Nime staafu rasmi.

Kutokana na sababu zilizo "ndani" ya uwezo wangu,nafurahi
kuwatangazi ndugu,jamaa na marafiki wote ninao wafahamu na wale
nisio wafahamu kwamba:-

1.Sitashiriki katika kikao chochote cha harusi ya yeyote yule.
2.Sitatoa mchango wa sherehe yoyote ile,iwe harusi,kipaimara,sendoff etc.
3.Sitaomba mchango kwa ajili ya chochote kati ya hivyo hapo juu ambavyo vitakua vina
nihusu mimi.

Lakini,likizo yangu hii haimaanishi kwamba sitasaidia wala kushiriki katika
shughuli za mazishi (kuchangia mazishi),harambee ya kupeleka watoto shule,
harambee ya kumpeleka mgonjwa hospitali kwenye matibabu.

Uamzi huu unatokana na ANASA zilizopo kwenye maeneo niliyo yapiga BAN kwani
hela ninazo toa zinatumika kulaani "FURURE" ya yeyote anae fanyiwa sherehe hiyo.

Mimi nina mwaka sasa hivi, na kuna best friend wangu anaolewa kaniomba mchango; nikamwambia simpi saana nitampa zawadi.

Ofisini kuna dada mmoja anaumwa umwa, baada ya kumuona nimempiga msimbazi 2 yaani haamini; nafikiri haelewi kwanini nafanya hivyo. I am into education, health restoration na misiba tu (ambayo mtu hawezi plan before).

Welcome on board Speaker!
 
Last edited by a moderator:
Uamuzi wako uwe wa dhati, na wengine wakuunge - labda polepole kansa hii itaanza kupungua Tanzania.

Ita pungua tu.
We jiulize kwa kutumia mifano hii.

1.a) Kwanini ukitaka kufanya harusi watu wana changia sana?
b)Kwanini ukitokea msiba,hata utake kwenda kuzikwa INDIA watu wata changa na utaenda.

2. a) Kwanini ukitaka kwenda shule ukaomba mchango hakuna wa kukupa?
b)Kwanini ukiwa unaumwa,hata daktari hakutibu bila hela kutoa hela kwanza,wala ndugu hawatoi hela,lakini ukifa hata daktari anaweza kukusafirisha hadi kwenu ukazikwe?

Harusi ni sehemu za kudanganyana kwamba tuna pendana,ila ukweli wake utaupata kwenye mazishi,HATUPENDANI.
 
Basi wenzio watakukamata kwenye matatizo,walimwengu ni ngumu sana kuwakwepa.

Wata kwepeka tu,nashukuru Mungu najua sana kula na kipofu aisee.
Ila mchango wangu kwa ajili yaa harusi hawapati NG'OOOO
 
nimependa mawazo yako_ingawa kwenye utekelzaji ni ngumu kidogo.
 
Mimi nina mwaka sasa hivi, na kuna best friend wangu anaolewa kaniomba mchango; nikamwambia simpi saana nitampa zawadi.

Ofisini kuna dada mmoja anaumwa umwa, baada ya kumuona nimempiga msimbazi 2 yaani haamini; nafikiri haelewi kwanini nafanya hivyo. I am into education, health restoration na misiba tu (ambayo mtu hawezi plan before).

Welcome on board Speaker!

Nime karibia sana tu.
Naamini ninaweza sana huku,maana my mum ni mchezaji mzuri wa hii
platform ya kukwepa MICHANGO YA HARUSI NA ANASA ZINGINE.

The good thing ni kwamba hawawezi kukuchukia,coz wataona huchangii harusi lakini
una mnunulia bibi/bwana harusi Biblia/Quran,....una mpa mtoto wa flani ada,...lazima watajua tu.
 
Last edited by a moderator:
Hii ni thread ambayo nimegawa like za kutosha_kutokana na umuhimu na uzito wake...lo!
 
