Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hilo ndilo la kwanza, unaweza kutafuta mchawi kumbe mchawi ni wewe mwenyewe. Husali una mlolongo wa maasi, utakosa wapi kua na matizo ya kiroho?

Kuna Hasad, ni tatizo kubwa kuliko uchawi, lakini mara nyingi hasad tunaikaribisha wenyewe bila kujijua. Hasad ni husuda.

Tiba za kiroho ni tofauti na tiba za kiganga na kitabibu.
Simba.
 
Kuna mtu aliuliza juu ya maana ya haya maneno ninayoelezea kwa mujibu wa quran nadhani ni FaizaFoxy naendelea nilipo ishia.

AFRIT au IFRIT - ni aina ya majini.
Katika maelezo ya Qur'ani na Hadithi, 'Ifrit ni majini wenye nguvu Wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa na mara nyingi wanahusishwa na uovu na uasi. wametajwa katika quran surat Naml aya ya 39
قَالَ عِفْرِيتٌۭ مِّنَ ٱلْجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّى عَلَيْهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌۭ
Tafsir : Akasema Ifrit Mimi nitakuletea kiti chake kabla hujainuka kutoka mahali pako, na mimi nina nguvu juu yake na ni muaminifu.’"
Katika aya hii, Nabii suleyman (a.s) aliwauliza baraza lake na tunajua nabii sulyman alipewa utawala kwa wanadamu na majini na wanyama hivyo aliuliza nani anaweza kwenda kuniletea kiti cha malkia wa sheba aliyeitwa balqis ndiyo huyu ifrit akamjibu mimi naweza kuleta kabla hujanyuka kutoka kwenye kiti chako.

Pia katika kisa maarufu cha Isra na miraj Bwana mtume Muhammad (S.a.w) wakati wapo na jibril mtume aliona kiumbe kuna wafuata mtume akamuuliza jibril ni kiumbe gani hicho ndipo jibril akamwambie mtume huyo ni Ifrit minal jinn nikufundishe maneno ambayo ukiyasema ataacha kutufatilia, Jibril a.s akamwambia sema.
بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Bismillahi alladhi la yadurru ma'asmihi shay'un fil ardhi wa la fis-sama'i,Wahuwas-sami'ul-alim":
Tafsir:
Kwa jina la Allah, ambaye hakuna kinachodhuru, iwe kwenye ardhi au angani, naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua."
Baada ya mtume kusema maneno haya jinn huyu akaacha kuwafatilia hii ni dua ya muhimu na inasisitizwa waislamu kuisoma katika adhkari za asubuh na jioni.

Kwa ujumla, Ifrit ni Majini wenye nguvu na waovu, lakini siyo wote wanakuwa na tabia mbaya. Kama majini wengine, wanaweza kuwa na tabia mbalimbali na uwezo wa kuchagua matendo yao.

MALAIKA - Kwa mujibu wa Qur'ani, malaika ni viumbe wa kiroho walioumbwa na Allah kwa nuru kwa ajili ya kutekeleza amri zake na kusimamia masuala mbalimbali ya ulimwengu. Malaika wana sifa maalum ambazo zinawafanya kuwa viumbe wa kiroho tofauti na wanadamu na majini.

Sifa za malaika​

  1. Viumbe wa Kiroho : Malaika ni viumbe wa kiroho
  2. Wanawajibika kwa Amri za Allah : Malaika hutekeleza amri za Allah na wanapokea maagizo kutoka kwake. Hawana uhuru wa kuchagua kama wanadamu; wao huishi na kutekeleza amri ya Allah kwa utii kamili.Sura ya 16 aya 49-50.
  3. Wanaweza Kujidhihirisha : Malaika wanaweza kujidhihirisha kwa watu kwa umbo maalum au kwa njia ya kiroho.
Wapo wengi sana ila kubwa zaidi kwao hawamuasi Allah wanatekeleza wanaloamrishwa tu wametajwa sana katika quran na hadithi kuna Jibril, Mikael, Israfil, Munkar, Nakir n.k na wanamajukumu tofauti tofauti na wapo wengine wao wanafanya ibada tu na kumtukuza Allah.
 
