asante ndugu nakujaNaomba mawasiliano yako PM, then nitakupa maelekezo mengine huko
asante ndugu ila kuhusu deni la bank kiwanja kiliuzwa, pia sikuwa vibaya sana nikalipa ila ndio nikabakia sina kitu kabisa.Pole Sana mkuu
Ila kuhusu suala la deni naamini benk nyingi Zina kipengele cha disability kama security ya kutokuendelea ila lazima iwe permanent na iathiri ufanisi wako wa kazi
Ivo fuatilia mkataba maana uwa hatusomagi
TRUST NO BODY EVEN UR SHADOW
asante dadapole kaka
Kwa kujazi nakushauri ifanye haya..
1. Kama unatumia pombe ili kuondoa mawazo acha!
2. Tafuta hobby ya kukukip busy! Nashauri anza kushabikia mpira! Tafuta timu ya kushabikia, nakushauri kama huna timu anza kushabikia man united na simba kwa bongo!
Yani ikifika weekend jichanganye kwenye kibanda umiza kama huna tv!
Ukitoka hapo akili itakua imetuliaaaa... rudi geto jipange kwa ajili ya kesho!!
3. Anza kuangalia namna ya kujiajiri. Tumia muda mwingi kuweka akili yako kwenye biashara yako.
4. Kaa mbali na mapenzi kwa sasa.
5. Futa kila kitu kinacho muhusu huyo mwanamke... kuanzia namba mpaka picha.. hii ndio hatua ya kwanza ya kumsahau (actually hii nlitaka kuiweka namba moja...)
6. Anza kuwa karibu na Mungu (Muhimu).
Pole sana na nikutakie kila heri.
Mshana Jr Divine... Heaven Sent et al.,
asante mkuu ndio maisha yenyeweKuna wanawake wana roho ngumu sana aisee.
Jitahidi umsamehe mkuu,usonge na maisha
Ndugu, unasema "Bado unalia sana". Pole sana, lakini sasa USILIE TENA. Bado una uzima japo sio 100%. Uchungu na hasira na huzuni yote uliyo nayo, iweke kwenye kupambana na maisha hadi ufanikiwe sana.Habarini
Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.
mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.
Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.
Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.
siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.
sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango
Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.
baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.
baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu
baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.
Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.
ewe maisha nilikukosea nini?
Nitakuombea lkni na wewe inabidi ukubali kuachilia uchungu ulionao mkuu ndipo maombi yatafanya kazi.pole sana
asante naumia ila ndio maisha yenyewe ndugu yanguUmeongea kwa hisia sana Kaka,Inaumiza sana,Lakini mtumainie Mungu bro atakushindia katika mengi haya maisha kuna wakati yanatugeuka na kutuumiza lakini tumtazame Mungu analo tumaini letu
Honestly nimeumia sana
Hii
Testimony yako inahuzunisha sana. Imenisilitisha sana. Kiukweli umepitia mengi sana hadi leo. Nakushauri uangalie NGOs zinazotoa misaada kwa walemavu. Wasiliana nao wakusaidie. Wanatoa hata grants za mitaji nk. Sio kirahisi sana, lakini usikate tamaa ukiambiwa hapana hapa na pale. Mwishowe utafanikiwa.
Kiukweli watu wengi mapenzi yanawaharibia maisha. Kuna hata watu wanajiua sababu ya mapenzi. Naomba kuanzia sasa ugundue kwamba matatizo yanatokea katika maisha ili KUTUIMARISHA. Wazungu wanasema, whatever doesn't kill you, makes you stronger. Tatizo sasa ni kwamba kwa baadhi ya watu.. badala ya janga la maisha kukuimarisha linakudhoofisha.
Hapo ndio kosa ulilolifanya ulivyomkuta mpenzi yuko na best yako. Ujue ulemavu wako wala yeye hajali, na hata ungekufa, asingejali. Hakuna mtu wa kujali maisha yako, malengo yako, na mapambano yako zaidi yako ww binafsi. ULIRUHUSU AKAKUCHANGANYA AKILI, HADI UKASAHAU UNAVUKA BARABARA.
Binafsi, natumia changamoto kama hizo zinakuwa MOTO katika maisha yangu ya kuendelea mbele na kufanikiwa sana, na kuwaangamiza kabisa kimawazo wanaonitakia ubaya. T Woods alisema winning takes care of everything.
Inatakiwa mtu kama huyo anakufanya unakuwa IMARA, hata kama inaumaje.. usiruhusu malengo yake ya kukurudisha nyuma yakatimia. Kumbuka ukitetereka NDIO RAHA YAKE
Ndugu, unasema "Bado unalia sana". Pole sana, lakini sada USILIE TENA. Bado una uzima japo sio 100%. Uchungu na hasira na huzuni yote uliyo nayo, iweke kwenye kupambana na maisha hadi ufanikiwe sana.
Hebu chukua mahari umkabidhi kwangu nami ntamkabidhi dunia na vilivyomoHapa naona 90% ya wachangiaji mnaishia kumlaumu mleta mada, lakini mnasahau kwamba huu sio wakati sahihi wa kumlaumu zaidi mlipaswa mumfariji na kumshauri the way forward.
Watu wengi mnasahau kwamba mistakes wengi tunazifanya wakati tupo deep in love, lakini bahati njema/mbaya wengi wetu makosa yetu wengi hawayafahamu na hatuja yaandikia threads hapa jf.
Alafu nanyi akinadada, ebu hata mmoja basi ampende jamaa mleta mada maana yupo singo na mwamba anaonekana ni mwenye upendo wa dhati kabisa. Hana wenge kama akina mimi...![]()
Hilo tu....Hebu chukua mahari umkabidhi kwangu nami ntamkabidhi dunia na vilivyomo
Amen ndugu yangu naimani ipo siku yataishaA very touching story.Ki-umri nipo sawa na wewe ila kwa uliyopitia na unayoendelea kuyapitia ni mazito sana ndg yangu M/Mungu akupe uvumilivu na subra kama vitabu vya dini vinavyotusihi.
Muda wote kiumbe kiitwacho mwanamke au kiumbe chochote chenye jinsia ya kike kiogope sana because generally they have short sight on how to see things.
Usije ukajaribu katika maisha yako katika kiumbe hiki ukawekeza moyo wako,mali zako,siri zako au hata uaminifu kwake ni jamii isiyo na shukrani kabisa though sio wote ila naamini 95% hawana shukrani yaani wamejawa na tamaa.
Ulikosea sana ulipoamua kuwekeza 7.M kwake ili afanye biashara lakini asivyo na shukrani amekusaliti mbele ya rafiki yako then uka-panic na kupata ulemavu ambao hukua nao katika kipindi cha kuzaliwa.
Jipe moyo ndg yangu naamini utashinda kwani ulemavu sio mwisho wa maisha.