Binadamu tunatakiwa kuishi maisha kulingana na uhalisia wake. Tukitaka kuishi maisha ya kufikirika; basi tutambue fika msongo wa mawazo, maamuzi ya kukurupuka, chuki na hasira zisizo na kichwa wala miguu haziwezi kutuacha salama.
Ifikie wakati tuukubali ukweli ili maisha nayo yaendelee. Siyo lazima ufanye kazi ya ndoto yako! Ni wachache sana waliopata hiyo bahati. Hivyo ukipata kazi ya kukusaidia kuishi na kuisaidia familia yako, mshukuru Mungu! Siyo kazima uoe/uolewe na mwanamke/manaume uliyemuota ndotoni! Ukimpata mtu sahihi wa kuishi naye, mshukuru Mungu!