Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

tufunge mjadala swala la jamaa kuhusu viza kuisha kuingia lesotho.
rushwa tunayo ijua tz sio rushwa inayoa anzia mpakani mwa zambia na tz yani hapo boda utajua tu sasa hapa kuna nuka rushwa unapotoka tanzania,askari na idala zote tena ngozi nyeusi ni tatizo.
rushwa imekisili kuanzia zambia,zimbabwe mpaka south yani border kama huna pesa hapo betbriji unapita japo kuwa na boda kali.
na wanangu ambao hawana hata passport kila mwaka wanakuja na kurudi.
mimi nimeishi na mda ulikwisha na ni lilipa rand 500 inavushwa boda ina gongwa kutoka na kurudi na safi ,ila ukitumia airport inaweza kukuzingua ila boda za barabara huko ni rushwa kwenda mbele.
sio mzuri sana wa kuandika ila maisha ya kule kama GTA -5.rushwa imetawala sana kwa watu weusi,ufanye kosa ukikuta mtu mweusi askari unampa chake ili kukuacha na nimeona sana.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya kwanza kufika Beit Bridge, mpakani mwa Zimbabwe na South Africa, ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi, Wakenya. Wabongo tulikuwa 4 tu. Wabongo tulipiga mastori kibao, kama watu tuliofahamiana miaka mingi, kumbe ndo ilikuwa mara yetu ya kwanza kukutana.

Tulijichanganya sana na Waburundi na Wakenya. Wazimbabwe hata lugha yao tulikuwa hatuelewi. Dah ilikuwa moment fulani tamu sana.

Pale border Mbongo mmoja hakuruhusiwa kuingia South Africa. Alikamatwa alitaka kutoa rushwa kwa Afisa wa Uhamiaji (Mkaburu) ili apewe miezi 3 ya kuishi kwa Madiba. Huyu mwenzetu aliyekamatwa yeye ilikuwa sio mara yake ya kwanza kuingia South Africa. Ujuaji mwingi ulimponza.

Sisi wengine tuligongewa muhuri wa mwezi 1 tu kuwepo kwa Madiba. Lakini tuliishi zaidi ya Miaka 6, Sio miezi 6, ni miaka 6. Harakati za mtu Mweusi bhana.

Nakumbuka Wabongo wote tulienda kufikia Pretoria kwa jamaa fulani. Kumbuka wote hapo hatujuani, halafu mfukoni nimebakiwa na kama Elfu 50 tu ya Kibongo.

Kati ya sisi tuliotoka Bongo, kuna mwenzetu mmoja anafamiana na huyo jamaa tuliyefikia kwake. Jamaa wa kuitwa Ibra, alitupokea vizuri sana.

Tulikutana na Wabongo kibao pale Pretoria, walituchukua maelezo, tulikutana mpaka na yule demu video queen wa Matonya, wimbo wa Vailet, demu South Africa bado wanamuita Vailet, bado mrembo sana.

Harakati za kuingia mtaani kusaka mishe ndo zikaanzia hapo.

Nilikaa pale ghetto kwa washkaji kama wiki mbili ivi, ndani ya hizi wiki mbili na jamaa zangu tulikuwa tunaenda sana Johannesburg. Mwenyeji wetu alikuwa na rafiki zake wengi huko. Johannesburg na Pretoria sio mbali sana, kwa daladala ni kama dakika 40 tu.

Basi bhana, katika kwenda kwenda Johannesburg siku mmoja kwenye daladala nikawa nimekaa na demu mmoja mkaliii, nikawa namsemesha semesha mara pap akanipa namba yake ya simu. Washkaji zangu wananichora tu.

Mademu wa South Africa wakitongozwa sio wagumu sana kama Dada zetu wa Sinza, siku ya pili demu akawa demu wangu, fasta tukaanza kupanga maisha. Ha ha ha ha

Demu anafanya kazi Bank FNB, pale Midrand njia kama unataka kuelekea Kalfonteen. Baada ya kama siku 4 toka tufahamiane na yule manzi tukaanza kupiga story za jinsi ndoa yetu itakavyokuwa. Jinsi atakavyokuja Bongo kukutana na ndugu zangu, alivyoleta tu stori zake za siku moja atakuja Bongo kukutana na ndugu zangu, mtu wa kwanza kumuwaza alikuwa Mama Riziki, Muuza Vitumbua, Jirani yetu Buza, atakavyoongea mtaa mzima.

Yaan mimi na yule demu ilikuwa ni full uongo uongo tu mpaka demu akajaa. Akaamini kabisa kama kweli mimi ntamuoa.

Zote hizo ni Harakati za Mtu mweusi katika kutafuta sehemu ya kuanzia. Mara siku akanipigia simu akaniambia kwa Kingereza 'Keagan nataka tuishi wote'

Dah

Wadau itaendelea na nyinyi kama mna mastory yenu wekeni hapa Harakati zenu tujifunze



Hii Stori inafanana na haina Kanya wala Kinyesi

Bs tupu
Ni mwenyewe aliianzisha
 
Wakuu hii story pigieni mstari ndio imeishia hapa, alishawahi kuisimulia na haikuwa na wachangiaji lakini hakuimaliza. Kwaiyo fanyeni mambo mengine tu...

Watu washafukua kaburi kilichobaki ni kuchange ID kwishnei
 
Halafu kumbe alikaa Mwezi Sauzi akarudi kula kulala kwao Buza

Kwenye ile Stori anawaponda akina Ibra kwa kupiga kazi kumbe yeye ni Kula kulala bure
 
Naona harufu mbaya hapa unataka kumkimbia jamaa sababu kafukuzwa kazi?
Kwani issue yako ya juice ofisini si inaendelea vizuri
Nan kafukuzw kazi mzee baba! Juic si ilikua miaka ya 2015 huko? Nimkimbie ili iweje? Uwe unasoma unaelewa..unaleta mambo ya nyuz zingine nikimbie niende wap...! Hebu soma vzr uwe unaelewa..nakimbia au nataka kutoa gundu
 
First attempt ya kujilipua ilikuwa United States ...akiwa Nigeria Ila hakufanikiwa..
Anadai Nigeria Hadi bank statements wanakughushia .. Akiwa ubalozini alikamilisha kila kitu ...kufika dirishani akaulizwa kuhusu invitation letter Akawa hajui Ni nini anajiuma uma tuu ..wakamweka ndani ..Kama gaidi...wakamuuliza do you want/like coffee akasema yes wakamuuliza upo hatiani hiyo nguvu/gut ya kunywa coffee unaitoa wapi lastly aliamua kuzungumza ukweli juu ya ugumu wa maisha wakamwambia afuate procedures vizuri ndo aende ...wazungu wakabaki wanacheka ..baada ya kumchukua maelezo na kujiridhisha wakamwachia
Endeleza story mkuu...
 
Back
Top Bottom