Niliyoyaona jana kwenye ATM ya NMB Gongolamboto yanatia aibu kwa watumishi

Walimu kwa mfano hua wanapenda sana kupanga foleni. Ni hobby yao hata ukiwawekea options 90 watakusanyana watiane ujinga weee wote watachagua option moja wakajazane ili wapange foleni.
 
Ahueni kwenye maelezo yako umetumia neno watumishi wa umma!

Angekuwa ni mpwayungu village, moja kwa moja angesema hao watu wote aliowakuta kwenye hiyo ATM mashine ya Gongolamboto; ni walimu!
 
Kutoa wa wakala
KIASI GHARAMA
100,000 4,800

Kutoa kwa ATM
100,000 1,200

Kupanga ni kuchagua.
Binafsi sioni mantiki ya hii tabia ya Watanzania walio wengi ya kupenda kufuatilia maisha ya watu, na pia kupenda kuwapangia watu cha kufanya!

Imagine mtu yuko zake barabarani! Lakini anaumizwa kichwa na watu waliopanga foleni, kwa ajili ya kuchukua hela zao kwenye ATM mashine!!
 
Sasa Hilo Jimbo lenu lots ATM zipo nne tu unategemea Nini?
 
Ahahahaha.
Kumbe ni walimu wale waliokuja na wadeni wao.
Hongera mwalimu
 
Mishahara yote kupitia NMB ni maamuzi ya ajabu
Hapana.
Mimi 2015 wakati naajiriwa niliambiwa nipeleke account ya NMB, NBC, penki ya posta au crdb.
Ila kipindi kile crdb walikuwa wakilipwa siku moja kabla ya NMB na siku 2 kabla ya NBC na posta. Hivyo hr akanishauri nitumie crdb .
Sema kuna taasisi hawawaambii watumishi wao kuwa wana uhuru wa kuchagua benki ya kupitishia mshahara wao.
Hata mifuko ya hifadhi ya jamii ma hr wengine walikula rushwa na kuwapangia watumishi mfuko mmoja jambo ambalo ni kinyume cha haki za mtumishi.
 
1. Hivi enzi hizi bado mtu na akili zake timamu anapoteza muda kwenye foleni huku makato ukitoa kupitia internet au sim banking yanalingana. Huu muda unaopotea kuokoa mia 4, buku au mia 5 mtu haoni ni hasara.
Kwani umeshaona mtu ana passbook miaka hii? Nadhani ungeanza kwa kuyashambulia mabank kwanini wanainstall ATM machine na kwanini wanatengeneza card, mabank yakiua hiyo teknolojia ya atm basi watu watatumia simu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…