Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Ni ndefu hapo Tunduma haujafika bado kubadilisha fedha mpaka Lusaka na hapo chirundu na mkifika beitbriedge (mussina) kuna series nyingine mpaka unaimaliza polokwane mpaka Pretoria kuelekea park station huko yanakoshukia ma bus ya wazim zim itaisha kesho kutwa hii..
 
Ukimaliza itabidi na mimi nitoe yangu ya siku kwenda China kufunga mzigo bila ndugu rafiki wala nini
China ni nyepesi ukiwa na Visa Kuna nini tena na China usalama upo kidogo tofauti na huko alikoenda jamaa kwanza anaenda kutafuta maisha sio kununua mzigo maana kama kununua mzigo napo SA ni rahisi mzigo unanunuliwa sehemu moja tuu dragon city na China City...na China sehemu za kununua ukinunua unawapa jina la kampuni watakayobeba mzigo mimi sijaona kote ugumu wake wengine wanazunguka Singapore,Skorea,Vietnam,Thailand na Cambodia kufunga mizigo na yote ilikua inafika Tanzania kabla ya mzee baba kuharibu mfumo..
 
SEHEMU YA NNE

Kwenye Bus kama kawaida ya Watanzania tulianza kufahamiana na kupiga story za hapa na pale. Wengi wetu ilikuwa ni mara etu ya kwanza kwenda South isipokuwa jamaa mmoja alituambia anaitwa Ahamad yeye ndo ilikuwa kama mara yake ya Tatu kwenda huko na Kuna Dada aliitwa Matlida, ni mtu wa Mbeya ila yeye ilikuwa anaishi South Miaka Mingi. Hata kwenye hii Safari yeye bus alikuja kupandia Mbeya.

Tulifika Boda ya kwanza Tunduma Majira ya saa Sita Usiku. Kulikuwa na Baridi sana. Ukweli Wakuu nitaahadithia kila kitu kama kilivyotokea. Tulivyoshuka pale Tunduma tulipokelewa na Vishoka wengi sana waliokuwa wanakimbilia Abiria ili kuwapa Msaada kwenye zile Ofisi za Uhamiaji. Vishoka walikuwa wengi sana tena walikuwa wanajiamini sana na kuingia mpaka ndani ya Ofisi za Uhamiaji.

Ukweli nilishangaa sababu nilishawai kufika Boda ya HoroHoro kwa Upande wa Tanga, Nilishawai kufika Boda ya Sirari kule Tarime, Boda ya Namanga Arusha pia naifahamu lakini sikuwai kuona Vishoka wanaingia mpaka ndani ya Ofisi za Uhamiaji kama vile unaweza kudhani wao ni Maafisa Uhamiaji.

Niligonga Mhuri wa EXIT kwenye Passport yangu upande wa Tanzania kisha nilikwenda kugonga upande wa Nakonde Zambia. Nakumbuka nilivyofika kwenye ile Kaunta ya yule Dada wa Uhamiaji Upande wa Zambia alinikatalia kugonga muhuri kwa madai kwamba nimuoneshe kama Nina Balance ya Pesa ya kutosha ya kuweza kuishi South Africa. Alisema hayo ndo Matakwa ya Sheria. Kwa wakati ule sikujua kama alichosema ni kweli ama La. Nilimwambia yule Dada kuwa Pesa ninazo kwenye Account ila alikataa, alihoji nina uhakika gani kama kweli kwenye Account una Pesa? Niliwaza labda nilipaswa kutembea na Bank Statement lakini ndo ivo nimeshachelewa.

Yule Dada alivyokataa kunigongea nikasogea pembeni ya ule mstari kupisha wengine waendelee. Nikaona Vishoka kama watatu hivi wananifuata kuniuliza nini Tatizo, Nikawaeleza kuwa yule Dada amekataa kunigongea mhuri. Mmoja ya wale Vishoka nakumbuka akaniambia kazi ndogo sana hiyo, akaingiza mkono wake mfukoni akanipa Kwacha 50 pesa ya Zambia. Akaniambia chukua hii pesa mdogo wangu weka katikati ya Passport yako kama Rushwa halafu rudi tena kwa yule Dada. Nikafanya kama alivyoniambia.
 
Back
Top Bottom