Nime staafu rasmi.

Nime staafu rasmi.

Naunga mkono hoja bila kipingamizi. Michango ya harusi bora ukanywe bia na marafiki watakukumbuka mda wote.!
 
Kujitoa mbona rahisi sana. Ni maamuzi tu na kutokua na mshipa wa aibu. Siku hizi harusi unaandaa mwenyewe then unaalika watu wako wa karibu. Kupunguza gharama unawaambia harusi ya leo ni ya kilokole so BIA hazitakuwepo hivyo nyote mnakaribishwa.
 
Hayo ndiyo maamuzi magumu na ya busara kaka ambayo tunapaswa kukuiga mkuu.
Naahidi kukuunga mkono.
 
nakuunga mkono Speaker hata mm sitahudhuria
harusi yangu ilikuwa simple na sikua na kikao hata kimoja
hadi leo ndugu na jamaa wananishangaa lakini nshawaeleza
sitachangia labda shule,matibabu lakini sio sherehe
bora kuchukiwa lakini kimaendeleo unasonga mbele.
utashangaa kijana anataka harusi ya mil 20 wakati mfukoni ana laki 2 na anaishi nuyumba ya kupanda
 
Kujitoa mbona rahisi sana. Ni maamuzi tu na kutokua na mshipa wa aibu. Siku hizi harusi unaandaa mwenyewe then unaalika watu wako wa karibu. Kupunguza gharama unawaambia harusi ya leo ni ya kilokole so BIA hazitakuwepo hivyo nyote mnakaribishwa.

ha ha ha,naskia harusi za kilokole watu hawachangii
hela nyingi ni kweli?
 
Hayo ndiyo maamuzi magumu na ya busara kaka ambayo tunapaswa kukuiga mkuu.
Naahidi kukuunga mkono.

Kweli Fukara mwenzangu,inabidi tuupinge ufukara na makando kando
yanayo leta ufukara kwa nguvu zote
 
Last edited by a moderator:
Speaker mpwa hapa kwetu walinuna. Soda za laki mbili walikunywa hadi wakabakiza wenyewe. Gharama sio kubwa harusi ya kilokole. Lamsingi ni kuelewana tu na mwenz wako.
 
Mkielewana na mwenzako mambo rahisi sana,
Mnakwenda asubuhi kwa kasisi wenu, mnavishana pete na kutoa viapo, huyo nyumbani kwenu, kama ni siku ya kazi, unakwea daladala na jioni unakwenda kula kiti moto na best man wako. Hapo hata laki tatu haijaisha. Nina miaka mitano sasa sijashiriki vikao kabisa. Yaani kadi peke yake unapata kama nane hivi na mama chanja naye ana kadi kumi za kitchen party, na hiyo ni kila mwezi.

Nikibanwa huwa nachangia, lakini kwa mbinde.Sherehe ikiwa mbali kama 5km na kuendelea siendi vile vile.
 
Kinachoniudhi kwenye michango ni kuweka viwango, minimum laki 3...........
kuna maharusi wengine wanataka kununua hadi pete zao kwa michango ya watu. au wengine ni wa hali ya kawaida tu lakini wanataka kukufuru kwenye harusi/sendoff etc then wanarudi kwenye umasikini, what is the point?
na tabia mbaya tunayo wadada, yaani anataka harusi/sendoff yake iwe gumzo kwa rafiki zake kwa miaka kadhaa. yaani wanataka mambo makubwa sana, madai yao haiji mara 2. Speaker mi nakuonea huruma tu unavyopanga harusi ndogo, wenyewe wadada wa karne hii wanasema harusi inachaguliwa na mdada............... kama atataka kubwa ujue imekula kwako. sisi enzi zetu hata hujui huko wameandaa nini, la muhimu lilikuwa umehudhuria mafundisho ya ndoa kanisani, umeletewa gauni la harusi, umekuja kuchukuliwa kwenda saluni na kanisani, ya huko ukumbini utayakutia huko. siku hizi kila kitu kinapangwa na mdada, kuanzia k/party, sendoff, harusi.......... bibi harusi anaanza kugombana na mawifi kuanzia kwenye maandalizi ya harusi.........
Kila la heri, mimi sina ubavu wa kujitoa ingawa ninaowachangia hakuna hata aliyenichangia
 
Last edited by a moderator:
kwa mda mrefu sijafika jukwaani.....leo kuna mada kali kweli...uamzi ni wako mkuu uheshimu
 
Dah, nilikuwa natamani tuongezeke hatimaye wenye msimamo kama wangu tanaongezeka, hongera mkuu, you are welcome
 
Halafu kali zaidi umechanga, harusi inafanyika Mbezi Garden, Mbezi Beach halafu wewe unakaa Mbagala Charambe na huna hata kimkweche!!

Kuna Tax driver mnaeshimiana hapo ndio inabidi umuandalie 50,000/= ndio akupeleke na kukurudisha tena kwa heshima tu maana waiting charge yake hapo huiwezi.

Ila kwa busara zangu mimi sijari nina mkweche wangu au sina kwa distance za namna hiyo usinitajie kuhudhuria, maana hata juzi nimeukacha mnuso wa Dezo kumpongeza mama Fulani hivi amestaafu lakini nilipopiga hesabu ya wese nikaona bora nijigharamie mwenyewe bia mtaani na kuondokana na risk za barabani kurudi usiku kisa bia za bure.
 
