Nilivyonusurika kutapeliwa milioni yangu ya kwanza kuishika hapa duniani

Nyamwage

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
634
1,535
Habari

Hii ni pesa yangu ya mara ya kwanza kuimiliki nikiwa under 18 sikuipata kwa mkupuo hapana nilidunduliza kidogo kidogo kutokana na kibarua nilicho tafutiwa na mzee wangu

Huyo tapeli tulikua tunawajibika wote katika kibarua hicho pia alikua na urafiki na mzee wangu wakikutana wanapiga story za hapa na pale mzee nae ananisifia kua nina akili sana maana kiasi cha pesa nilichokua nakisave nilikua namjulisha mzee ni kiasi fulani basi katika mazungumzo ya mzee na huyo rafiki yake anagusia na kiasi changu cha pesa sio kwa ubaya ila alikua anajisifia kuwa kapata kijana mtunzaji wa pesa mzuri kilicho sababisha pesa hiyo kuwa nyingi nilikua naishi home chakula cha usiku nilikua nakula home nilikua najilisha chai na mchana tu siku za kazi lakini siku za j1 na j2 nilikua nakula home

Basi hiyo pesa ikakua mpaka ikafika 700k ziko mfuko naogopa kuziacha home sababu madogo wanaweza nipiga na kitu kizito ilikua 2010 ndio mambo ya m-pesa yameanza kuamika hapo mkoani kwetu.

Nikaenda kusajiri laini ya voda na maswala yote ya m-pesa nikaweka pesa zangu zote humo kwenye simu nikawa sasa na amani takakimbiza hicho kibarua baada muda kile kibarua kikawa kimeisha tukawa hatuna kazi muda huo kwenye m-pesa nilikua nimefikisha milioni 1.1

Kuna siku sasa huyo rafiki yake na mzee akaja home tulikua temezoana maana alikuna ni kabila moja na sisi alikuja nimuazime kitambulisho changu cha mpiga kura akasajili laini mpya maana ya kwake kampa demu wake nikampa bwana kama dakika 40 hivi naona kwenye simu yangu kuna neno la kingereza nimelisahau na simu yangu haina huduma yoyote najiuliza kulikoni au ni mtandao wenyewe unazingua nikapotezea kuwa baadae huenda ukawa sawa

Kumbe mwamba bwana kaenda kusajiri namba yangu upya akawa na laini yangu mpya ikiwa na pesa zangu zimehamia kwenye hio laini mpya kipindi kile ukisajili m-pesa namba ya siri ilikua ni mwaka wako wa kuzaliwa na huyo boya mwaka wangu anaujua kang'ang'ana kutoa hio pesa kashindwa ikabidi afunge safari mpaka mjini vodashop ili kuongopa kua mwenye hii simu ni mdogo wake yuko hospital kazidiwa hawezi hata kuongea kwahio nisaidieni kutoa hizi pesa nikayaokoe naisha yake

Wale mabwana wa Vodacom wakamkataa huyo tapeli nawapa hongera sana akanirudia sana mimi kujaribu mbinu yake ya mwisho kafika tu mimi namuuliza vipi mbona simu yangu haifanyi kazi kimetokea nini huko akanza kujichekesha chekesha anasema eti wakala ailiemsajilia namba ndio kakosea katoa namba zimefanana na yangu sasa mimi nimepanic nikachukua simu yake ili niangalie inawezekana vipi hilo jambo ni geni kwangu nikaingia m-pesa kuangalia salio nakuta ni kiasi changu cha pesa kipo kwenye laini mpya hiyo aliyo sajili nikatukana sana huku nina jazba tumfute huyo alio kusajilia hiyo laini

Sasa wakati tupo njiani kuelekea akaitoa ile laini yangu akanipa akasema ngoja niingie chooni hapo bar mara moja mimi nikasema kwakua nimepata kaini yangu ngoja niitoe hii iliokufa niiweke hii mpya Mungu wangu kumbe kanipa laini nyingine tofauti sasa najaribu kuingia m-pesa kuangalia salio inaniletea ujumbe kuwa namba ya siri ulioingiza sio sahihi

Ikabidi nichukue gari mpaka vodashop nawaeleza nilichofanyiwa nao wakaniuliza huyo mtu yuko vipi nikawaambia wakasema alikuja hapa mimi nikamsukumia kwa mkuu wangu lakini mkuu nae alimkatalia basi nikamtajia namba huyo customer care aangalie salio anakuta 20k imetolewa kumbe pale kipindi nimepanic naangalia salio yule mpuuzi alikua makini kuona ni namba gani ya siri naiweka akaikalili basi yule muhudumu ikabidi aizuie huduma hiyo account yangu kilicho saidia asikombe kiasi chote ni utaratibu ulio kuepo kipindi hicho kuwa huwezi kutoa pesa nyingi kama hauna kitambulisho chenye majina yako kamili

Nilipotoka hapo nikaenda polisi kuelezea tatizo lililo nikuta polisi wakanipa askari mmoja amekaa kiraia ili nishirikiane nae nimpeleke mpaka jamaa anapokaa ili tuweze kumnasa kabla sasa hatujaenda huyo asikari ananiambia hajanywa chai hapo mimi nina moto tunaenda kumkamata mtu nikampa afande 5k takaenda nikamuonesha anapokaa huyo muhalifu akayacheki mazigira akasema sisi tuakuja wawili saa kumi asubuhi mapema ili tumkamate kabla hajaamka haya.

