Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

ndugu zangu mwenye uzoefu wa biashara ya mtumba kwa mkoa wowote ambao unatoa sana bidhaa hii naomba anijulishe na anipe ni nguo gani naweza anza nazo.
 
We sema tu binadamu kwa ujumla.

Wala sio wanaume peke yao.
Haya mapenzi ya kuwaza bettering partners ndo upendo inafanyika tu pande zote.
Nimeangalia upande kulingana na alichosimulia mtoa mada "yeye ni mwanaume" hata kama angekuja mdada nae angesimulia kama hivyo basi niangalia pia upande wa wanawake.
 
Pole broo .....lakini mbona kila siku tunawaambia humu kuwa mwanaume ishi maisha yako kwanza mbona hamuelewi.....? Tatizo ni ubishi na kujiona nyie ndio romantiki sana kushinda babu zenu na baba zenu....! Inauma sana ila ndio ishakuwa tutafanyaje sasa ...
Kama huo ujumbe huwa mnasemea humu basi haufikii walengwa
 
Pole ndugu, kuna jamaa yangu alikuwa anamla demu posho ya wiki demu, yalio mkuta acha kabisa hivi viumbe tuishi nao kwa akili kubwa
 
Habarini


Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.


mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.


Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.



Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.


siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.


sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango


Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.



baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.


baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu


baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.


Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

ewe maisha nilikukosea nini?
Pole sana chapati mbili na chai moja
 
Mkuu chapati 2, pole sana
Vipi tangu upate matatizo ulishawahi kukaa kuongea na NAIMA,
 
Pole sana inasikitisha sana,
Ila jamani mchumba hasomeshwi,,
Pia mpenzi or mtarajiwa hafunguliwi miradi ,,
Hayo yote yafaa yatekelezwe na wazazi wake sometimes wanaume tuache viherehere tutaishia jera kwa kufanya matukio ya ajabu kisa kulipa visasi
 
Mzee acha kumsingizia Mungu. Mwenyezi Mungu alitupa akili na utashi ndani yake, na akaja kutuagiza tuishi nao kwa akili pia . Sasa wewe mwenyewe maisha bado yalikua hayajatengamaa ukaona haitoshi wewe ndio wewe unaakili zaidi ya wazazi wake na kujipa majukumu yasiyo yako ya kuanza kukopa ili umridhishe yeye na wakati huo huyo Mwenyezi Mungu mwenyewe katuagiza kuwa wema usizidi kipimo, sasa hapo bwana mkubwa wa kumlaumu nani.........?

Cha kufanya kaa chini jikubali kuwa wewe ndio fala na ufala wako ndio ulio pelekea yote hayo na hakuna wa kumlaumu.

Na siku nyingine uwe mwalimu mzuri kwa wadogo zako wa kiume kuwa mwanaume tengeneza maisha yako kwanza na pesa unazo pata ni kwa ajiri yako na wanao hitaji msaada wako tu.

Hapa naweza kukuonea huruma lakini kumbe wewe ulipo pata hiyo kazi ndio ilikua chanzo cha kuwatelekeza wazazi wako na kuja kupenda malaya na hayo ndio malipo yako baada ya huzuni za wazazi wako.

Bro you have no one to blame except for.
Ukweli mchungu huu
 
Pole sana,
Maisha yana mitihani mingi
Najua umejeruhiwa moyo na nafsi,.lakini Mungu ni mponyaji na mfariji mkuu na tena ana jua sababu ya kila jambo ambalo tunalipitia maishani

Mkabidhi Mungu na umwombe akuwezeshe kusamehe na kusahau kumbukumbu mbaya zinazokupa huzuni ndani ya moyo wako

Ukisamehe, amini kwamba Mungu atakufungulia mlango mwingine wa baraka na furaha,hali ya ulemavu isikufikirishe inaweza mpata binadamu yeyote

Jambo moja, kwa sasa unaweza kufanya kazi gani au shughuli gani ili uweze kuendesha maisha yako pasipo kumtegemea mtu? Pengine una wazo na huna mtaji, naamini wasamaria wema hapa tunaweza kushikamana tukakuwezesha chochote kitu ili uweze kusimama tena

Mungu ni hakimu mkuu
 
Back
Top Bottom