Nilivyomliza mke wangu kwa siku 366

Nilivyomliza mke wangu kwa siku 366

Lol kumbe ilishaisha Smart911 nae mfukunyuku tehtehteh [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Aliona nilimwekea link mtu akiimaliza hii nitamwekea link nyingine nimeona ni mpenzi wa story
 
SEHEMU YA 52-NYEMO CHILONGANI

Tarehe mbili Januari ndipo nilipopona kabisa, nilimshukuru sana Salama kwa kile alichonifanyia, sikuamini kama kweli, kwa jinsi nilivyomtesa angeweza kunifanyia mambo kama yale, ndiyo kwanza angenikatili na hata kuniulia mbali, ila yeye, walaa hakufanya hivyo!
Mimi: Naomba unisamehe, sasa nipo tayari kuanza maisha na wewe!
Salama: Kweli?
Mimi: Ndiyo! Hakika umefanya kitu nisichokitarajia kabisa, nashukuru sana.
Salama: Asante sana kipenzi....

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya, baada ya hapo, tulikwenda kijijini kuwashukuru wazazi kwa kunipatia mke mwema, wenyewe waliniambia kwamba walihakikisha wananipa mwanamke mzuri, mwenye tabia njema na ndiyo maana walinichagulia huyo.
Basi baada ya mwezi mzima, Salama mke wangu akaniambia ana dalili zote za mimba, sikuamini, tukaenda kupima, kweli akaonekana kuwa mjauzito! Hivi ninavyoongea na wewe, tayari mimi ni baba wa mapacha wawili, wa kike aitwaye Claire na wa kiume aitwaye Clarence.

MWISHO

Ahsanteni kwa kuifuatilia simulizi hii tangu mwanzo mpaka hapa ilipoishia. Bila shaka kuna mengi mmejifunza. Kwa yale mazuri, yachukueni na yawe msaada katika maisha yenu ila kwa yale mabaya, yaacheni.

Tukutane siku nyingine!
Ahsante sana kwa simulizi nzuri sana na yenye mafunzo mapama.
Kwa kwel ipo vizur

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom