- Thread starter
- #121
kama umefanikiwa una uwezo wasaidie ndugu zako maisha kuna kupanda na kushuka
Mkuu Kill ndugu nawasaidia sana lkn wale wanaostahili kusaidiwa km nlivyowataja hapo juu ya uzi,em rejelea post yng uielewe
kama umefanikiwa una uwezo wasaidie ndugu zako maisha kuna kupanda na kushuka
nimesoma nimekuelewa hata mimi hayo matatizo yalinikuta lakini namshukuru Mungu nilipofanikiwa kidogo niliwasaidia wote uamuzi upo juu yako naheshimu maamuzi yako ukiamua kuwaidia wote sawa ukiamua kuwaidia waliokusadia ni sawaMkuu Kill ndugu nawasaidia sana lkn wale wanaostahili kusaidiwa km nlivyowataja hapo juu ya uzi,em rejelea post yng uielewe
Tatizo lako hujafika wala huyajui maisha ya uingereza. ....haihitaji usome saaaana ndio ufanikiwe. ...kuna kazi za kawaida ambazo hazihitaji kusoma sana lkn zinalipa ile mbaya. .....unaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kujibana ulaya lkn ukafanya ya maana sana bongo.
Wengi wanaosema maisha ya ulaya maguuuumu kwanza waulize wapo nchi gani ya ulaya? Waulize wana vibali vya kuwaruhusu kufanya kazi fulltime?..sio mtu anaishi kama mwanafunzi ukafananisha maisha yake na mtu mwenye indefinitely leave to remain
"Tenda wema uende zako, usingoje shukurani".
nimesoma nimekuelewa hata mimi hayo matatizo yalinikuta lakini namshukuru Mungu nilipofanikiwa kidogo niliwasaidia wote uamuzi upo juu yako naheshimu maamuzi yako ukiamua kuwaidia wote sawa ukiamua kuwaidia waliokusadia ni sawa
mkuu kwa ushauri wangu wale ambao wapo maofisini wana uwezo usiwasaidie ila wale ambao hawana uwezo wapo nyumbani hawana hata ajira ukiwasaidia hata Mungu atakuongezeaKwanza pole mkuu kwa kukumbana na matatizo yanayolingana na ya kwangu,lkn vilevile hongera kwa kusamehe na kuwasaidia wote. Ni uamuzi mzuri pia lkn sasa kwa mm inakuwa ngumu kutokana na hawa ninao wazungumzia hapa ni wale wanaoshinda ofisini kila leo lkn wanapoona nimetuma ela kwa wazazi wangu na zingine kwa wale ndugu ambao hawana ofisi na wasiojiweza kabisa. Utaona na wao wanaanza kurusha mikuki ya kufatana tena utafikir wameambiana mara bamkubwa anaeshinda ofisi karusha mkuki wa kuomba dola 500 wakati mi najiandaa kuukwepa unasikia tena sim mjomba anapiga mkuki wa dola 1000 wakati tena najipanga kuupangua mara bamkuu mungine anajiandaa kuufyatua mkuki wa mbavu huyu sasa anaweza kukwambia umtumie dola 2500 eti asafishe ofisi ake maana imechakaa, yan ilimradi wahakikishe ww hupumui wala humeki ki2 na ktk hao wale au yule utakaemwambia sina hizo ela kwa sasa basi ndo wanaanza majungu na kusahau kuwa wakati mm nlipohitaji msaada kwao walinisengenya na kusahau kuwa mm ni mtoto wa ndugu yao. Afu basi wasingenisaidia mm wakamsaidia ndugu yao lkn walimwaacha mzee wangu hadi alizeeka kabla ya mda wake
Tatizo maisha ni mzunguko hata wewe usijione kuwa umEshaukata.jana wao walikuwa vizuri we uko vibaya,leo wao wako vibaya we uko vizuri, kesho wao au watoto wao watakuwa vizuri wewe utakuwa vibaya.
mkuu kwa ushauri wangu wale ambao wapo maofisini wana uwezo usiwasaidie ila wale ambao hawana uwezo wapo nyumbani hawana hata ajira ukiwasaidia hata Mungu atakuongezea
Unajuaje kama Sijawahi kufika nchi za Kibepari? Halafu embu nitajie hiyo kazi ambayo utafanya Nchi za Kibepari ukawa na Maisha mazuri huko na vile vile ukajenga nyumba mbili Bongo na kununua Magari bila ya kuwa na Utaalamu unaohitajika!
sasa mbona uliyoyaandika tu hapa yanajibu swali ulilouliza hapo juu??!!! Fyi watanzania wengi wanafanya unskilled labor uk na vitu vidogo kama nyumba na magari wanayo....