Pole mkuu, kumbe ulikuwa bado unachangia tu, milishapiga ban siku nyingi hivyo vitu

Tena bora ningekua nimeoa nika faidi michango.
Sijaoa,na sitegemei kuoa ndani ya miaka 4 ijayo,...lakini hela nilizo
kwisha changa iiiiiiiiiii,natamani kulia.

Sio tu ni hela zina niuma,lakini kufuru za sherehe sioni umuhimu wake
kwa maisha ya kitanzania ya sasa,naskitika kuchangia ufujaji wa mali na
laana kwa wanandoa.
 
my wedding was planned 1moth only with my poket only sikuwa na wapambe,sijui watoto blabla ndugu wakalazimisha wakaambia jichangeni wenyewe sichangii chochote

speaker oyeeeeeee...Amsterdam upo juu vibaya mno. tumezidi kuendekeza anasa za kipuuzi...
 
Kinachoniudhi kwenye michango ni kuweka viwango, minimum laki 3...........
kuna maharusi wengine wanataka kununua hadi pete zao kwa michango ya watu. au wengine ni wa hali ya kawaida tu lakini wanataka kukufuru kwenye harusi/sendoff etc then wanarudi kwenye umasikini, what is the point?
na tabia mbaya tunayo wadada, yaani anataka harusi/sendoff yake iwe gumzo kwa rafiki zake kwa miaka kadhaa. yaani wanataka mambo makubwa sana, madai yao haiji mara 2. Speaker mi nakuonea huruma tu unavyopanga harusi ndogo, wenyewe wadada wa karne hii wanasema harusi inachaguliwa na mdada............... kama atataka kubwa ujue imekula kwako. sisi enzi zetu hata hujui huko wameandaa nini, la muhimu lilikuwa umehudhuria mafundisho ya ndoa kanisani, umeletewa gauni la harusi, umekuja kuchukuliwa kwenda saluni na kanisani, ya huko ukumbini utayakutia huko. siku hizi kila kitu kinapangwa na mdada, kuanzia k/party, sendoff, harusi.......... bibi harusi anaanza kugombana na mawifi kuanzia kwenye maandalizi ya harusi.........
Kila la heri, mimi sina ubavu wa kujitoa ingawa ninaowachangia hakuna hata aliyenichangia

hapo kwenye red hapo...umenipa raha...msema kweli mpenzi wa Mungu...sio wote tunaochangia tunapenda kufanya hivyo bwana...
 
Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea "Mwanza", na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharami...a shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni MOSHI utatakiwa umpeleke huko "Kibosho-Umbwe Onana". Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane (Ba Mkwe, Ma Mkwe, Ba Ubatizo, Ma Ubatizo, Mjomba, Shangazi, Kaka mtu na Dada mtu) kutoka Mwanza uwalete Moshi. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

5. MAHARI ndio topic tatanishi inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: “We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa bana!!

10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!

11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!

12. “Baby, rafiki yangu Maimartha alinunua gauni la harusi China yani lilimpendezajee” 700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 3.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu “Mangi eeeeh, Sasa tunavunja lini kamati?” Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!

25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 still poor!
 
Nimependa ulivyofanya huo mchanganuo mkuu!
 
Kinachoniudhi kwenye michango ni kuweka viwango, minimum laki 3...........
kuna maharusi wengine wanataka kununua hadi pete zao kwa michango ya watu. au wengine ni wa hali ya kawaida tu lakini wanataka kukufuru kwenye harusi/sendoff etc then wanarudi kwenye umasikini, what is the point?
na tabia mbaya tunayo wadada, yaani anataka harusi/sendoff yake iwe gumzo kwa rafiki zake kwa miaka kadhaa. yaani wanataka mambo makubwa sana, madai yao haiji mara 2. Speaker mi nakuonea huruma tu unavyopanga harusi ndogo, wenyewe wadada wa karne hii wanasema harusi inachaguliwa na mdada............... kama atataka kubwa ujue imekula kwako. sisi enzi zetu hata hujui huko wameandaa nini, la muhimu lilikuwa umehudhuria mafundisho ya ndoa kanisani, umeletewa gauni la harusi, umekuja kuchukuliwa kwenda saluni na kanisani, ya huko ukumbini utayakutia huko. siku hizi kila kitu kinapangwa na mdada, kuanzia k/party, sendoff, harusi.......... bibi harusi anaanza kugombana na mawifi kuanzia kwenye maandalizi ya harusi.........
Kila la heri, mimi sina ubavu wa kujitoa ingawa ninaowachangia hakuna hata aliyenichangia

Nime furahi sana kwa kufunguka kwa ukweli wako wote.
Ni kweli,bibi harusi ndo wana panga kila kitu,lakini ninacho jipendea ni
kwamba siwezi kujionesha kwa binti kwamba mimi ni mtu wa 1M wakati nina laki1 tu.

na huwezi nilazimisha nitumie laki1 wakati nina elfu50,hayo lazima atayafaham/ana ayafaham
kabla ya ndoa so hamna miujiza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom