kevin strootman
JF-Expert Member
- Nov 26, 2017
- 1,077
- 1,728
Nimekaa sana Kigamboni na nimetembea sehem nyingi, sehemu kubwa ya Kigamboni ni mapori tuu, miundombinu mibovu sana, barabara za lami ni chache mno, hakujajengeka sijui kwanini watu hawajengi Kwa Kasi.
Ukitoka Mji Mwemba mpaka Pemba mnazi Kuna sehemu lami inaishia, Kimbiji ya miaka 10 iliopita na ya Leo hakuna tofauti, huko Buyuni Sasa kama mkoani, njoo Mwasonga hapo kati ni mapori tu na barabara mbovu, ukitokea kiwanda cha Nyati cement kupitia mwasonga-kibada barabara ni mbovu balaa, mvua zikinyesha hapapitiki, kuna sehemu kuna mashamba ya mpunga kunajaa maji balaa hakuna nyumba ni nyasi tuu na mapori unaweza ukasema sio Dar.
Nashangaa sana juzi nmetoka Chanika nikataka kupotea, kumbe Chanika kumekuwa mjini kabisa, nashangaa sana kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo hamna au kwakuwa wilaya mpya ndio maana inakua ya mwisho Kwa maendeleo Kwa hizi wilaya 5 za Dar??