I strong support you, kwa sababu Watanzania tumekuwa tunashabikia vitu unnecessary, na ningependa nikupe ushuhuda hivi vikao vya harusi ni benefit kubwa sana kwa baadhi ya watu, kuna mtu harusi ikiwa na bajeti nzuri anatengeneza mpaka million 3 za kuweka mfukoni kwake kwa kugawa tenda za vyakula vinywaji na mapambo.

Kwa uzoefu wangu nimekuja kugunduwa harusi kwa maana ya kitu simple na kuadhimisha maagano yenu shilling millioni 5 ni pesa inayotosha sana kufanya hiyo shughuri na gharama hizi zinapaswa kubebwa na bwana harusi na familia yake. huu ni upuuzi ambao utaendelea kuwagharimu Watanzania unless mtu mmoja mmoja aseme sasa imetosha kama alivyofanya Speaker.
 
ha ha ha,utatoka tu.
Cha kushangaza wasio na HELA ndo wahudhuriaji na watoaji wakubwa wa michango ya harusi.

unazidi kuumiza moyo wangu ujue!ah niache bana hapa nishatoa wa ya kitchen party miwili na sare za kitenge juu!
 
I strong support you, kwa sababu Watanzania tumekuwa tunashabikia vitu unnecessary, na ningependa nikupe ushuhuda hivi vikao vya harusi ni benefit kubwa sana kwa baadhi ya watu, kuna mtu harusi ikiwa na bajeti nzuri anatengeneza mpaka million 3 za kuweka mfukoni kwake kwa kugawa tenda za vyakula vinywaji na mapambo.

Kwa uzoefu wangu nimekuja kugunduwa harusi kwa maana ya kitu simple na kuadhimisha maagano yenu shilling millioni 5 ni pesa inayotosha sana kufanya hiyo shughuri na gharama hizi zinapaswa kubebwa na bwana harusi na familia yake. huu ni upuuzi ambao utaendelea kuwagharimu Watanzania unless mtu mmoja mmoja aseme sasa imetosha kama alivyofanya Speaker.

Tumefanya kitu simple cha mil3 recently na wageni wachache tu (120) bila kumchangisha yeyote and it turned out to be great party.

Kwenye bold, hiyo hadi inachefua.
We must change, vitu vingi vipo ndani ya uwezo lakini waTZ kama viongozi wa wetu wa CCM vipaumbele ndiyo shida yetu kuu. It begins with you!
 
Wata kwepeka tu,nashukuru Mungu najua sana kula na kipofu aisee.
Ila mchango wangu kwa ajili yaa harusi hawapati NG'OOOO
Nadhani kwenu upo peke yako hata ndugu huna hivyo kuyafanya maisha yako kutotegemea mtu,hongera kwa hilo
 
Kifuta jasho:

Namna nzuri ya kukwepa hii michango ya kipuuzi usikubali kuhudhuria kikao cha kwanza cha kuahidi michango, wewe waambie wakuletee kadi halafu unaiweka nyumbani kama mapambo.

Huwezi kuamini kuna kinako nilihudhuria cha jamaa mmoja ile pesa aliyotumia kuwakaribisha watu ili wamchangie ilitosha kabisa kuandaa harusi yake bila kumchangisha mtu, Maana kila aliyehudhuria alipata kinywaji anachotumia bila kupangiwa na chakula kuna catering alikuja kutowa huduma, sasa nikabaki najiuliza kwa nini pesa hii asingeandaa sherehe halafu atualike sisi ili tuje na zawadi tu?

We need to chage our mind set otherwise ni kutafutana ubaya tu.
 
unazidi kuumiza moyo wangu ujue!ah niache bana hapa nishatoa wa ya kitchen party miwili na sare za kitenge juu!

Ha ha ,tena kama nyie wanawake ndo nawa hurumia sana.
Mnachangia kitchen party,sendoff,na mengineyo.

Wakati nyumbani mtoto hakumbuki mara ya mwisho ni lini amevaa
nguo "spesheli",....hakyanani,....kisa?