Swali lako zuri sana tena sana.

Alieandika Qur'an aliukuta moto upo tayari.

Alitia kidole ukamuunguza. Wewe kwani ulijuaje kama moto unaunguza?
Simba?
Mwenzio kaandika ulikuwa Moto wa tofauti ina maana sio huu unao uongelea hapa.
Sasa nataka kujua huo Moto wa tofauti ukoje ?
Aweke sifa zake hapa Kama unachoma ukitoa chumvi au lah.
 
Somo la Adamu ungeendelea nalo inaonekana limebeba mambo mengi.
kuhusu hili la sasa la majini kuumbwa kwa moto umesema quran imetumia tashbiha katika hili tupe ufafanuzi, Inaposema majini wameumbwa kwa moto ina maana gani?
Mara nyingi kazi yao kuharibu.

Tutafafanua kwa kina siku za usoni, kupitia Qur'an.
Simba.
 
tusubiri jibu la Arsis maana shida kama hizi hatoagi majibu ya maana yeye amekariri jibu lake la "fanya ibada,sali sana acha maasi" ndo kamaliza hivo hakupi suluhisho ya kipi ufanye ujitibu shida yako..ngoja aje
Unajua, cha kwanza kabisa kabla hujamtibu mtu mambo ya uzazi unatakiwa uelewe, ameolewa au anataka kuzaa kwa uzinzi tu?

Ukijua ni uzinzi kwanza umpe ushauri mpaka aolewe na huyo anaetaka kumpa ujauzito ndio umtibu.
Simba.
 
Isome mada utapima wewe nini ninachokijua na nini nisichokijua. Ndio kwanza tupo chapter 1.

Wanasema. kisichopimika hakipo.
Simba.
 
Usipunguze, acha kabisa.
Simba.
 
Usipunguze, acha kabisa.
Simba.
Ni suala la mchakato, kuacha pigo za “cold turkey” ni mwanzo wa kufeli. Kwahiyo una taper down mdogo mdogo mpaka unaacha kabisa.
 
isome mada utajua nini ninachokijua na nini nichokijua. Ndio kwanza tupo chapter 1.
Simba.
Simba, ninakusoma na ninakusoma tena...

Mambo ya 'Chapter/Chapters'....

Huu ukumbi ni wako; sema kila unachoandika 'kinapimika' ama/na 'kutathminika'--kwa kheri lakini.

Siyo kwamba hauna unayoyakosea ama vipi--ila unayo liberti ya kushiriki kusudi lako; ni vema hili kusudi lifanywe safi, safi tena safi iwezekanavyo...

Wakati mmoja, yote ambayo umewasilisha humu lakini 'hayajafanyika bora' yanaweza kuja kuboreshwa na wewe mwenyewe kwa 'msaada utakaopata isivyo moja kwa moja'...

'Moyo Mkunjufu' ni silaha ya ulinzi katika 'Rehema na Fadhili'...

Hmmm
 
Mwenzio kaandika ulikuwa Moto wa tofauti ina maana sio huu unao uongelea hapa.
Sasa nataka kujua huo Moto wa tofauti ukoje ?
Aweke sifa zake hapa Kama unachoma ukitoa chumvi au lah.
Nimekujibu wewe ulichouliza.
Simba.
 
I bet huyo Biti Mkunguni ni Muislam na hata hao uliowataja hapo juu usikute ni Waislam pia. Nakumbuka mwaka jana niliwahi kukutana na jini FaizaFixy pale Mtaa wa Tandamti, Kariakoo, alikuja kwangu kwa tabasamu na kunipa halwa akaniambia katumwa kwangu eti nijiue kwa kuvaa mabomu mwilini kisha nijilipue ili nikifa nikapewe mabikra 72 kule motoni. Nikakataa, kugeuka nyuma sikumuona tena ila nashangaa eti yupo hapa Jamii Forum.
 
Bro maandish yako mtu akisoma kidogo inabidi aende Instagram kwanza akapumzishe macho ndo arudi .. au we ndio robot wa CCM nini
 

Attachments

  • Screenshot_20240910_191839_Chrome.jpg
    108.4 KB · Views: 34
FaizaFoxy ni jini...?!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…