CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Shalom,
Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.
Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.
Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.
1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.
2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.
3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.
4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.
Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo

- Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
- TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
- Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
- Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
- Daraja la baharini Selandar
- Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
- Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
- Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
- Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.