naomba TANESCO watuambie kuna nini kinaendelea mgao huu miezi mitatu mfululizo?

Najiuliza kwanini Mgao bila taarifa?

Hapa mimi kama mimi nimeshapata Hasara ya zaidi ya mil 4 tangu mgao Uanze Mkoa wa Morogoro, ikiwepo wilaya ya kilosa. Na kuna taarifa, sio hapa MOROGORO tu, maeneo mengi nchini YALIOPO PEMBEZONI yana mgao mkali sana wa masaa kati ya 16-24

Najiuliza Pia waandishi wa habari mpo wapi Kuutetea Umma ulioko pembezoni ya miji mikubwa kwa mateso haya?

Yan mnaandika tu mgao wa UMEME wakikosa umeme wakazi wa Dar es salaam. Kwann? Au hamjui haya?

Nadhan Tunahtaji kufikiri pamoja. TANESCO tangazeni mgao Tujue, tujipange tununue Majenereta. Mna turudisha nyuma kimaendelo na maisha yamekuwa ghali maradufu.

Mashine za unga zinasaga usiku wa manane, Wachoma mageti hawalali wanakesha kumalizia tenda za watu. Samaki wangu wa mil 3 waliozea kwenye freezer 😡 nikifika hapo. Huwa natamani kufanya lolote. (hasira sana). Maana nakaribia kufiliska.

Eeh Mungu Nisaidie!
NOTE: umeme huu una katika kila siku iendayo Kwa Mungu. Na hatujui hatima yetu

Tafadhali Moderator msiunganishe uzi huu, unahtaji Majibu yakina sana, hasara tunayopata kwa mgao huu ni kubwa kuliko propaganda zinazofanya na Tanesco.
.POLENI NDUGU ZANGU WA KILOSA.nilikuwa huko miaka ya 2012/13.mi naona maeneo ambayo ccm imeweka mizizi ndo mgao mkali sana.vipi sasa huko kichangani?
 
Hizi ni sababu zinazojitosheleza kuwapiga chini ccm mwezi ujao.Shughili nyingi za kiuchumi zimekwama kutokana na kusekana kwa Umeme.CCM miaka yote hiyo mpo madarakani,mmeshindwa kutupatia umeme wa uhakika?
 
Ni aibu zaidi pale waziri was nishati na madini anapoutangazia umma ktk tv kuwa tatizo la umeme litakuwa historian,siku mbili baadae tatizo linarudi palepale!....ccm no majanga
 
Tanesco inakera sasa na haya mambo ya kampeni hatupati fursa kupata uhondo wa habari

We dada! We umuhimu wa umeme kwako ni kupata uhondo wa kampeni? Kwa watu wa namna yako raisi hata wawe watatu bado naendelea itakuwa hadithi. Punguza kufata mkumbo na angalia taarifa za Tanesco
 
Wakimaliza kuunganisha mfumo wa gesi wataanza kudai miundombinu chakavu. Nchi hii sababu za utendaji mbovu hazikosekani....!!
 
Hapa yawezekana kuna kamchezo nyuma ya pazia.

Ili mzoee siku ya kupiga kura Masanduku ya Goli la Mkono yaingizwe kwenye vituo vya kupigia kura na zoezi la kuhesabu lifanyike Gizani Goli la Mokono litoe matokeo ya gizani kwa msaada wa Tanescoccm.
 
We dada! We umuhimu wa umeme kwako ni kupata uhondo wa kampeni? Kwa watu wa namna yako raisi hata wawe watatu bado naendelea itakuwa hadithi. Punguza kufata mkumbo na angalia taarifa za Tanesco

Kwa hiyo unataka kusema sababu ya wewe kuhitaji nishat ya umeme inapaswa kufanana na wengine. Kamwe hatuwez kuwa sawa, mi ntahitaji umeme kwa ajili kuku wangu, mwingine atahifaji kuhifadhi samaki wasioze, mwingine aangalie tv nk. We unataka watu wote wawe sawa, akili ya wapi hii.
 
We dada! We umuhimu wa umeme kwako ni kupata uhondo wa kampeni? Kwa watu wa namna yako raisi hata wawe watatu bado naendelea itakuwa hadithi. Punguza kufata mkumbo na angalia taarifa za Tanesco
hebu tuwekee hizo taarifa za tanesco tuelewe,si unajua nchi ya malofa hii.
 
