Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Kuna wakati kujilipua kusiwe kama fasheni kwasababu unaona watu wanajilipua, hapana jitahidi uwe na sababu hasa ya kujilipua..

Jitahidi unapotaka kujilipua uwe tayari umepambana vya kutosha humu humu imeshindikana na njia pekee ni kujaribu kwingine, kuna wimbi la vijana wako nje kwa sababu ni sifa kwake kuwa nje na hakuna juhudi alizojaribu kufanya akiwa hapa na hata huko aliko hana anachokifanya zaidi ya kuishi normal life ambayo hata hapa si ajabu ungeweka nguvu kidogo ungefanikiwa..

Kwenye kusafiri kuna namna nyingi, wapo wanaosafiri kwenda kutembea, wapo wanaosafiri kwa kutumia ramani zilizoanzia hapa na kwenda kupiga michongo mbele na kurudi hapa, wapo wanaosafiri baada ya kushindwa kabisa kutoboa hapa...

Umeongea kweli mkuu . .
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafanya hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Hakuna tabu kama kuishi na mtu ambae asubuhi anaamka amenuna bila sababu. Mtapiga story pale atakapojisikia yeye kuongea. Alikuwa Mjinga kweli yule jamaa. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. South Africa chakula bei rahisi. Kule gharama kubwa ipo kwenye Kodi za Nyumba na Nauli kwenye vyombo vya Usafiri. Kule Umbali wa Makumbusho mpaka Posta, Kwa Taxi zao, Kule ukisema Taxi ndio Daladala, unaweza kulipia hata Elfu 2 mpaka 3 za Kitanzania. Hiyo ni nauli ya kwenda tu.

Sasa Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi kula nyumbani. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Lakini Kanya aliniganda kinyama.
 
Ukija kuendelea pia udokeze kidogo namna ulivyofanikiwa kuongeza muda wa kibali chako kukaa huko (maana mwanzoni ulisema ulipewa kibali cha mwezi mmoja tuu). Na harakati zote hizi, na assume kuwa mwezi ulishaisha kitambo. Au kuextend muda wa kibali ukiwa huko sio issue sana?
Otherwise, ni story very interesting na yenye mafunzo mengi sana kuhusu harakati za utafutaji na kujilipua kwetu vijana.
Keagan Paul
Mkuu nitarudi kufafanua hii ishu
 
Nimeishi nao nawajua vizuri sio hao tu,asilimia kubwa ya west African kupata viza ya Europe au USA ect ni ngumu sababu ya tabia zao,unasema ni wamoja wanabagua sana kama hujui
Sijui utakuwa umekaa nao kwa muda gani mkuu, lakini kila nchi ina wahuni sijui wewe ulibahatika kuishi na kundi la aina gani mkuu
Maana kila nchi ina wahuni wa aina yake

Binafsi wanaigeria,cameroo,ghana,senegal, nimekaa na marafiki wa sehemu hizo takriban 7 years

Wana walio wengi wengi ni wanaigeria ambao nimekaa nao na wenye uhuni ni hawa wenye hustle za kibabe
Wapo wenye kazi zao ukimwona huwezi hata kujua ni mnaigeria ikubalike east african ladies hasa kenya/tanzania wanawapenda sana kwasababu ya hustle zao wao hawana kuna maali naiskilizia😂😂

Kutokana na uhalifu/utapeli na matukio mengine yanayofanywa na hustlers wao ndo maana visa zao ghali ila siyo ngumu kupata
in short wametuzidi kwenye mengi tu
 
Mkuu Nimecheka Lakini Nakufurahia Sana Comments zako... Kuna kitu unanijenga... Aisee na huu uzee Wangu Huku Kigoma Kasulu Ndani Ndani Huku Kijiji Cha Muyegera Nimetamani Sana Kujilipua. Hapa leo hi naelekea Uhamiaji kuangalia Utaratibu wa Gamba.... Asante Sana
Huo ndo ukweli ndugu yangu. Ukizunguka zunguka duniani utaona jinsi wanaija na wakenya wanatupiga magepu yaani kuna watoto wazazi wao walifanya shughuli za ajabu ajabu wanesomea mambelez huko saiv wana kazi za heshima balaa. Na huwez amin kiakili za darasani tumewaacha mbali sana ngozi nyeupe. Sie tunadumaa kutokana na malezi

Ila mwanao akikulia mbelez wanakujaga kuwa moto sana biashara kubwa au makazi makubwa udaktari mainjinia IT specialists ila watoto wa vibaka wa zamani. Saivi wanarudisha investment nyumbani

Sasa huku wewe unazaliwa masikini unalaani hadi kizazi chako wazaliwe vile vile km ww kwa uoga wa kujilipua

Ndo nimetoa mfano mdogo huo wale wapelelezi waliokuja mwanzoni kabla ya ukoloni unadhani walikua hawaogopi?? Wamekuja sehemu ni misitu tu na stori kuwa watu wanakula nyama za watu hata nguo hatuvai ila wakaja wakatuua wakatukata mikono mpk tukatia akili na wakatutawala kwa manufaa ya nchi zao. Leo hawaonekani kama wahalifu Bali mashujaa
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafasi hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi nyumbani kula. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Kanya oooh kanya ...kanya ohhh kanya...
One time for ma kanya ooh kanya...
 
Back
Top Bottom