Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Mkuu chapati 2, pole sana
Vipi tangu upate matatizo ulishawahi kukaa kuongea na NAIMA,
sijawahi pata wasaa wa kuwasiliana nae maana hata ukitumia rafiki zake wanasema hawana mawasiliano nae, ila nauhakika anajua hali yangu
 
Pole sana,
Maisha yana mitihani mingi
Najua umejeruhiwa moyo na nafsi,.lakini Mungu ni mponyaji na mfariji mkuu na tena ana jua sababu ya kila jambo ambalo tunalipitia maishani

Mkabidhi Mungu na umwombe akuwezeshe kusamehe na kusahau kumbukumbu mbaya zinazokupa huzuni ndani ya moyo wako

Ukisamehe, amini kwamba Mungu atakufungulia mlango mwingine wa baraka na furaha,hali ya ulemavu isikufikirishe inaweza mpata binadamu yeyote

Jambo moja, kwa sasa unaweza kufanya kazi gani au shughuli gani ili uweze kuendesha maisha yako pasipo kumtegemea mtu? Pengine una wazo na huna mtaji, naamini wasamaria wema hapa tunaweza kushikamana tukakuwezesha chochote kitu ili uweze kusimama tena

Mungu ni hakimu mkuu
Asante mkuu naimani Mungu ataniwezesha kusamehe na kusahau.

Kuhusu mtaji kwakweli nashukuru kwa wema huo ninamtaji wa laki 6 na naona inanitosha kuanza biashara ya mtumba japo mkoa zinapouzika sana na nguo gani zinauzika sana ndio nakosa taarifa sahihi
 
Hongera kwa kujipanga, naamini wadau wenye uzoefu wa biashara ya nguo wanaweza kukusaidia hapa ukapata taarifa sahihi za kufanikisha nia yako

Be blesse
 
sijawahi pata wasaa wa kuwasiliana nae maana hata ukitumia rafiki zake wanasema hawana mawasiliano nae, ila nauhakika anajua hali yangu
Daaah huyu mwenzangu sijui ana moyo gani, najua hawezi kurudisha viungo vyako
Lkn km angejishusha na kukuomba msamaha pengine ingekusaidia wewe kupata ahueni moyoni na yeye pia aondokane na mabalaa sababu ya manunguniko yako

Kwa sasa jitahidi kuomba Mungu upate mke atakaye kupenda wewe kwa dhati , na kama unaye focus na huyo kwa sasa
Ubarikiwe
 
asante ndugu Mungu akijaalia itakuwa hivyo maana yote yanawezekana kwake.
 
Habarini

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu

baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

ewe maisha nilikukosea nini?
Watu twaweza toa pole kumbe utunzi wa shigongo.
 
Mapenzi upofu.
 
Unayo nafasi ya pili kwenye maisha

Fungua moyo wako narudi Tena fungua moyo wako katu usikatishe maisha yako

Bado unayo thamani kubwa katika haya maisha .

Move on focus on yourself and work

Msamehe na na malipo yake atayapata hapa hapa dunia
 
Back
Top Bottom