kuanzia ulipo kua mdogo ?
Ndio
Nakumbuka wakati flani
Maeneo ya kwetu kule baridi kali kwa hiyo tunakulia jikoni
Si unajua mazingira ya jiko za vijijin
Nyumba na jiko vipo tofauti
So mama akawa na mgeni ndani na wadogo zangu ndani wanakula
Mi nikabaki jikoni na kulikua kuna baridi
Nikala kidogo tu nikapata hisia kali yaani kama mtu anakusimamisha nikabeba chakula na chai ile nafika mlangoni kuna mti wa mgunga ulikua nyuma ya jiko ulikua ushapekechwa na wadudu aisee ulishuka kwenye bati la jikon kama radi inavyolia ule mti ulilalia jiko na kuharibu vitu ndani sana
So sisahau lile tukio kwa kwel
Na mifano mingi midogo midogo
Naweza nikawa nimelala fofofo nikahisi kuna maji yamemwagika na labda sijayasikia yamemwagika ila najua tu yapo maji
Mimi nisipofua hiyo siku na wewe usifue maana lazima mvua inyeshe
Yaani napata hisia sana
Nilipata mdada mmoja...hakua hata na dalil mbaya
Ila moyo wangu ukaniambia huyu ni mchawi
Kumkagua aiseee ana hadi ungo
Kabla muheshimiwa flan ajapewa sumu niliota atapewa sumu
So nikamuadithia mama yangu
Hadi coment niliiweka kwenye ule uzi
Na alikuja kupewa
Vitu ni vingi ila huwa siweki record