Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Aug 8, 2020
92
400
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.

Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.

1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.

2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.

3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.

4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.

  • Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
  • TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
  • Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
  • Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
  • Daraja la baharini Selandar
  • Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
  • Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
  • Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
  • Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.
Mwisho - siyo kwamba napachukia nyumbani lengo la uzi huu ni kutaka tubadilike na ikiwa tunataka maendeleo ya kweli ya miji yetu ni lazima tukubali kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje. Ili dsm yetu iwe na hadhi ya kidunia ni lazima (ukweli mchungu) kubomolewa upya, labda kuacha maeneo machache sana, na kujengwa upya (ni hasara lakini baada ya kujengwa upya faida yake ni kubwa sana)

Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo
 

mweongo

Member
Aug 23, 2010
58
150
Umeongea vizuri sana. Ki ukweli utadhani viongozi wetu na wataalamu wetu hawajawahi kusafiri nje ya Tanzania. na hata kama hawajawahi sehemu zilizojengwa na kupangwa na wakoloni kwenye miji yetu ndio nzuri hadi leo hii.

Hakika miji ya tanania inasikitisha sana. Hata hizo highway tunazoambiwa kila siku ni shida tupu maana zimejaa matuta yanayoharibu magari. Watanzania hata wale waliosoma na kufuta ujinga, na hata wale waliotembea nje wabebaki kusifu na kuabudu. Sijui nani ameturoga.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,115
2,000
Wakati mwingine ujitahidi pia kutembelea stendi yetu mpya ya kimataifa ya Mbezi! Tumelazimishwa kuiita stendi ya magufuli! Utajionea mwenewe wanyonge wanavyo fanya biashara ndani ya hiyo stendi bila bughudha!

Hutokuja uuone huo utaratibu sehemu yoyote ile duniani zaidi ya huku kwenye nchi yetu ya wanyonge.
 

madindigwa

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,755
2,000
Aisee nimeishia tu kuguna Yani unavyo ponda Kama sio kwenu ndio Mana katika story zako zako hujazungumzia hata nyumbani kwenu inamana hujafikia kwenu umeishia hotel nilivyo kuelewa Mimi ni kwamba unatusimulia Kama umefika ulaya we tuache na Tanzania yetu kaishi Ulaya.
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
619
1,000
Limbukeni akioneshwa mwezi hujidai yeye ndiye mwanzilishi wa kuona mwanga; ulichokielezea kinasadifu na laiti kama mzazi wako anakaa kijijini akisoma hiki alichokiandika hawezi kukuruhusu kurudi hata kuona kaburi lake ABADI.

Ni bora upotelee huko huko ulikolowea kuliko kubagaza taifa lako. Usiache mbachao kwa msala upitao. Huna mfano boara wa kuigwa na yeyote anayetafuta kutoka katika maisha yaliyojaa changamoto.

Wanaokutumia kwa kukulipa pesa ambazo hujui zimetokana na nini ndio waliokujaza kiburi ambacho kabla hujarejea ukimbizini utarejea kwenye jukwaa hili kuomba msamaha.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,383
2,000
Tatizo tumepotoka, tunataka Tanzania iwe kama Ulaya / Hata viongozi wetu wanadhani hivyo na kwamba kuwa ulaya ni kuwa na maghorofa, nyumba za vigae na mabati sijui ya Mu-South. Huo mimi naita ulimbukeni.

Maendeleo ni mji uliopangika, msafi unafuata master plan na kila huduma muhimu zipo karibu na kila raia. Kwahio kabla hatujapotea zaidi katika kila plan zinazokuja wasisahau kwamba kila plan zinahitaji mambo matatu kuyakidhi Social, Economical Bila Kusahau Environmental. Kama Jamaa zetu Red Indians walivyotwambia.

"When the last tree has been cut, the last fish eaten, and the last stream poisoned, you will realize that you cannot eat money"
 

Trondheim

Member
Dec 16, 2020
73
150
Aisee nimeishia tu kuguna Yani unavyo ponda Kama sio kwenu ndio Mana katika story zako zako hujazungumzia hata nyumbani kwenu inamana hujafikia kwenu umeishia hotel nilivyo kuelewa Mimi ni kwamba unatusimulia Kama umefika ulaya we tuache na Tanzania yetu kaishi ulaya
Akuache wewe na nani, sisi pia umechoka na hizo kalele za viongozi kumbe hata Kenya hatuwafikii sasa kwetu mbona kelele hivi? Mbona Kenya hatuyasikii haya, Asante sana Baharia kwa kututowa tongotongo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom