Jifunze Kusema HAPANA: Linda Muda na Malengo Yako

Jifunze Kusema HAPANA: Linda Muda na Malengo Yako

Dr Arshavin

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
26
Reaction score
80
Jifunze kusema HAPANA.

Kusema HAPANA ni muhimu kwa sababu si kila kitu kinachokuja kwenye maisha yako kinafaa kubeba muda wako, nguvu zako au akili yako.

Watu wengi wanachoka, wanapoteza focus na wanabaki nyuma si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawawezi kusema hapana.

Ukishindwa kusema hapana, utaanza kuishi maisha ya kuwafurahisha wengine kuliko kujenga maisha yako mwenyewe. Kila mtu atataka kipande cha muda wako, nguvu zako na attention yako.

Mwisho wa siku unajikuta umebaki umechoka lakini hujajenga chochote kikubwa kwa ajili yako.

Kusema hapana kunakulinda dhidi ya distraction.

Kuna marafiki, mazingira, starehe na hata opportunities ambazo zinaonekana nzuri, lakini zinakuondoa kwenye direction yako.

Watu wenye maono makubwa wanajua kwamba kila “ndiyo” kwa kitu kisicho muhimu ni “hapana” kwa ndoto yao.

Pia kusema hapana kunaonyesha kwamba unajiheshimu.

Ukiweza kuweka boundaries, watu watajifunza kuheshimu muda wako, kazi yako na malengo yako.

Usipoweka mipaka, dunia itatumia maisha yako kama sehemu ya kutatua matatizo ya wengine.

Kwa sababu kila kiwango kipya cha maisha kinahitaji uwezo mpya wa kuchagua nini kiingie kwenye maisha yako na nini kibaki nje.

Hapana nyingi ni ndio kwenye kufikia malengo yako.

#LifeIsMindset
 
Nakubaliana nawe bila shaka .
Nikiwa na ushuhuda wa hayo ulio yasema matokeo na ndio kwa kila kitu.
Lakini binafsi naona kusema hapana ni mbaya sana, ni sawa na kumfungia mtu mlango.

Sote binadamu tunahijiana, hamna hata mmoja alie mkamilifu, kusema hapana kwa anae kujia ni sawa na kumfungia mlango anae kugongea.

Kadhalika pia kesho nawe kuna namna utahitahitaji ndio mtu, jaribu kuwaza uambiwe hapana wakati unahitaji ndio.
 
Mimi nimesema

Hapana sex kabla ya ndoa 😎
 
Back
Top Bottom