Niliyoyaona jana kwenye ATM ya NMB Gongolamboto yanatia aibu kwa watumishi

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
8,429
21,834
Nilikuwa napita jioni kuelekea job. Si mnajua night shift zetu walinzi ndugu zangu. Nilikuwa nimempa lift mfanyakazi mwenzangu tukitokea Chanika.

Sasa nafika NMB Gongolamboto nikiwa barabarani jamaa akaniambia ona ile foleni, nikacheki kushoto nakuta foleni ya haja. Nikakumbuka kuwa ni tarehe ya mshahara. Mimi tayari nishatoa kwa simu, nina karibu mwaka siijui ATM machine.

Kwanini niseme niliyoyaona ni aibu kwa watumishi wa umma?
1. Hivi enzi hizi bado mtu na akili zake timamu anapoteza muda kwenye foleni huku makato ukitoa kupitia internet au sim banking yanalingana. Huu muda unaopotea kuokoa mia 4, buku au mia 5 mtu haoni ni hasara.

2. La pili linalotia aibu ni kwamba watumishi wengi wameambatana na wadeni wao ambao ndio walimiliki ATM card zao mpaka siku ya mshahara.

Jamaa yangu aliniambia wale waliokaa kwenye mawe ni wadau wanaowakopesha watumishi na kumiliki kadi zao na kuwapa siku ya mshahara wanapokutana kwenye ATM.

Nikafanya utafiti kuhusu hilo na kujihakikishia kuwa ni kweli. Aibu hii itaisha lini?

Serikali ipeleke wataalamu wa fedha na uchumi kwenye taasisi zake ili kuwafunda watumishi. Pamoja na maslahi ndogo ila mambo mengine yanatokana na ujinga (kukosa elimu ya kiuchumi na fedha) kwa watumishi.

Mtu anashindwa hata kui sacrifice laki 3 kujitosa kwenye ufugaji wa kuku. Aibu.
 
QUIGLEY

JF-Expert Member
May 23, 2015
28,484
81,032
Hapo chini umemalizia kirahisi sana.
Wote wakifuga kuku wanunuzi watatoka wapi?.

Hali ngumu za Watanzania huanzia mbali mkuu.
Mnyororo wa matatizo huanza day one ya kuajiriwa.
Mfano baadhi ya waalimu huanza kazi bila pesa ya kujikimu na baadhi hulalamika kuwa mishahara ya awali huchelewa sijui hadi waingizwe kwenye system ya malipo.

Kwa hali hiyo mikopo huanza day one ya ajira:
1. Nauli mkopo
2. Chumba cha kupanga mkopo
3. Mahitaji ya kila siku mkopo
4. Mshahara wa kwanza unaanza kulipa madeni, sijui kugawana wazazi na ndg...aaah

Nchi ngumu sana hii
 
Trinity

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
1,234
1,958
Hivi najiuliza kitu, ni kweli wengi huwa wanakopa na kuwekeza kadi za benki, sasa ikatokea nineunganisha simbanking na nikakopa nikaweka kadi mwisho wa siku mkopeshaji anabaki na kadi isiyo na msaada.

Wanafanyaje kuepuka kupigwa hawa wakopeshaji?
 
QUIGLEY

JF-Expert Member
May 23, 2015
28,484
81,032
Hivi najiuliza kitu, ni kweli wengi huwa wanakopa na kuwekeza kadi za benki, sasa ikatokea nineunganisha simbanking na nikakopa nikaweka kadi mwisho wa siku mkopeshaji anabaki na kadi isiyo na msaada.

Wanafanyaje kuepuka kupigwa hawa wakopeshaji?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Pili mtu anaweza kuripoti kuwa kapoteza kadi then akapewa nyingine
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
8,878
9,331
Kundi dogo la watumishi lina beba kundi kubwa la wategemezi,jambo linalopelekea kuwepo na mahitaji mengi kwa mwajiriwa,pia maslahi duni na fursa nadra za posho na marupurupu huchangia maisha magumu na madeni kwa watumishi walio wengi
 
Rashidi Jololo

Senior Member
Sep 21, 2022
132
136
Nilikuwa napita jioni kuelekea job. Si mnajua night shift zetu walinzi ndugu zangu. Nilikuwa nimempa lift mdanyakazi mwenzangu tukitokea Chanika.

