Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Gdd Tech

JF-Expert Member
Nov 1, 2018
551
1,000
Huo ndo ukweli ndugu yangu. Ukizunguka zunguka duniani utaona jinsi wanaija na wakenya wanatupiga magepu yaani kuna watoto wazazi wao walifanya shughuli za ajabu ajabu wanesomea mambelez huko saiv wana kazi za heshima balaa. Na huwez amin kiakili za darasani tumewaacha mbali sana ngozi nyeupe. Sie tunadumaa kutokana na malezi

Ila mwanao akikulia mbelez wanakujaga kuwa moto sana biashara kubwa au makazi makubwa udaktari mainjinia IT specialists ila watoto wa vibaka wa zamani. Saivi wanarudisha investment nyumbani

Sasa huku wewe unazaliwa masikini unalaani hadi kizazi chako wazaliwe vile vile km ww kwa uoga wa kujilipua

Ndo nimetoa mfano mdogo huo wale wapelelezi waliokuja mwanzoni kabla ya ukoloni unadhani walikua hawaogopi?? Wamekuja sehemu ni misitu tu na stori kuwa watu wanakula nyama za watu hata nguo hatuvai ila wakaja wakatuua wakatukata mikono mpk tukatia akili na wakatutawala kwa manufaa ya nchi zao. Leo hawaonekani kama wahalifu Bali mashujaa
Thanks Mkuu.... This Year..... Lazima nivuke Boda Kadhaa
 

Hplp2275H

JF-Expert Member
Jan 21, 2021
491
1,000
Wakuu eeh mnawafahamu wasomali...
Umoja wao mnaufahamu?
Umeshawahi onalife lao?
Wanaishi mtaa mmoja..
Wanachukuana kwao kila siku...
Tatizo wanalibeba wote...
Pia nao kwa kujilipua so haba ..border hapa karibu kila siku wanavushwa kwenda Sa ...Baada ya muda wanarudi walionyookewa na maisha wanakuja kuchukua wenzao.. l
Kama wasomali wa hapa border dah Mshikamano wao nimeipenda.

Wabongo tuache ungese
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
31,204
2,000
Hii Kitaalamu tunaitaje mkuu?
900099.jpg
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,556
2,000
@Noelia unajua huwa tunakosea sana sisi wabongo...

Passport ni hati au kibali cha kusafiria na tena kukutambulisha wewe kwa taifa jingine kama ni Mtanzania...

Sasa tujiulize wote tu, kama hauna mpango wa kwenda nchi nyingine, kwa nini uhitaji passport?

Halafu pia restrictions zinakuwa nyingi sababu kuna watu wanatumia passport kufanikisha shughuli zao za kiharamia kama kupitisha madawa ya kulevya n.k, sasa kama taifa huwezi tu kuwa unatoa passport ili kufanikisha mauharamia...

Mfano kipindi tulipokuwa na passport ya zamani (ile ya gamba la kijani), passport ya bongo ilikuwa shamba la bibi, watu wa mataifa mengine waliitumia sana kufanya mambo yao especially kwa zile nchi ambazo mbongo anaingia kwa kupata entry visa airport...
Sasa pamoja na kubana kote huko "kwa RAIA wote wanaostahili" bado wakapewa "Wasiokua RAIA" unadhani ni approach sahihi???

Kwani wanaouaza madawa ya kule vya hapa hapa Tanzania wana passport?? Yaan passport haishusiani na madawa ya kulevya kwanini waihusishe??? Hapo ndo kuna tatizo ni mawazo ya kizamani sana

Okay kama Passport ni document mpaka uwe na safari Ingekua inadumu kwa hiyo safari moja uliyoombea tu halafu inaexpaya. Mtu aliyesafir mara moja tu kihalali anakua nayo kwa miaka 10 kwanini kila mtu anayehitaji asiwe nayo standby?? Mtu akishaomba manaake ana mpango wa safari na ni haki yake apewe. Makosa yatakayofanyika akiwa na hiyo passport atahukumiwa kwa aliyotenda kwann umnyime kwa kudhania "eti" atafanyia uhalifu

Muhalifu ni muhalifu tu akiamua hata asipokua nayo atasafiri tu......
 

Gdd Tech

JF-Expert Member
Nov 1, 2018
551
1,000
Ila tuache Utani JF Ni Raha Sana Yaani Mpaka unakuwa Addicted kabisa Bila Kuingia JF unaona siku haijaenda Kabisa
Mimi (Keagan Paul) nikiwa na akili zangu timamu, naapa kwamba nitasimulia kila kitu kama nilivyoahidi kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Na kwamba nitasimulia mwanzo hadi mwisho bila kuingiwa na tamaa za kuhamia telegram.

Ee mnyaazi Mungu nisaidie.
 

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,890
2,000
Na washarika Tuungane nae Kwa pamoja tuseme ee myaazi Mungu Utusaidie...

Much:Bwana awabariki na kuwalinda.
Awaaangazie Nuru ya uso wake apate kuwafadhili.

Mch: Bwana akae nanyi.
Ush:Akae na roho yako.
Mch:Tummhimidi bwana.
USH:Tumshukuru Mungu....

Mch:Tukienda kulipia matoleo yetu kule telegram Usharika Tuimbe wimbo namba 205 Beti 5..

Baada ya hapo dada Noelia atatuongoza pambio wakati tunamsubir Keagan Paul Aje atupe Uzi wa leo.
Noma sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom