Nilipokuwa mdogo nilikuwa na uwezo wa kufanya Miujiza

Nilipokuwa mdogo nilikuwa na uwezo wa kufanya Miujiza

Hii ni story yangu na nitatoa na mifano ya vitu nilivyowahi kufanya. Watu wengi hawakujua, lakini kuna matukio kadhaa yaliyotokea nikiwa mtoto ambayo hayakuwa ya kawaida kabisa. Haikuwa mara moja ilikuwa vitu ambavyo vilitokea mbele ya watu wengine pia.

Mfano wa kwanza ulikuwa mvua.

Kuna siku anga lilikuwa wazi kabisa. Hakukuwa na dalili ya mvua hata kidogo. Nilisimama nje nikaangalia juu halafu nikasema tu mvua inyeshe. Baada ya muda mfupi, mawingu yakaanza kukusanyika polepole, upepo ukabadilika, halafu mvua ikanesa. Watu walishangaa lakini hawakujua nini kilitokea dakika chache kabla.

Mfano wa pili ulitokea nyumbani.

Kuna siku taa ya chumbani ilikuwa imeharibika kabisa, haikuwaka hata kidogo. Watu walijaribu kuigusa mara kadhaa bila mafanikio. Nilishika tu swichi nikasema iwake, na ghafla taa ikawaka kama kawaida.

Watu walikaa kimya kwa muda.

Mfano wa tatu ulitokea nilipokuwa nje nacheza.

Kulikuwa na kitu kidogo nilichokuwa nacho mkononi kama sarafu. Niliitupa juu halafu kwa sekunde chache ilikaa hewani bila kuanguka mara moja. Ilikuwa kama imesimama kidogo hewani kabla haijarudi chini. Watu wawili waliokuwa karibu waliona hilo.

Walishangaa sana.

Mfano wa nne ndio uliwashangaza zaidi watu wazima.

Kulikuwa na glasi iliyoanguka na kuvunjika vipande vipande. Nilivikusanya vile vipande nikaviweka pamoja, nikavishika kwa mikono yangu kwa sekunde chache… halafu vile vipande vilikaa pamoja tena kama havikuvunjika kabisa.

Watu waliokuwa pale hawakuongea kwa muda.

Na mfano wa tano ndio ulionifanya nijue uwezo huo ulikuwa wa kweli.

Nikikia na uwezo wa kufungua madirisha au milango kwa kuiangalia tu kwa macho na kuifikiria ikiwa inafunguka au kufunga nayo inafanya hivyohivyo kama nilivyoifikiria akilini.

Baada ya hapo, mambo hayo yalianza kupungua polepole kadri nilivyokuwa nakua.

Mpaka sasa ni nadra naona kama yamepotea.

Lakini ukweli ni kuwa…
nilipokua mdogo miujiza ilikuwa inatokea mbele yangu, na wakati mwingine mikononi mwangu kabisa.
 
sijui ni nini natafuta njia ya kurudisha ili niweze tena
Kurudi sidhani kama ni rahisi, back in the day nilikuwa na uwezo wa ku predict kinachokuja kutokea mbele yangu yaani sometimes images kabisa naziona. Sixth sense I mean ambayo kwa sasa kwangu imepotea, maisha ya deals kama unaweza ku sense 💰 au ku sense danger huwa ni faida sana lakini ikipotea hiyo ni songombingo tupu kwenye harakati husika.
Nilishawahi kuuliza sababu ya nguvu za aina hiyo kuwepo(normally I don't believe in things that cannot be proved scientifically so this is a tag of war within me) nikaambiwa kuwa you only possess those kinds of powers when you are 'clean and pure'.
 
Kurudi sidhani kama ni rahisi, back in the day nilikuwa na uwezo wa ku predict kinachokuja kutokea mbele yangu yaani sometimes images kabisa naziona. Sixth sense I mean ambayo kwa sasa kwangu imepotea, maisha ya deals kama unaweza ku sense 💰 au ku sense danger huwa ni faida sana lakini ikipotea hiyo ni songombingo tupu kwenye harakati husika.
Nilishawahi kuuliza sababu ya nguvu za aina hiyo kuwepo(normally I don't believe in things that cannot be proved scientifically so this is a tag of war within me) nikaambiwa kuwa you only possess those kinds of powers when you are 'clean and pure'.

Nazingatia hapo kwenye "Clean and Pure".

chai ya rangi , mim Nakuamini except mfano wako wa nne .(mgumu sana😎😎😎)

Mm pia nilikuwa nina kanguvu fulan.
Mfano nilikuwa naweza kuota ndoto na zikatokea kweli,. Watu wa karibu kabla ya kufa nilikuwa naona wiki 2 au 3 kabla. Awe anaumwa au kufa gafla au ajali. Nikiota na nikimwambia Mama alikuwa anaanza kulia. Na wiki za mbele msiba unatokea kweli.
Nadhan Misiba inaweza fika 10+ kidogo niliyoiona.

pia Hiyo ya Mvua nilikuwa naweza. Na wingu likitanda nikinuia jua liwake linawaka kali ndan ya sekunde chache tu.
Kufungua milango nilikuwa naweza pia.
Kunuia kitu na kikatokea nilikuwa naweza pia.
nakumbuka form 4 niligombana na washkaj kadhaa (walikuwa wananionea bwenini na kunichezea rafu uwanjan) na nikanuia wapate zero na wote walipata. Watu kama 5 hiv 😎😎😎😎.

Na mengne meng nilinuia na yakatokea.

Na hapa sio kwamba ni dini au uchawi. Hapana. Nasema tu "Mungu naomba hivi na hivi" then unatulia na ukikumbuka unaomba tena, na baadae kinatokea.

Too Bad nimepoteza hiyo Nguvu kwa miaka Mingi sasa.

So nakuamin Bro. Hivyo vitu viko.
 
Back
Top Bottom