Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hilo nimemueleza. Ana majibu mepesi kweli
 
Mimi interest yangu zaidi ni kuhusu majini tu na si kingine kama hao washenzi wachawi.Huwa napenda kupata ilm ya hawa viumbe direct kutoka kwa mtu mwenye experience nao hususani kufanya nayo kazi,story za kwenye Qur'an zinazosemaga sijui majini waliumbwa kwa moto,sijui wanakaa sijui kwenye magofu na sehemu chafu naonaga tu kama ni hadithi tu za kutungwa.Sasa nikirudi kwenye swali langu la msingi, iwapo majini ni viumbe wa asili,je inawezekanaje mtu anamtengeneza jini,maana kuna mabwana kama wawili niliwasikia wakilizungumzia hili linalohusiana na majini ya kuyatengeneza na kuyatega sehemu.Na je majini yote yanayotegwa ni ya kutengenezwa au hata majini ya asili yanaweza kutegwa kwa ajili ya kuleta maangamizi
 
Bwana simba nna swali hivi Arsis anasemaje Au ana maaarifa Gani juu ya binadamu Watu Wenye Viganja Vyenye Herufi M.
 
Mbona hii anayotoa ndio solution ya kila kitu ndugu....🤔
Narudia tena hii ndio solution ya kila kitu🤝🤝
Naweza nikakuthibitishia hilo kwa vitendo!!!
Sema sijui namna ya kuweka sawa hii kitu, ila ningetoa somo lisilo rasmi kuhusu namna ya kuwa connected na Mungu direct!!!
Ila naogopa sabb elim yangu ndogo sana (maana mm ntaongea kutokana na experience wala sitotumia vitabu na uthibitisho wa hadithi sana.... Mm ntaongea kinachonitokea, Sasa mwisho ntajitukanisha hapa maana ntashindwa kutoa ushahidi🤝🤝

Na Kama ujuavyo humu wenye elim ni wengi 🚶🚶

(Ila ukiishi kama watu wa zamani ni rahisi Sana kumpata Mungu na kuuona ukubwa wake, hii nimeijaribu kwa baadh ya vitu ni really kabisaaaa
 
kaingia kwenye ukumbi mose ana mada nzito na uhakika atakua na majibu mazito.

Tustahamiliane tu.
Simba
Ndiyo kuna mambo 'yanasubiri'...

Hakuna namna,

Wanajamii inabidi wafanye bidii kutafuta kujua ilivyobora--hakuna 'njia ya mkato' kwa 'maarifa'.

Maarifa yana 'Mbegu ya U-JUA-JI' -- hili linataka nidhamu ya aina yake na siyo mambo ya 'Tumbuizo Asilia' kwa stori stori za maisha...

Na ndiyo, In Shaa Allah, uwezekano wa kufika kwenye 'Shams al Maarif' kwenye huu uzi upo...

Ngoja wadau wakidhi uwezo wa kukomaa na mambo ya kiufundi wa kawaida kwanza...

Hmmm
 
Bwana simba nna swali hivi Arsis anasemaje Au ana maaarifa Gani juu ya binadamu Watu Wenye Viganja Vyenye Herufi M.
Kwa ufupi hatufahamu.

Kama umekiona kitu katika huu uzi, hatuna utabiri wa aina yoyote, isipokua kuna kisa siku za usoni huko cha time travel na kwa kiwango kikubwa kitakua kwa siku za nyuma. Tunaweza kuelezea vilivotokea tu isipokua vichache sana ambavyo havijatokea., tunavisoma kwenye vitabu, si vyetu.
Simba.
 
Mwaga elimu.
Simba.
 
Muelekeo:
 
Kama unadhan unakijua kiswahili basi soma hizi post za huyu mwamba,dah hatar sana
 
Ungeweka link tukufate jwenye uzi wako badala ya kuharibu uzi kwa copy and paste.
 
Usikubali kukaa katikati maana utakuwa mtumwa... Hakika mwanga na ukuongoze
 
Chief hakika andiko lako au maandiko yana maarifa mengi tatizo lugha kiswahili unayotumia ndio shida,yaan ni kiswahili lkn kigumu sana

Mimi huwa ni mbishi wa kutaka kuelewa lkn huwa inaniwia ugumu kuelewa ujumbe wako

Ebu naomba uandike kwa lugha nyepesi,kwasababu inafika kipindi mtu unapoteza hamu ya kusoma kwa lugha iliyotumika
 
Kama ushasema "sijui" si uulize uelimishwe?

