Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
996
1,000
Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?
Pole
 

qarem

JF-Expert Member
Oct 19, 2018
430
500
Imagine kuna mwanamke alinumiza moyo wangu mpk sasa nashindwa kumsamehe he wewe uliepata majanga ya ulemavu for life utamsamehe?

Mmh pole sana lakini Mara nyingi wanaume huwa tunajitakia wenyewe,mkopo kwa mpenz kwel?
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
19,013
2,000
Imagine kuna mwanamke alinumiza moyo wangu mpk sasa nashindwa kumsamehe he wewe uliepata majanga ya ulemavu for life utamsamehe???

Mmh pole sana lakini Mara nyingi wanaume huwa tunajitakia wenyewe,mkopo kwa mpenz kwel???
Songa na maisha mengine sahau, kutosamehe ni kuongeza sumu
 

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
803
1,000
Pole sana mkuu! Amini Mungu hatokuacha kamwe, mtumainie yeye yuko katika mtihani wa maisha! Kuna usemi unasema ....Sometimes God lets you pass through certain hardship so that you learn something!
Amini kabisa Mungu ana maana makusudi yake na hali unayopitia! Kumbuka hapa duniani sisi sote ni wapita njia! Anyway Mungu akufanyie wepesi wa kila jambo, ila nimepata uchungu mkubwa sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom