Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hata swala Adam kuwa binadamu wa kwanza lipo kwenye Biblia, waandishi wa Quran walisahau kucopy.
hapana. watafsiri ndio walikolitoa huko. Adam wa kwenye Qur'an na kisa cha Adam wa Qur'an ni tofauti kabisa na Afdam wa biblia. Kwenye Qur'am mimi na wewe na wengine wengi ni Adam pia.

Msome Arsis kaanza kuchambua ni nini Adam kwenye Qur'an, ndio, ni nini, sio ni nani.
Simba.
 
alafu huyu Arsis huko post za nyuma alisema biblia ni kitabu cha wagiriki..nyie kama wakristo mnasemaje kuhusu hilo embu mbane Arsis atupe majibu kuhusu biblia ni kitabu cha wagiriki kivp yaan?
Swali zuri sana, ukweli ni...
Kwa sababu hakuna mtume yeyote aliekuja na Biblia. Hata neno Biblia ni la Kigiriki. Hata ndani ya bilia hakuna neno biblia kwenye aya hata moja ya biblia.
Simba.
 
Arsis anasema anangoja umalize atarudi kuja kuchambua, kwani kisa cha adama kinaendana sambamba na majini, mtakiona anavyoendelea na kisa cha adam, na atakuja kujibu hizi post zako.

Mwaga elimu.
Simba.
 
Naam, Nitajaribu kuweka katika mpangilio ambao unaweza lete mtiririko mzuri nitaanza na Jinni

JINNI - Ni kiumbe wa Allah aliyeumbwa kwa lengo la kumuabudu Allah, Wameumbwa kwa moto na wanauwezo wa kuchagua kufanya mema au maovu, sawa na wanadamu.
Wanaulimwengu wao ambao wanadamu hatuwezi kuwaona labda mpaka ufunguliwe macho kama bwana Simba. Wapo wema na wabaya lakini wana maisha simple compared na mwanadamu yaani wengi katika majini ni waasi wanafanya mabalaa sana habari zao kwa undani zipo katika Quran Surat jinn lakini pia Quran 51:56, 6:128.

INSAN - Huyu ni mwadamu ameumbwa kwa madhumuni maalum ya kumuabudu Allah na kuwa khalifa duniani, Kama walivyo majini basi na wadamu wana uhiari wa kufanya mema au maovu. Habari za mwanadamu zimejaa katika quran.
Kuhusu uumbwaji wake 23:12 -14 Inaeleza malengo ya kuumbwa kwake 51:56 Inaeleza.
Mpaka hapa utaona viumbe ambavyo vimeumbwa kwa lengo la kumuabudu Allah na wana uhiari ni majini na wanadamu ndio maana hukmu siku ya malipo ni kwa ajili ya majini na wanadamu tu.

IBLIS - Huyu ni katika majini, Ndiye aliyekataa kumsujudia Adam, na akafukuzwa katika rehma za Allah, Jambo ambalo watu wengi hawajui ni kuwa Iblis anawadanganya sio wanadamu tu bali hata majini wenzake.
Majini kwakuwa wanaweza kuwa wema au wabaya basi iblis huwa anawadanganya majini wenzake wamuasi Allah kisha anawatuma waje kuwadangaja wanadamu pia, Hivyo kuna majini wengi tu hawaijui haki kwasababu Iblis anawachezea kwa kuwalaghai.
Imeelezwa katika hadithi kuwa iblis ana kundi kubwa la wafuasi na anawatuma kila siku kuwafarakanisha wanadamu

عَنْ جَابِرٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «إِنَّ إِبْلِيسَ يَضَعُ عَرْشَهُ عَلَى الْمَاءِ ثُمَّ يَبْعَثُ سَرَايَاهُ فَأَدْنَاهُمْ مِنْهُ مَنْزِلَةً أَعْظَمُهُمْ فِتْنَةً. يَجِيءُ أَحَدُهُمْ فَيَقُولُ فَعَلْتُ كَذَا وَكَذَا فَيَقُولُ: مَا صَنَعْتَ شَيْئًا. ثُمَّ يَجِيءُ أَحَدُهُمْ فَيَقُولُ: مَا تَرَكْتُهُ حَتَّى فَرَّقْتُ بَيْنَهُ وَبَيْنَ امْرَأَتِهِ، فَيُدْنِيهِ مِنْهُ وَيَقُولُ: نِعْمَ أَنتَ»

Tafsir : Kutoka kwa Jabir, alisema: Mtume Muhammad ﷺ alisema: "Hakika Iblisi huweka kiti chake juu ya maji kisha anatuma vibaraka wake. Yule ambaye anaonekana kuwa karibu naye zaidi ni yule ambaye anafanya maasi zaidi. Mmoja wao huja na kusema: ‘Nimefanya hivi na hivi,’ naye (Iblisi) husema: ‘Hujafanya chochote.’ Kisha mwingine huja na kusema: ‘Sikumuacha mpaka nilipomtenganisha yeye na mkewe,’ naye (Iblisi) humkaribisha karibu naye na kusema: ‘Wewe ni mbora''
Hapo utaona jinsi Iblis anavyowatuma majini kufanya mabaya lakini pia Wanadamu wapo wanaomuabudu huyu Iblis.