UnKataa wachawi wakati mwenyewe unajiita roho ya kishetani?
 
Nadhan tuko kujifunza elimu kwa mapana yake,wewe eleza uzoefu wako kuna kitu tutajifunza

Mwenye uzi mwenyewe kuna mambo huwa anaandika lkn tunasoma tu ingawa hayaafikiani na uelewa au kwa jinsi tunavyofahamu,kwahiyo mwaga elimu
 
Nadhan tuko kujifunza elimu kwa mapana yake,wewe eleza uzoefu wako kuna kitu tutajifunza

Mwenye uzi mwenyewe kuna mambo huwa anaandika lkn tunasoma tu ingawa hayaafikiani na uelewa au kwa jinsi tunavyofahamu,kwahiyo mwaga elimu
Kama lipi hilo?

Usifikiri unachoelewa wewe ndio kila kitu. Mimi kuna vingi wewe unavyo sivielewi na kama ninavielewa umevikosea nitakueleza wazi hivo sivo, ni hivi...

Binadam tuna kasoro ya kudhani tunachofahamu sisi na mwenzetu anakifahamu au fikra zatu sawa na za mwengine.

Uelewa na ufahamu wako ni tofauti na wangu na mimi halikadhalika, kama utafanana ni kwa uchache wake tu, sio kwa wingi wake.

Ndio maana Mwenyezi Mungu katupa mwongozo, ili hata tutapohitilafiana tusipotee njia. Turudi kwenye njia iliyonyooka kwa kujikumbusha kutwa mara tano kwa uchache.
Simba.
 
Arsis nimeguswa na swala au changamoto ya madam Farijala wa Farijala kuhusu mumewe,hakika huyo mwanaume mwenzetu anaumia sana lkn na dada yetu anaumia pia,kwasababu si nature ya mwanamke kulea familia,yaan analea lkn ni mzigo mzito kwake sana
Sasa kuna ushauri ulimpa wa ibada na kuacha maasi kitu ambacho ni sahihi kabisa,lkn inajulikana Mwenyezi Mungu ndio suluhisho la kila kitu sisi wengine ni sababu tu,kwahiyo kama kuna sababu ya kumpa kama ni dawa au namna nyingine yoyote basi msaidie ila mponyaji ni Allah

Kwangu mimi nashauri huyo mumeo wakati wa kuoga aweke chumvi ya mawe katika maji yake na iwe sehemu ya zoezi lake la kila siku,hiyo ni dawa ya asili ya kuondoa uchafu mwilini ya kichawi na kishirikina

Ila asiweke imani juu ya hiyo chumvi kwamba itamsaidia ila anapoweka chumvi katika maji anuie mfano wa hivi EWE MWENYEZI MUNGU HAKIKA WEWE NDIO ULIYO UMBA HII CHUMVI NA KUIPA NGUVU YA KUONDOA UCHAFU NA.MIKOSI NA MABALAA,NAOMBA KUPITIA HII CHUMVI IWE NI SABABU KUNITAKASA NA MABALAA YOTE YA KICHAWI,NUKSI NA UBAYA WOWOTE ULIO KATIKA MWILI WANGU

Kwa nia hii utakuwa umemtegemea Mwenyezi Mungu na si chumvi kama chumvi

Nakumbuka kipindi fulani pamoja na kufanya ibada nilitumia chumvi kuogea mara kadhaa,kuna matokeo yalionekana ikiwemo kuota usiku kitu kama majini yametoka nyuma ya mgongo wangu na.kusema huku yanapaa kutoka ndani kwenda nje ya nyumba "wewe si unajifanya mjanja sawa " baada ya kuamka niliwaza sana juu ya ile ndoto

Kwa kifupi habar za chumvi kuwa sehemu moja wapo ya tiba ya asili inakubalika sana na si uchawi,ila nasisitiza usiegemeze kuwa chumvi ndio suluhisho la shida zako ila Mungu kwanza na chumvi ni kama sababu tu

Kama vile tunavyokunywa dawa za hospitalini,anayetuponya ni Allah na dawa ni sababu tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…