ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Hakika hakuna ajuaye kesho yake, hata wewe kamwe usije kujikatia tamaa katika maisha kwahakika siri ipo kwa Muumba wetu.
Haimaanishi kwamba nawe utakuja kutamba na VAT laa,namaanisha kwa safari yoyote ya maisha uliyokuwa nayo basi haijaisha mpaka iishe, kwa hiyo endelea kupambana bila kuchoka na amini ipo siku moja nawe utashaini tu
Back in the days, nikiwa ndani ya ukumbi wa Bilcanass pale posta mpya,wakati huo Mwana FA alikuwa anazindua album yake akiwa pamoja na East Coast Team kama kumbu kumbu zangu zipo sawa
Alikuwa amevaa jezi ya team ya mpira wa kikapu Maana Enzi hizo Basketball kama ilikuwa ina mwamko sana, kichwani akiwa amesuka msuko wa twende kilioni, yaani ile kinyamwezi sana, dah ilikuwa way back
Guess what? Today ni Naibu Waziri kitu ambacho hata yeye wakati huo huenda hakuwahi kabisa kufikiria au kuota ndoto hiyo japo kiutani utani, hiyo ndio siri ya maisha ilivyo
Endelea kufunua page za maisha yako huwezi jua page ya mwisho kabisa ikawa na matokeo bora kabisa
Kukata tamaa ni Sumu, endelea kupambana
Ni hayo tu!