Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Habarini

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu

baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

ewe maisha nilikukosea nini?
Mkuu pole saaan. Ulicho andika hapa ni funzo hata kwetu sisi ambao bado hatujaingia kweny mahusiano. Usikate tamaa huu ni mda mwafaka wa ww kuomba toba kwa mumba wako naamini atafanya njia pasipo na njia. Pia msameh huyo mwanamke kutoka moyoni maan hata mungu hatoweza kukubariki na kufanya njia kwako ile hali umebeba watu moyoni mwako. Ilo ni pito yu na kumbuka hakuna jaribio ninalo kuja kwetu ambalo ni kubwa kiasi kwamba tutashindwa kulifuka. Trust in god and forgive baada ya ww kufanya hvyoo trust me utaona Baraka zake mungu zitakavyo kumiminikia. Samehe kwanza mkuu wangu
 
asante ndugu yangu naumia ila haisaidii kitu
Kwakua hili umelitambua, basi samehe (najua ni ngumu kusahau) kisha anza maisha mapya kana kwamba ndio unaanza moja.
Usiangalie kwamba una ulemavu, bali jitazame kama binaadam. Na usipoteze muda wako kumfikiria huyo binti alieku jeruhi maana utaongeza tatizo la sonona ndani yako.
Nina hakika utakuja kumpata atakae kupenda kwa dhati, kikubwa ni kuomba uzima na afya njema.
 
Pole sana kama ni kweli
Ifikie wakati sasa wanaume tujitambue, kwani wewe sio wa kwanza kupatwa na mkasa kama huo kwenye maisha, kabla ya kuangalia utamsaidiaje mwanamke umpendae ili kuweza kujikwamua kwenye lindi la umaskini, basi ni vyema kuanza kujipanga na kujiimarisha mwenyewe katika maisha yako kwa kuwa na mikakati na mipango imara.

Hii itatusaidia pale ambapo uliejitolea kumsidia hata asipokujali basi maisha yako hayatotetereka wala kuyumba.

Wanaume tunajiona tuna upendo kiasi kwamba tunajisahau kupenda maisha yetu na kuhamishia upendo wote na kutaka kuwajengea maisha bora tuwapendao, hii tabia mara nyingi huwa inatucost pale tunapopatwa na majanga kwani hao tunaowajengea upendo huwa hawana upendo wa dhati kwetu.

Tuachane na hawa viumbe, wajengewe upendo na familia zao tusiwe watu wa kutumika kama daraja na badala yake mwanamke baada ya kupata mafanikio kiasi wanatuona sisi kama takataka. Na endapo tukipatwa na matatizo ndio wanatuacha njiani kama hawatujui na badala yake ana move on kuelekea kwa mwengine.

Tujifunze kutokana na makosa ya watangu wetu, naamini hata wewe ulishawahi kusikia/kuona mwengine kupatwa na mkasa kama huo kabla yako lakini hukujifunza na kuhisi hautakuwa miongoni mwa watakaopatwa na mkasa kama huo.

Pole sana
Genious
 
Asante kaka hakika neno lako la baraka likafanikiwe kwangu nisimame tena vizuri
Kitu nilichojifunza in life, kila binadamu anabadilika na haijalishi utawapa nini ambacho unadhani kitawafunga in life lakini wakikutana na watu au mazingira mengine watabadilika tu.. so, usijilaumu kwa kuwa mwema au kuyalaani maisha yako maana ndio uhalisia wa dunia ilivyo

Pia Pole sana maana naelewa unachokipitia lakini usijilaumu kwa yaliyotokea au kwa ulivyopoteza maana mara nyingine maisha hutufundisha masomo tunayoyahitaji kwa njia ngumu sana kama yako. hivyo Jifunze kwa ulipokosea na uanze kuhesabu kila baraka iliyobakia katika maisha yako na utajifunza kuyapenda tena kama yalivyo.

