Nime staafu rasmi.

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Kutokana na sababu zilizo "ndani" ya uwezo wangu,nafurahi
kuwatangazi ndugu,jamaa na marafiki wote ninao wafahamu na wale
nisio wafahamu kwamba:-

1.Sitashiriki katika kikao chochote cha harusi ya yeyote yule.
2.Sitatoa mchango wa sherehe yoyote ile,iwe harusi,kipaimara,sendoff etc.
3.Sitaomba mchango kwa ajili ya chochote kati ya hivyo hapo juu ambavyo vitakua vina
nihusu mimi.

Lakini,likizo yangu hii haimaanishi kwamba sitasaidia wala kushiriki katika
shughuli za mazishi (kuchangia mazishi),harambee ya kupeleka watoto shule,
harambee ya kumpeleka mgonjwa hospitali kwenye matibabu.

Uamzi huu unatokana na ANASA zilizopo kwenye maeneo niliyo yapiga BAN kwani
hela ninazo toa zinatumika kulaani "FURURE" ya yeyote anae fanyiwa sherehe hiyo.

We jiulize kwa kutumia mifano hii.

1.a) Kwanini ukitaka kufanya harusi watu wana changia sana?
b)Kwanini ukitokea msiba,hata utake kwenda kuzikwa INDIA watu wata changa na utaenda.

2. a) Kwanini ukitaka kwenda shule ukaomba mchango hakuna wa kukupa?
b)Kwanini ukiwa unaumwa,hata daktari hakutibu pasipo kutoa hela kwanza,wala ndugu hawatoi hela,lakini ukifa hata daktari anaweza kukusafirisha hadi kwenu ukazikwe?

Harusi ni sehemu za kudanganyana kwamba tuna pendana,ila ukweli wake utaupata kwenye mazishi,HATUPENDANI.
 
Wengi wanaokimbia kama wewe ni wale ambao wameoa karibuni, wanaona mzigo kulipa fadhila!!! Mtu ambaye anatarajia kuoa/kuolewa, na atategemea kuchangiwa, hawezi kuweka kando hili suala la michango. Inauma but unakuwa huna jinsi...ndiyo jumuiya yetu na jamii yetu, ndiyo maisha tuliyoyachagua.
 
Tena bora ningekua nimeoa nika faidi michango.
Sijaoa,na sitegemei kuoa ndani ya miaka 4 ijayo,...lakini hela nilizo
kwisha changa iiiiiiiiiii,natamani kulia.

Sio tu ni hela zina niuma,lakini kufuru za sherehe sioni umuhimu wake
kwa maisha ya kitanzania ya sasa,naskitika kuchangia ufujaji wa mali na
laana kwa wanandoa.
 
hiyo michango huwa inaniuma roho sana huwa naipotezea tu.unakuta kila mwezi unachangia du ,yakwangu sikuomba mtu mchango ili nisijelipa fadhila sikutaka kabisa,
 
Ni jambo bora - japo ungechangia harusi fulani ya ndugu yangu kwa mara ya mwisho.
 
Du!Kujitoa ni ngumu sana,mimi naugulia ndani kwa ndani maana kwa maisha yetu ya kitanzania kujitoa kwenye mambo kama hayo inaweza tokea siku ukakodi watu wa kumzika ndugu yako au hata mke na watoto,jambo hili lina impact kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.
 
Ni jambo bora - japo ungechangia harusi fulani ya ndugu yangu kwa mara ya mwisho.

Ha ha,jana nimeenda kikao flani nikasema hiki ni cha mwisho.
Eti wao single elf60,double laki1,hutaki unaacha.

hapo kuna kadi kama 5 hivi unatakiwa kuchangia,....yaani hii michango michango tu
ya mwezi huu ningeweza nunua gunia 2 za mchele,mahindi mengi tu kwa ajili ya ugali
nikasahau njaa.

MBAYA ZAIDI SINYWI POMBE,NA SODA SINYWI ZAIDI YA 2,AGGGGGHRRRRR hasara tupu
 
Du!Kujitoa ni ngumu sana,mimi naugulia ndani kwa ndani maana kwa maisha yetu ya kitanzania kujitoa kwenye mambo kama hayo inaweza tokea siku ukakodi watu wa kumzika ndugu yako au hata mke na watoto,jambo hili lina impact kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.

Kwenye mazishi na matatizo sawa,ila hizi kufuru zingine SITAKIIIII.
Ninajua nitakavyo wakwepa
 
hiyo michango huwa inaniuma roho sana huwa naipotezea tu.unakuta kila mwezi unachangia du ,yakwangu sikuomba mtu mchango ili nisijelipa fadhila sikutaka kabisa,

Sitegemei kufanya harusi kubwa,itakua ndogo na waalikwa wachache tu.
Naamini hiyo ni budget nitakayo iweza.
 
Sitegemei kufanya harusi kubwa,itakua ndogo na waalikwa wachache tu.
Naamini hiyo ni budget nitakayo iweza.
my wedding was planned 1moth only with my poket only sikuwa na wapambe,sijui watoto blabla ndugu wakalazimisha wakaambia jichangeni wenyewe sichangii chochote
 
Ha ha,jana nimeenda kikao flani nikasema hiki ni cha mwisho.
Eti wao single elf60,double laki1,hutaki unaacha.

hapo kuna kadi kama 5 hivi unatakiwa kuchangia,....yaani hii michango michango tu
ya mwezi huu ningeweza nunua gunia 2 za mchele,mahindi mengi tu kwa ajili ya ugali
nikasahau njaa.

MBAYA ZAIDI SINYWI POMBE,NA SODA SINYWI ZAIDI YA 2,AGGGGGHRRRRR hasara tupu

Uamuzi wako uwe wa dhati, na wengine wakuunge - labda polepole kansa hii itaanza kupungua Tanzania.
 
Back
Top Bottom