Mkuu hakuna mji ambao una watu wabaya tu, wapo ambao ni wazuri. Hata Gamboshi kunakosifika kwa uchawi wapo ambao hawapractice huo uchawi, lakini hii haiondoi kwamba Gamboshi kuna tabia fulani ambazo zinafahamika.
Labda nikutolee mfano mwingine; mimi nimesoma hapo High School, na pale shule machalii wa chuga walikuwa wanamakundi yao na wanajiona wao ndo wao (again, sio wote) sijui walikuwa wanajiona wanajua kuvuta bange vizuri au vipi. Hawa jamaa walikuwa wanatuchukia sana tuliotoka mikoani tena hasa hasa Dar, yani mtu umevaa zako smart umepiga pasi basi utaitwa bishoo mara mtoto wa mama na majina mengine mengi sababu tu wao labda wapo rough na milegezo yao. Kuna scenario moja ilitokea nikashangaa sana, kuna mchizi wetu wa Dar alikuwa akinata na mtoto mmoja mkali wa chuga, na huyo demu kuna jamaa wa chuga alikuwa akimpenda sana lakini demu akawa hamuelewi. Siku moja tupo dinner tunashangaa mchizi kabananishwa na machizi kama watano wa Arusha wanataka kumfanyia fujo. Sababu tu eti anatembea na demu wa Arusha yeye mtoto wa mama wa Dar aachane nae. Kilichosaidia na sisi wa Dar tulikuwa na jamaa mmoja ulikuwa unamtoka mkono kinoma, yule ndio alikuja kuokoa lile jahazi. Bila hivyo lazima jamaa wangemzuru!!
Sasa hiyo ni scenario moja tu, lakini tabia kama hizi ni kawaida sana hapo Arusha, ndio maana hata mimi nilivyorushiwa mawe wala sikupanic nikajiona kama ni mkosefu. Nalikuwa nikifahamu hizi tabia zao!!
Sabaya na Gambo ni typical mfano wa vijana wa Arusha na tabia zao. Ukiacha hawa ambao wana tabia za ovyo ovyo wapo washkaji wa Arusha ni watu poa sana. I can’t forget some memories at Club AQ enzi hizo, Masai Club, La Fiesta na Pool table na washkaji pale Sun-dip, swimming Arusha Hotel!! I had a very good time there na siwezi regret