Mimi nikaondoka kesho naenda asikali anasema alitingwa sana hakuweza kwenda kwahio tuongozane mpaka anaposhindaga walikua wawili sasa wakati tunaenda wanataka ela ya mguu kama madalali vile nikatoa 10k nikawapa tumeenda tumezunguka hatujampata wakesema wewe nenda njoo jioni jioni nikaenda nimekaa pale nje ya kituo kidogo cha polisi kuna jamaa mmoja simjui nilimkuta pale tukawa tunapiga stori akaniuliza vipi mbona kila siku uko.

Hapa hujafanikisha unachokifatilia jamaa nikamwambia kwanini niko pale akanishauri kwakua jamaa kakuibia 20k achana nae hapa utatoa zaidi ya hiyo 20k na usifanikiwe akaniambia vuta pumzu alafu shusha pumzi achilia hayo yamepita utapoteza zaidi ukiendelea kuja hapa kakua umeshapata funzo utakua makini nikaondoka zangu mdogo mdogo.

Huyo tapeli alipopata taarifa kuwa anatafutwa na police akakimbia mkoa sijamuonaga tena mpaka leo.
 
Kuna siku sasa huyo rafiki yake na mzee akaja home tulikua temezoana maana alikuna ni kabila moja na sisi alikuja nimuazime kitambulisho changu cha mpiga kura akasajili laini
Umesema ulikuwa chini ya miaka 18 muda huo, ulimiliki vipi kitambulisho cha mpiga kura ?

screenshot ya kumbukumbu

1680900442566.png
 
Uzi wako una chai nyingi sana. Kwamba zamani ilikuwa namba ya siri lazima iwe mwaka wako wa kuzaliwa na huruhusiwi kutoa hela nyingi bila kitambulisho. Muwe mnaweka DISCLAIMER kwamba hizi ni stori za kutunga.
Afu hapo hapo anasema jamaa alikua makini kuangalia namba ya Siri wakati anasema namba ya Siri ilikua mwaka wa kuzaliwa na tayari kitambulisho alishampa jamaa mpaka akafanikiwa kusajiri laini yenye namba kama zake..
 
Uzi wako una chai nyingi sana. Kwamba zamani ilikuwa namba ya siri lazima iwe mwaka wako wa kuzaliwa na huruhusiwi kutoa hela nyingi bila kitambulisho. Muwe mnaweka DISCLAIMER kwamba hizi ni stori za kutunga.
Walikua wanapendelea kutumia mwaka wako wa kuzaliwa lakini ulikua unaweza kubadirisha mwenyewe namba mpya ya siri nadhani watu walioanza kusajili laini zamani wananielewa achana na nyinyi watoto wa juzi
 
Afu hapo hapo anasema jamaa alikua makini kuangalia namba ya Siri wakati anasema namba ya Siri ilikua mwaka wa kuzaliwa na tayari kitambulisho alishampa jamaa mpaka akafanikiwa kusajiri laini yenye namba kama zake..
Alifanya vile akitegemea kua namba yangu ya siri ni mwaka wa kuzaliwa kumbe mimi nilibadirishaga kitambo ndio maana alikua makini kuangalia naweka namba ipi tofauti na mwaka
 
Walikua wanapendelea kutumia mwaka wako wa kuzaliwa lakini ulikua unaweza kubadirisha mwenyewe namba mpya ya siri nadhani watu walioanza kusajili laini zamani wananielewa achana na nyinyi watoto wa juzi
Unajua maana ya neno DISCLAIMER?
 
Na hiyo laini aliyokubadilishia ukaangalia salio ukakuta sifuri, uliijuaje namba yake ya siri......dogo usitake kutuona sisi mapimbi wenzio
 
Na hiyo laini aliyokubadilishia ukaangalia salio ukakuta sifuri, uliijuaje namba yake ya siri......dogo usitake kutuona sisi mapimbi wenzio
Nimekosea uandishi namba ya siri nilio ingiza iligoma mkuu vingine nasahau maana imepita miaka 12
 
Na hiyo laini aliyokubadilishia ukaangalia salio ukakuta sifuri, uliijuaje namba yake ya siri......dogo usitake kutuona sisi mapimbi wenzio
...Baba Yako ana Urafiki na Matapeli ? Anaujua Msemo wa 'Nionyeshe Marafiki zako nitakuambia Wewe ni Nani'??...
 
Back
Top Bottom