Kwa hiyo unataka kusema sababu ya wewe kuhitaji nishat ya umeme inapaswa kufanana na wengine. Kamwe hatuwez kuwa sawa, mi ntahitaji umeme kwa ajili kuku wangu, mwingine atahifaji kuhifadhi samaki wasioze, mwingine aangalie tv nk. We unataka watu wote wawe sawa, akili ya wapi hii.
Mi nataka umeme nione isidingo tu,baas
 
Halafu hawahawa ndio wanataka kutetea nafasi zao katika uchaguzi huh huku wakituambia

Eti....."HAPA KAZI TU"

Mimi hata sijui hii kauli mbiu huyu jamaa Mr Magufuli na CCM yake alikurupuka nayo toka wapi maana inaonesha wazi kuwa haijafanyiwa utafiti!!

Mtasemaje kuwa "hapa kazi tu" wakati watu wenu wamekaa bila kazi, wanashinda hawafanyi kazi kwa sababu nyenzo za kufanyia kazi kama umeme havipo na uliopo hauna uhakika (unreliable)?

Inasikitisha sana kwa sababu, siku mbili zilizopita nilitembelea mji mdogo wa Isaka ulioko wilaya ya Kahama.

Wakazi wa pale wanategemea maji ya pampu za machine zinazosukumwa kwa nguvu ya umeme. Umeme una siku nyingi haupatikani, ukija masaa machache unasukuma maji kidogo kwenye matenki wakichota watu wachache tu yanaisha na hivyo sehemu kubwa ya raia wanakosa maji!

Pale pia pana machine nyingi za kukoboa nafaka kama mahindi na mpunga. Zote zimefungwa na vijana wengi ambao huzitegemea kujiingizia kipato cha kupitisha siku hawana kitu, wamelala tu!

Halafu tunaambiwa "ni kazi tu"... Hakuna kitu, ni uongo na ulaghai mtupu labda ndo maana kujipachika logo na motto ya wengine

M4C eti Magufuli For Change!!!
 
Kwa hiyo unataka kusema sababu ya wewe kuhitaji nishat ya umeme inapaswa kufanana na wengine. Kamwe hatuwez kuwa sawa, mi ntahitaji umeme kwa ajili kuku wangu, mwingine atahifaji kuhifadhi samaki wasioze, mwingine aangalie tv nk. We unataka watu wote wawe sawa, akili ya wapi hii.

Hizi zako bora sana na za kimaendeleo zaidi. Mungu akubariki kwa kuwaza Kazi hizi
 
Hivi hakuna namna yakuwashtaki hawa watu, hii imekuwa zaidi ya karaa, ni ujinga uliopitiliza hatuwezi kufanywa kama watoto wadogo kiasi hiki. Yani kila siku nikudanganywa tu
 
LUKU



Cost TZS 14,041.97
Service Charge TZS 11,040.00
VAT 18% TZS 4,514.75
EWURA 1% TZS 250.82
REA 3% TZS 752.46
TOTAL TZS 30,600.00
Cheki makato hayo halafu mnasema mnatoa huduma.Subirini tarehe 25/10 mtatutambua


Inategemea na vigezo vya hiyo huduma. Nijuavyo mie wanafanya Biashara na TANESCO ndio wanauza umeme bei nafuu ukilinganisha na nji zinazo tuzunguka
 
Nakumbuka kupitia vyombo vya habari tulijulishwa Tanesco wako ktk hatua za mwisho kuunganisha gesi ili umeme kukatika iwe ni historia, lakini hilo limeshindikana, sijui tatizo gani tena. Hatuna umeme muda mwingi mchana na usiku. Tanesco toeni taarifa yenye uhakika.

We VP mitambo ya umeme haijazinduliwa itatumikaje kama cyo wanakupotosha?kawaida ya serekali ya maccm yafanye uzinduzi ili 10% zipatikane .
 
Tatizo Lilikuwepo Kweli Kama Mlivoambiwa Kutokana Na Gas Ya Mtwara Kuingizwa Kwenye System Na Juzi Ndo Mashine Ziliwashwa,na Bado Wanaendelea Kuweka Vitu Sawa.Kama Ukiangalia Nusu Na Robo Ya Tanzania Kulikuwa Hakuna Uhakika Wa Umeme Kabisa Lakini Kuanzia Jana Na Leo Tatizo La Umeme Limepungua Katika Maeneo Mengi.Matatizo Katika Maeneo Mengi Yanatokana Na Kubadilishwa Mifumo Na Miundombinu Mf.Nguzo,transfoma Nk.Na Tusihusishe Siasa Na Hali Ya Tanesco Inayoendelea.
 
Back
Top Bottom