Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Kama nia yako ni kufanya adventure huna haja ya kukimbizana na magari makubwa japo kiukweli ukiwa na boxer na ikiwa imekolea mwendo vizuri unaweza ukatembea umbali mrefu bila kupitwa na magari makubwa.

Binafsi mimi huwa nacheza na side mirror tu muda wote, haiwezi kupita dakika sijaangalia nyuma kuna nini, kama kuna gari kubwa litakuwa nyuma yangu likinikaribia sihangaiki kukimbizana nalo huwa nabana pembeni tu lipite then naendelea na safari yangu.
 
Mkuu hongera sana kwa hiyo adventure I wish ningekujoin ila poa kuna siku na mimi ntasafiri umbali mrefu na mnyama wangu kiboko ya boxer (discover 4valve)

hua naiita the navigator wenye boxer hua wananikoma barabarani na hapa nna mpango niibomoe yote ili niifanyie overhaul

anayejua fundi mzuri kwa dar anifahamishe tafadhaliView attachment 1435376

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda Upanga mtaa wa Ally Khan maeneo karibu na Goete Institute unapoenda kuikuta Ally Hassan Mwinyi kuna mafundi pikipiki. Ukienda Muulize fundi Elisha.

Kinondoni Biafra kuna mafundi pikipiki kubwa uliza fundi Panya.
 
Uzuri mwingine wa boxer haina mitetemo so haichoshi kivile ukienda nayo umbali mrefu.
Next time usitembee usiku bora uweke malengo ya sehemu ya kulala, lala utapokua umefika at 6 PM.

Hongera sana mtoa mada.
Kwa nini asitembee uck wakati barabara ya itigi tabora haina magari

Stay home, stay safe
Corona kills
 
DAR TO ARUSHA.safari ilikua tamu sana hakuna changamoto kama chombo kikiwa % 100 kizima nilitumia masaa nane na full tank mbili
20180618_112147.jpeg
20180618_112303.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge la wazo. Tungekuwa na tabia ya kujiorganize na kufanya safari za namna hii, wallah mnaweza izunguka hii nchi na kuitalii yote. Mnajipa muda wa kutosha, mnaanzia Kilwa, Mtwara, Ruvuma mnaitafuta Mbeya na Iringa, unachapa kichochoro Mnaibukia Dodoma.

mnapanda Singida Kahama, Ushirombo...Uhayani...mnapiga Gear mnabidukia Mwanza, Mara mnaikata kimbugambuga Serengeti inaibukia Arusha, Kilimanjaro Tanga mnachanja ya Saadani mnaibukia Bagamoyo...hapo mnaBwaga Moyo

Mnafikia hospitali kutibiwa migongo
Umeanza vizuri , ila sasa ulipo malizia ndio nimebaki hoi
 
Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Basi huwezi amini , watu wenye magari makubwa ndio wastaarabu sana barabani ukilinganisha na hawa wengine hasa wa private car, na ukiwa barabarani na piki piki usikubali kuwa sambamba na mwenye gari kubwa au lori , hiyo ni kwa utafiti wangu.
 
Kuna jamaa hua anatoka Dar anaenda Malawi na Boxer BM 150 kila siku saa tisa lazima apite hapa kijijini kwetu Soliwaya.
 
Back
Top Bottom