Umezaliwa katika familia inayojiweza then mlikuwa mnashinda njaa!!
Story yako ungeweza kuiandika bila kutaja wabeba box na wa maofisini...sioni uhusiano zaidi ya generalization isiyo sahihi...
Hali zenu wanajamvi?
Ndugu zng leo nimekuja na mambo ambayo yamenitokea mm na naamini kabisa yashawai kuwatokea na wengine kuhusu hawa ndugu zangu vitambi manager tuliowaacha bongo.
Kwanza kabisa ningependa nije na kahistoria kafupi ili nieleweke vzr. Mm nlizaliwa ktk ukoo wa watu wanaojiweza. Yani ktk ukoo wetu naweza kusema kuwa 79 ni ya watu waliosoma na ambao kutokana na shule zao wengi wao sasa wanafanya kazi ktk maofisi mbalimbali,wapo wanaofanya kazi ktk ofisi za serikali,wengine ofisi za makampuni na wengine ofisi zao binafsi.
Katika kipindi chote cha mafanikio yao watu hawa wanaojiweza wameshindwa kuwa msaada kwa wale wenye familia zisizojiweza.
Wazazi wangu ni moja ya familia isiyojiweza ktk ukoo wetu lkn hakuna mt aliejitolea kutusaidia. Tulishinda njaa,wakati wenzetu vyakula viliharibikia frijini.
Nlikosa hela ya kulipa shule wakati wengine walikuwa wanajenga heshima baa na kwenye kumbi mbalimbali za starehe. Mwaka 1999 nilibahatika kwenda ng'ambo kwa mpango wa baba angu mdogo fulani anaefanya kazi katika ubalozi wa Norway.
Nilipofika uku ng'ambo kwa kuwa nillikuwa bado nina umri mdogo nilipata mfadhili ambae alinipeleka shule na baada ya shule nikapata kazi ambayo wananilipa vizuri tu kulingana na elimu yangu niliokuwa nayo.
Sasa nimejenga bongo nyumba kubwa tu, moja nimepangisha,nyingine nimewapa wazazi wangu. Nimeshatuma gari 2, moja la wazazi,lingine la yule baba yangu mdogo aliyenifanyia mpango wa kwenda nje.
Na nimekuwa nikituma vihela kidogo kwa baadhi ya ndugu zangu ambao hawana uwezo. Sasa tokea ninunue nyumba na magari na kutuma hela bongo,nimekuwa nikipigwa mikuki inayotoka kila pande ya nchi.
Mara mjomba mara shangazi mara bamkubwa mara binamu na wengi wao ni wale wanaofanya kazi kwenye maofisi mbalimbali na wameshasahau kuwa hata mimi wakati nipo TZ nilihitaji msaasa wao ukiwemo wa shule wakaninyima,lakini leo full lawama kwamba toka nifike ulaya eti siwajali.
So nitawajali vipi wakati hata wao hawakunijali? Hii ndo inanifanya niamini kuwa bora maisha ya mbeba mabox ulaya kuliko ya mshinda ofisini bongo au nyi mnaonaje waungwana wenzngu,am i wrong?
Tusubiri wenye wazoefu waje...
NOTE; natafuta bachelor mbeba box vumbi la bongo limenichosha!
wewe hacha ujinga kabisaa, dunia inazunguka na maisha hayana formla hata kidogo, pamoja na kuwa na vigali viwili na tu nyumba bado kumbuka vinaweza kutoka ukabaki kuwa ni mtu wa kuitaji msaada tena kwao. watu wengi tumewaona na mimi nina ushahidi sana kwa hilo. hivyo unacho tatikiwa kufanya ni kutolipiza kisasi ni kuwa penda tu na pale panapo bidi kuwasaidia uwasaidie bila hata kuwatangaza hapa mtandaoni. kadiri utakavyo wasaidia ndivyo Mungu atazidi kukubariki zaidi. haya mambo ya kusema hawakunisadia, huyo Mungu aliye kusaidia wewe kupitia mtu mwingine, ndiye Mungu anaye weza kuwainua wao wakawa msaada zaidi kwako, kuliko ule ulio ukosa mwanzoni. hachana na kisasi kabisa. kwa imani ya wakristo kwenye biblia kitabu cha mithali inasema, ASIRA UKAA KIFUANI MWA MPUMBAVU. Samehee kabisa