BIA ZIPOOOOOO
 
Binafsi nakuunga mkono ila si kuacha kabisa kutoa michango. Kama tayari umeoa utajua ni kwa jinsi gani harusi ilivyo na gharama mbaya zaidi utakuta uliwahi kuchangiwa sasa kwa nini usiwachangie wenzio? Kumbuka tunatoa ahadi wenyewe hivyo toa ahadi ambayo iko ndani ya uwezo wako na siyo kufanya mashindano ya nani kaahidi zaidi.
 
I strong support you, kwa sababu Watanzania tumekuwa tunashabikia vitu unnecessary, na ningependa nikupe ushuhuda hivi vikao vya harusi ni benefit kubwa sana kwa baadhi ya watu, kuna mtu harusi ikiwa na bajeti nzuri anatengeneza mpaka million 3 za kuweka mfukoni kwake kwa kugawa tenda za vyakula vinywaji na mapambo.

Kwa uzoefu wangu nimekuja kugunduwa harusi kwa maana ya kitu simple na kuadhimisha maagano yenu shilling millioni 5 ni pesa inayotosha sana kufanya hiyo shughuri na gharama hizi zinapaswa kubebwa na bwana harusi na familia yake. huu ni upuuzi ambao utaendelea kuwagharimu Watanzania unless mtu mmoja mmoja aseme sasa imetosha kama alivyofanya Speaker.

Dah,ndo maana wengine wana ng'ang'ania sana kuwa kwenye kamati za harusi duh.
Kweli mjini shule.
Na bado ule ushamba wa siku hizi,una changa hela,sawa,hata kama nimetoa elf50
na mwisho wa siku harusi budget ni mil30.

Kinacho uma zaidi,sio tu kwamba basi hizo hela anunuliwe zawadi za maana basi,siku hizi utaambiwa
MILIONI TANO YA KULIPIA KIPINDI PALE TBC TUKAOSHE NA SISI.,hela yangu haifanyi
ujinga huo aisee.
 
Tumefanya kitu simple cha mil3 recently na wageni wachache tu (120) bila kumchangisha yeyote and it turned out to be great party.

Kwenye bold, hiyo hadi inachefua.
We must change, vitu vingi vipo ndani ya uwezo lakini waTZ kama viongozi wa wetu wa CCM vipaumbele ndiyo shida yetu kuu. It begins with you!

Nime andaa sherehe yangu itafanyika tarehe 3 november.
Wageni waalikwa ni 60 maximum,na gharama yote ni kama 1.2M.
Hakuna anae changishwa,hakuna na itakua njema coz kila kitu kiko planned kwa ufundi.

Na hata hivo,asipo ridhika mtu hakuna anae nidai,hiyo ni sherehe yangu na wao ni waalikwa.
Uwezo wangu umeishia hapo,ATLEAST SIAZIMI UMAARUFU/UTAJIRI. lol
 
safi,hiyo poa sana Speaker.nikabidhi kazi ya kuwapikia hao wageni wako!utafurahi mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ,tena kama nyie wanawake ndo nawa hurumia sana.
Mnachangia kitchen party,sendoff,na mengineyo.

Wakati nyumbani mtoto hakumbuki mara ya mwisho ni lini amevaa
nguo "spesheli",....hakyanani,....kisa?

BIA ZIPOOOOOO
wala sio utani ila wanangu siwasahau i see ,ila michango ndoa kila siku rafiki yangu na usipoangalia mshahara unaishia huko?
 
Nadhani kwenu upo peke yako hata ndugu huna hivyo kuyafanya maisha yako kutotegemea mtu,hongera kwa hilo

Hilo halikuhusu chalii.
Lakini hata kama niko peke yangu au tuko wengi cha muhimu ni kula nyasi kutokana na urefu
wa kamba yako.
Huwezi kua na 5M bank,unataka kuoa,sawa,afu unataka harusi ufanye kwa 20M.
Zinatoka wapi?
Eti kwangu kwakua mimi kaka yako?Ujinga huo,nenda kanisani,funga ndoa,fanya party ndogo nyumbani
mambo yaishe.

TATIZO LETU NI KUFANYA JAMBO ILI KUJIOSHESHA NA KUFURAHISHA WENGINE.
 
Back
Top Bottom