SHETANI - Hii ni sifa ya kiumbe muovu katika majini na wanadamu hivyo jinni au mwanadamu akiwa muovu anakuwa shetani ingawaje katika quran kuna aya nyingi zinataja shetani zikimaanisha Iblis hii ni kwa sababu Iblis aliaswi na akahukumiwa moto na lengo lake nikutafuta kundi kubwa katika majini na watu wa kwenda nae motoni hivyo Iblis ni shetani moja kwa moja, Jinni na mwanadamu wanaweza kuwa mashetani kwa vitendo vyao vya kufru. Nawaweza wasiwe mashetani kwa wema wao na uchamungu.
Ndio maana kabla ya kuanza kuosoma Quran tunataka hifadhi kwa Allah kutokana na shatani kwa maana wabaya wote katika watu na majini na Iblis mwenyewe Allah atukinge kwao.

Nitaendelea Inshaalah.
 
Hapana msimamo wangu mpaka sasa Adamu ni binadamu wa kwanza kulingana na nilivyosoma mimi na uelewa wangu wa quran na wanzuoni wanavyosema.
Suala la wanazuoni wanaosema Adamu sio binadamu wa kwanza nilikubali lipo ila mpaka sasa hoja za wamaosema Adamu ndio wa kwanza nazielewa zaidi, Ndio maana nasisitiza Arsis aendelee na Mada ya Adamu huenda nikaona kitu kipya au akatoa hoja zenye nguvu, Ila msimamo wangu ni kuwa Adamu ni binadamu wa kwanza kuumbwa kulingaana na hoja nilizozitoa na wachangiajiwengine walivyotoa. Kuna sehemu nasubiri Arsis afike hapo tutakuwa tunatafuna Muwa kwenye fundo.
 
Unaweza kutupa ushahidi wako wa kwenye Qur'an?

Au wewe unafata hoja za watu badala ya Qur'an?
Simba.
 
Hapa mimi nina swali kwenye hoja ya kwanza ya Jini.

Kama jini ni kiumbe cha Allah wameumbwa ili wamuabudu Allah, je majini wanatumia kitabu gani?

Je majini ni dini gani?

Je majini wanaswali wapi?

Je kuna ukweli wowote kwamba kuna binadamu wanatengeneza majini na kuyafuga na kuyatuma?

Naomba na Arsis atie neno kwenye haya maswali yangu yanayonitatiza.

Asante.
 
Simba nauliza kwanini bank haziibiwi kishirikina/Chuma ulete wanasema kwamba Bank zinalindwa na majini. Kuibia lazima utumie silaha au kuvunja

Hayo majini yanayolinda bank isiibiwe kishirikina yanamilikiwa na nani? Bank au serikali au bank ya dunia?
Wanaiba sana tu lakini kuna ulinzi wa kwenye bank ambao ni siri kubwa sana, unalinda kuibiwa na watu na majini, lakini watu wana akili sana wanaiba na huo ulinzi upo, wakipata upenyo tu.
Simba.
 
Swali zuri sana, ukweli ni...
Kwa sababu hakuna mtume yeyote aliekuja na Biblia. Hata neno Biblia ni la Kigiriki. Hata ndani ya bilia hakuna neno biblia kwenye aya hata moja ya biblia.
Simba.
Swali: Kitabu Kitukufu cha Imani ya Uislam kilikuja na Mtume gani?
 
alafu huyu Arsis huko post za nyuma alisema biblia ni kitabu cha wagiriki..nyie kama wakristo mnasemaje kuhusu hilo embu mbane Arsis atupe majibu kuhusu biblia ni kitabu cha wagiriki kivp yaan?
Quran ni kitabu kimoja, lakini Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 ndio unapata jina Biblia.

Mtume Muhamad hakuacha vitabu vya sunna hadithi na sila.

Jews kitabu chao kinaitwa Tanakh ni mkusanyiko wa vitabu pia ikiwemo Torati.

Ni simple logic tu.
 
Ma shaa Allah ilm za kila aina zimepamba moto huku.

Ingawa tunachota lakini Simba usichelewe kukimalizia kisa cha Kojani na Comoros.

Unakuwa kama tamthilia za kituruki?
Umenitelekeza kinamna flan hiv, wakat nataka unimwagie elimu yakujitoa Jini likikukumba.
 
Maswali mazuri sana
Nitakujibu inshaallah
Arsis kuna ombi hapa Arsis atiye neno kwenye maswali ya Dr Matola PhD
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…