Nilivyomliza mke wangu kwa siku 366

Nilivyomliza mke wangu kwa siku 366

Tarehe moja ni sikukuu... Unaomba ruhusa kwa boss ya nini?


Watunzi wa story wawe makini basi.
Mkuu siyo kila MTU anafanya kazi selikalini,, private sector Trh 1 January watu wanaingia kazini mkuu, mfano unaenda hotelini na familia yako sikuku mwaka mpya wanaokuhudumia unadhani hawako kazini??? Think big
 
Mkuu siyo kila MTU anafanya kazi selikalini,, private sector Trh 1 January watu wanaingia kazini mkuu, mfano unaenda hotelini na familia yako sikuku mwaka mpya wanaokuhudumia unadhani hawako kazini??? Think big
Ila ruhusa ya kazi za shift haitolewagi kirahisi unless ubadilishane na mtu.
 
Yan ndo naiona sahz sasa hapa ninaweza kukesha bila kujielewa wallah
 
. aisee . ilikua hamna longolongo kazi murua kabisa thank you.....
 
SEHEMU YA 51

Hebu fikiria, nimetembea na wanawake wote unaowajua wewe! Weupe, weusi, wanene, wafupi, wembamba, warefu, wenye wowowo, vipotabo lakini kote huko, sikupata kitu chochote zaidi ya kumaliza pesa zangu na kukaribia kupata magonjwa.

Walipoondoka, nikamuita Salama na kumshukuru kwa ukarimu wake kwangu na kwa wageni wangu, akaniambia huo ulikuwa wajibu wake na wala hakutakiwa kushukuriwa, yaani ni sawa na daktari kumponya mgonjwa halafu umshukuru, hapana, ule ni wajibu wake, wapo hapo kwa ajili ya kazi ya kuwaponya wagonjwa.
Sikuwa na nafuu, niliendelea kuumwa lakini Salama alikuwa bega kwa bega. Wakati nikiwa naumwa hivyo, wanawake wangu, yaani michepuko ikawa inanitumia meseji kwamba walikuwa wakitaka pesa, yaani hata kunijulia hali walishindwa, hivyo nikaachana nao.
Mimi: Mke wangu! Siwezi kulala peke yangu, naogopa nitakufa.
Salama: Unatakaje?
Mimi: Tulale wote.
Salama: Kweli?
Mimi: Ndiyo!
Salama: Hapana, nimepazoea sebuleni mume wangu, kunanifanya nijisikie amani, huru, naomba niendelee kulala sebuleni.
Mimi: Hapana! Hautakiwi kulala sebuleni tena, wewe ni mke wangu!

Nimekutesa kwa mwaka mzima, siwezi kukubali kukutesa tena, naomba tulale wote.
Salama: Ila kumbuka wewe ni mgonjwa.
Mimi: Najua ila naomba tulale wote.
Kweli usiku wa siku hiyo, kwa mara ya kwanza nikalala na Salama. Sikutaka kufanya kitu, si unajua nilikuwa mgonjwa hoi, nilikuwa mpole tu. Salama hakunifanyia utundu wowote, muda wote alikuwa kimya, hakulala, aliuchukua mto, akauweka nyuma, akauegemea na kisha kunilaza katika mapaja yake.
Hata nilipokuwa nikishtuka usiku wa manane, nilipomwangalia, alikuwa macho akiniangalia tu.
Mimi: Mbona hulali? Saa nane hii?
Salama: Nakulinda, sitaki kulala kwa kuwa unahitaji ulinzi wangu mume wangu! Nisipokulinda mimi, nani atakulinda? Naomba nifanye wajibu wangu!
Nilibaki nikimshangaa, alikuwa mwanamke wa ajabu kabisa. Kama alivyosema, kweli alimaanisha, hakulala, alibaki akinilinda usiku kucha, nilimuonea huruma, alipoamka, kama kawaida akawa ananipetipeti mpaka hali yangu ilipoanza kutengemaa.

Sehemu ya 48 hadi 51 inaonyesha namna ambavyo michepuko sio deal in our daily lives, they are there for destructions and destructions only.

Hii hali ipo sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Nyakati za faraja/mafanikio michepuko ndio inaenjoy ila fedha zinapopiga chenga au maradhi mama nyumbani ndiye anayepata shida na kutusaidia. Wanaume TUJITATHMINI kwakweli....
 
Jamani uzi wa mkufu wa malkia wa Goshen nautafta siku ya pili mpk kichwa kinauma nsaidien jamen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom