Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,170
Mkuje huku Maserati, Tumosa, Money Talk, Tater Evarist Massawe mtu mwembamba koncho77 swahiba92 muya ataho muya Jackal skfull kisukari na wengine jaman mpo wengi mnooo
SEHEMU YA 01-MTUNZI NYEMO CHILONGANI
Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana, nadhani wakati mgumu kuliko nyakati zote nilizowahi kupitia katika maisha yangu. Kilichokuwa kikiendelea kati yangu na msichana mrembo, Isabela ndicho kilichonifanya nigombane na mke wangu, Upendo, tena kutemeana maneno kwa sauti ya juu kabisa.
Alikasirika, ndiyo, hata ningekuwa mimi ningekasirika sana na kama ningekuwa na moyo mwepesi basi ningemuua. Ngoja nikwambie kastori kafupi kuhusu mimi na huyu mrembo Isabela.
Mara ya kwanza nilikutana naye Dar Free Market, kwa kumwangalia tu, alionekana kuwa msichana wa gharama, sista duu ambaye kwa ujumla, nguo na vitu vingine alivyokuwa navyo siku hiyo ingefika gharama ya shilingi milioni moja.
Watu walimwangalia kwa matamanio, uzuri wake wa sura hakika ulimchanganya kila mtu, hakuna aliyemfuata ila kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa najiamini, mifuko imejaa, nikapiga hatua kumfuata.
Watu wote wakanitolea macho, hawakuamini kama kungekuwa na mwanaume aliyekuwa na moyo wa kumfuata na kuzungumza naye, hilo wala sikujali, si nilitaka kuwaonyeshea kwamba watoto wa kike niliwazoea, hivyo nikaamua kufanya hivyo, nilipomfikia tu, nikatoa tabasamu pana, akanirudishia kwa kukunja ndita, sikutishika, nikapiga moyo konde.
Mimi: Mambo vipi mrembo!
Isabela: Poa (Akaendelea kufanya mambo yake mengine)
Dizaini kama hakutaka kuzungumza nami, ila sikutaka kuondoka. Nilikuwa mzoefu sana na watoto wa kike, najua mapozi yao yote yanamaanisha nini na ndiyo maana sikutaka kumuacha kabisa. Nilisimama karibu naye, nami nikajifanya bize kuchagua vitu kumbe akili na mawazo yangu yalikuwa kwake.
Mimi: Umependeza.....(nilimwambia tena huku nikimwangalia, uso wangu ulikuwa na tabasamu pana)
Isabela: (Kimyaaaaa)
Mimi: Umeumbika pia na una uzuri wa ajabu.....
Isabela: (Kimyaaaa)