Sasa nafika NMB Gongolamboto nikiwa barabarani jamaa akaniambia ona ile foleni, nikacheki kushoto nakuta foleni ya haja. Nikakumbuka kuwa ni tarehe ya mshahara. Mimi tayari nishatoa kwa simu, nina karibu mwaka siijui ATM machine.

Kwanini niseme niliyoyaona ni aibu kwa watumishi wa umma?
1. Hivi enzi hizi bado mtu na akili zake timamu anapoteza muda kwenye foleni huku makato ukitoa kupitia internet au sim banking yanalingana. Huu muda unaopotea kuokoa mia 4, buku au mia 5 mtu haoni ni hasara.

2. La pili linalotia aibu ni kwamba watumishi wengi wameambatana na wadeni wao ambao ndio walimiliki ATM card zao mpaka siku ya mshahara.

Jamaa yangu aliniambia wale waliokaa kwenye mawe ni wadau wanaowakopesha watumishi na kumiliki kadi zao na kuwapa siku ya mshahara wanapokutana kwenye ATM.

Nikafanya utafiti kuhusu hilo na kujihakikishia kuwa ni kweli. Aibu hii itaisha lini?

Serikali ipeleke wataalamu wa fedha na uchumi kwenye taasisi zake ili kuwafunda watumishi. Pamoja na maslahi ndogo ila mambo mengine yanatokana na ujinga (kukosa elimu ya kiuchumi na fedha) kwa watumishi.

Mtu anashindwa hata kui sacrifice laki 3 kujitosa kwenye ufugaji wa kuku. Aibu.
Mshahara tayari Mwalimu?
 
Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
2,785
3,068
Waache tu, bila masikini hakuna tajiri..

Movie ya six flying dragons.. Gil tami.. anausema ukweli kabla ya kufa na ndiyo msemo wangu...

"Kuanzia dunia imeumbwa hadi itakapoisha masikini ata endelea kutawaliwa na tajiri na hakuna usawa kati ya tajiri na masikini"

Hivyo pambana kutafuta chako hao wapo na wataendelea kuwepo hadi kufa kwako
 
Mr Gadaffi

JF-Expert Member
Nov 14, 2022
401
559
Mtu anaelipwa mshahara, anategemea mshahara.
kusubiri siku 30 ndipo upate pesa yataka moyo sana.
Siku 30 zinatosha kuufyekelea mbali mshahara wote wa mwez uliopita.
Kuhusu kufuga kuku kama ulivyosema, wanaona ni kazi ya kipumbavu na kujidhalilisha.
Wao wana malengo ya kufanya biashara baada ya kustaafu, akishapata kiinua mgongo.
Kama utamuona mfanyakazi ana vimiradi vyake pembeni huyo ni mjanja sana anaetumia common s.
Mafanyakazi anaona ajira aliyonayo serikalini ndicho chanzo tosha cha mapato, mshahara ukichelewa siku 2 tu anakunja ndita na kutamani kumtumbua rais samia.
Mfanyakazi kuanzisha kabiashara kwa mtaji wa milioni 1, 2 anaona ni upotezaji muda, wengi wana malengo ya muda mrefu (miaka 10+)

Fanya kazi muda mfupi kajiajiri, au hakikisha jiwe moja linaua ndege wawili. Ova
 
dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
246
302
Kumbe na wee unawaonea wivu walimu kwani kupiga foleni Ni aibu gani wakati naenda kuchukuwa mpunga wangu alfu siyo kila kitu nikimbilie internet au sim banking sometime hyo simu bank sinasumbua na kupeleka kusubiri sna pesa iingiee

Tuache bhna tukachukue hell zetu na zako za ulizni subiria upewe dirishani kwa muhindi
 
19 Reactions
Reply
Top Bottom