Nilipokuwa mdogo nilikuwa na uwezo wa kufanya Miujiza

Nilipokuwa mdogo nilikuwa na uwezo wa kufanya Miujiza

Hii ni story yangu na nitatoa na mifano ya vitu nilivyowahi kufanya. Watu wengi hawakujua, lakini kuna matukio kadhaa yaliyotokea nikiwa mtoto ambayo hayakuwa ya kawaida kabisa. Haikuwa mara moja ilikuwa vitu ambavyo vilitokea mbele ya watu wengine pia.

Mfano wa kwanza ulikuwa mvua.

Kuna siku anga lilikuwa wazi kabisa. Hakukuwa na dalili ya mvua hata kidogo. Nilisimama nje nikaangalia juu halafu nikasema tu mvua inyeshe. Baada ya muda mfupi, mawingu yakaanza kukusanyika polepole, upepo ukabadilika, halafu mvua ikanesa. Watu walishangaa lakini hawakujua nini kilitokea dakika chache kabla.

Mfano wa pili ulitokea nyumbani.

Kuna siku taa ya chumbani ilikuwa imeharibika kabisa, haikuwaka hata kidogo. Watu walijaribu kuigusa mara kadhaa bila mafanikio. Nilishika tu swichi nikasema iwake, na ghafla taa ikawaka kama kawaida.

Watu walikaa kimya kwa muda.

Mfano wa tatu ulitokea nilipokuwa nje nacheza.

Kulikuwa na kitu kidogo nilichokuwa nacho mkononi kama sarafu. Niliitupa juu halafu kwa sekunde chache ilikaa hewani bila kuanguka mara moja. Ilikuwa kama imesimama kidogo hewani kabla haijarudi chini. Watu wawili waliokuwa karibu waliona hilo.

Walishangaa sana.

Mfano wa nne ndio uliwashangaza zaidi watu wazima.

Kulikuwa na glasi iliyoanguka na kuvunjika vipande vipande. Nilivikusanya vile vipande nikaviweka pamoja, nikavishika kwa mikono yangu kwa sekunde chache… halafu vile vipande vilikaa pamoja tena kama havikuvunjika kabisa.

Watu waliokuwa pale hawakuongea kwa muda.

Na mfano wa tano ndio ulionifanya nijue uwezo huo ulikuwa wa kweli.

Nikikia na uwezo wa kufungua madirisha au milango kwa kuiangalia tu kwa macho na kuifikiria ikiwa inafunguka au kufunga nayo inafanya hivyohivyo kama nilivyoifikiria akilini.

Baada ya hapo, mambo hayo yalianza kupungua polepole kadri nilivyokuwa nakua.

Mpaka sasa ni nadra naona kama yamepotea.

Lakini ukweli ni kuwa…
nilipokua mdogo miujiza ilikuwa inatokea mbele yangu, na wakati mwingine mikononi mwangu kabisa.
chai ya rangi
 
Maisha ninayoishi sasa niliyaona na kuyawish yatokee miaka 20 nyuma. Miaka ya 2000's. Too Bad tangu miaka 2010's nikawa siwez tena kuona mbele. Kila nikiwish naona roho inakataa, mind inagoma kuimagine, mapigo ya moyo hayadund the way yalivyokuwa yanadunda kwenye zile Wishes za nyuma. Na Naona giza mbele.

Na hapo ndio nikajua Sina nguvu tena. 😔😔😔😔😔.

Ngoja nifike 40's niache starehe za dunia na kutuliza Mind tena.
Niwe msafi. Nione kama ntaweza rudisha zile nguvu.😎😎😎😎
 
Mpaka niwe nakufahm
Na sikuot hivyo
Lazima iwe karibu sana
Na sioti direct kwamba ni wewe
Naweza ota tu kwenu kuna msiba
Ila sijui wa nani

Mm nilikuwa naona msiba, na zile character za mtu. Kwahiyo nikisema. Na kama yule mtu anaumwa bas hawez kupona,
Na hao watu kumbuka mim siwajui au sijui kama anaumwa maana nilikuwa mdogo 7-12 yrs hivi.
(Mama ndio anawajua na nikisema nimeona na nikataja mtu anafanaje, Mama ndio alikuwa anaanza kuangua Kilio)

Au naota kuna msiba alaf Flan ambaye ninaemjua analia sana.

Bas huyo mtu atafiwa na mtu wake wa karibu, kwa namna yoyote.
 
Mkuu upo chupa ya ngapi asaivi ni bora ukapumzike tu..
Kwa leo imetosha

Hii naijua hii. Mm nimesoma Cuba 😂😂😂😂

PhotoCollage_1773856951352.jpg
 
Back
Top Bottom