Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Safi
 
unaposema Quran ilichukua vitabu vya biblia.. je,ww ushawahi kuisoma Quran ukadhibitisha imecopy toka katika biblia yaani yaliyomo kwenye Quran na Biblia yana fanana? au ww ulidhibitisha vp ya ndani ya Quran yanafana na yaliyo ndani ya biblia.?
Jibu swali, Torati ipo kwenye quran haipo? Kama unakubali ipo basi ni copy n paste na hakuna cha kushushwa kutoka wapi sijui..
 
Jibu swali, Torati ipo kwenye quran haipo? Kama unakubali ipo basi ni copy n paste na hakuna cha kushushwa kutoka wapi sijui..
Torati haipo kwenye Qurani, wala Zaburi wala Injiri.
Kama ipo iwekwe hapa tuione.
Mzizi wa Torati ni Amri Kumi alizopewa Musa.
Kwenye Qurani hazipo.
 

Mbona umerukia "kuchomoa"? Kwani nilichomeka wapi?

Mafundisho mema kabisa hayo, hapo tunafundishwa kuomba dua, ndio Waislam tukiomba dua na sisi wenyewe tunajiombea "rabbana 'ghfirlana..."

sasa umeona sura inaitwa Muhammad ukapachika reference juu hapo kupotosha watu? Upoyoyo huo. Huo ni ujumbe kwetu sote, hakuna jina la mtu hapo. Unakuhusu wewe pia huo ujumbe kijana, Qur'an ni kwa walimwengu wote siyo kwa watu fulani tu. Kumbuka hilo.
 
Torati haipo kwenye Qurani, wala Zaburi wala Injiri.
Kama ipo iwekwe hapa tuione.
Mzizi wa Torati ni Amri Kumi alizopewa Musa.
Kwenye Qurani hazipo.
Hizo hazipo popote isipokuwa zimetajwa kwenye Qur'an. Biblia haina chochote katika hivyo hata Injili ya Yesu hakuna. isipokuwa...

Qur'an haina tofauti na ujumbe waliopewa mitume wa kabla ya Muhammad, yaani hivyo vyote ulivyotaja havipingani kabisa na Qur'an. ndiyo tunasema vitabu vya mitume wote utavipata kwenye Qur'an, kwa ujumbe wake kijana. Qur'an ni kitabu cha kipekee ulimwenguni. Kumbuka hilo.

Au ulifikiri Allah atawapa kila mtume ujumbe unaokinzana na wa mwenzake kama ilivyo ndani ya biblia?
 
Kupitia uzi huu nimegundua mambo kadhaa
1. Asilimia kubwa ya waumini wa Kiislam wanaamini katika stori za kufikirika na ni wepesi sana kushikwa kiakili hasa mtu anapotunga hadithi na kuihusianisha na dini yao.
2. Watu wengi wana matatizo na wanaamini yanaweza kutatuliwa kiroho na si kwa juhudi binafsi na akili! Kupitia uzi huu wa kufikirika nimeshangaa kuona watu wanaandika maombi yao kwa mtunzi eti awafikishie kwa huyo jini! Huu ni zaidi ya wendawazimu.
3. Uislam na shirki ni ndugu wa damu.
Mengine ntaendelea kuandika...
 
Wacha kuruka ruka.
Kama ujumbe wa watu wote Allah huwa anasema kama hapa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
(AL - BAQARA - 172)
Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.
...
Hiyo 47:17 ana amrishwa mtu mmoja ambaye ni Muhammadi.
Kama hutaki kuielewa hebu tuambie hii Aya anaambiwa Nabii gani maana hakuna jina
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
[ AL - AH'QAAF - 9 ]
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.

Leo hadi utaje dhambi za Muhammadi.
 
mheshimiwa stori siioni msukule part 3.. naona watu wana debate tu.
anyways umesema ukifunguq jicho la tatu unaweza kuwa ndan ya nyumba na ukawa unaona nje. sijui ila
wakat wa zama za khalifa umar aliwahi kuwa yupo kwenye mimbar madina akawa anatoa maelekezo ya jeshi lipo mbali sana kitu kama nchi nyingine wakamulliza akasema alikua anaona kinachoendelea hivi Umar alikua ana matukio yake i think ni level za uchamungu tu.
 
Kweli tupo tunafuatilia kwa makini lakini kwa tahadhari pia tunashangazwa na usahihi katika mambo ambayo tunajua wanadamu wengi hawajui yanasemwa hapa.
 
Sahihi sana ila kuna maarifa ya ki Mungu ukikosa waweza kusumbuliwa sana na wachawi licha ya uchamungu wako. Hasa mambo yako yaweza kusakamwa kama hawawezi moja kwa moja kukugusa wewe watagusa vya kwako.
 
Kweli tupo tunafuatilia kwa makini lakini kwa tahadhari pia tunashangazwa na usahihi katika mambo ambayo tunajua wanadamu wengi hawajui yanasemwa hapa.
Mkuu unavyosema kwa tahadhari unamaanisha nini?
 
Mkuu unavyosema kwa tahadhari unamaanisha nini?
Viumbe hawa katika ulimwengu wa roho ni werevu sana na wanatafuta namna ya kukubalika na wanadamu. Wanaujua uwezo wa ajabu wa mwanadamu lakini pia wanajua mapungufu yake. Tupo kwenye ushindani wa falme na mamlaka, vita hii ni kubwa sana na inapiganwa kati ya wanadamu. Na kati ya silaha kubwa sana anazotumia adui wa wanadamu ni UWONGO. Ndio maana nasema tuwe na tahadhari kubwa.
 
Asante mkuu, Kuna comment ulisema kama kuna mambo ya kiroho huyajui wachawi watakusumbua unaweza kutoa mfano wa mambo ambayo tunatakiwa kuyajua na kuyafanya ili kuishinda hii falme ya giza?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…