Naamini utakaa poa brother
 
Hakuna ajuae kesho yake na kupotea njia ndio kujua njia. Na wengi wetu huwa tunaamini yaliyotokea ni mipango ya Mungu, hivyo ni sehemu ya mitihani ya dunia. Msamehe kwa yaliyotokea, huwezi kujua pia Mungu amekupangia nini kurudisha furaha yako.
Mshukuru Mungu kwa kila jambo.
Asante ndugu naimani nitasamehe na kusahau japo sio rahisi
 
Mkuu yameshatokea huwezi rudisha wakati nyuma.msahau,samehe move on na maisha yako
Jiweke karibu na Mungu atakulinda,atakubariki,atakuinua kwa viwango vingine.una ulemavu wa sikio na mguu sio wa akili.bado una uwezo wa kufanya mambo makubwa
Utafanikiwa,utapata mke mwema,utapata familia bora..yote yanawezekana ukiamini na kumtanguliza Mungu.
Samehe jifanye mjinga ili uruhusu baraka zitue katika maisha yako.
Amen asante sana kwa neno hili la faraja.
 
Pole sana kama ni kweli
Ifikie wakati sasa wanaume tujitambue, kwani wewe sio wa kwanza kupatwa na mkasa kama huo kwenye maisha, kabla ya kuangalia utamsaidiaje mwanamke umpendae ili kuweza kujikwamua kwenye lindi la umaskini, basi ni vyema kuanza kujipanga na kujiimarisha mwenyewe katika maisha yako kwa kuwa na mikakati na mipango imara.

Hii itatusaidia pale ambapo uliejitolea kumsidia hata asipokujali basi maisha yako hayatotetereka wala kuyumba.

Wanaume tunajiona tuna upendo kiasi kwamba tunajisahau kupenda maisha yetu na kuhamishia upendo wote na kutaka kuwajengea maisha bora tuwapendao, hii tabia mara nyingi huwa inatucost pale tunapopatwa na majanga kwani hao tunaowajengea upendo huwa hawana upendo wa dhati kwetu.

Tuachane na hawa viumbe, wajengewe upendo na familia zao tusiwe watu wa kutumika kama daraja na badala yake mwanamke baada ya kupata mafanikio kiasi wanatuona sisi kama takataka. Na endapo tukipatwa na matatizo ndio wanatuacha njiani kama hawatujui na badala yake ana move on kuelekea kwa mwengine.

Tujifunze kutokana na makosa ya watangu wetu, naamini hata wewe ulishawahi kusikia/kuona mwengine kupatwa na mkasa kama huo kabla yako lakini hukujifunza na kuhisi hautakuwa miongoni mwa watakaopatwa na mkasa kama huo.

Pole sana
We sema tu binadamu kwa ujumla.

Wala sio wanaume peke yao.
Haya mapenzi ya kuwaza bettering partners ndo upendo inafanyika tu pande zote.
 
Kusahau haiwezekani ila kuweka kinyongo na chuki kwa mtu asiyejali maumivu yako ni sawa na kujiumiza mwenyewe kama unavyofanya sasa.
Yeye kashaendelea na maisha yake na wewe inakupasa kufanya hivyo pia yaani hakuna njia nyingine

naelewa Kitu kibaya kuhusu watu wema kama wewe ni kudhani kila binadamu ana utu na wema kiasi cha kutokuweza kuendelea na maisha yake akimuumiza mtu.. Si kweli kabsaa maana kuna watu hawajali maumivu ya watu wengine, Cha msingi usijiumize walq kujidhuru kwa ubaya wa mtu mwingine. Jitahidi uendelee na maisha yako na yeye atanyooshwa na maisha yake mwenyewe
Shukrani kwa ushauri ndugu nitafanyia kazi ushauri wako
 
Hapa naona 90% ya wachangiaji mnaishia kumlaumu mleta mada, lakini mnasahau kwamba huu sio wakati sahihi wa kumlaumu zaidi mlipaswa mumfariji na kumshauri the way forward.
Watu wengi mnasahau kwamba mistakes wengi tunazifanya wakati tupo deep in love, lakini bahati njema/mbaya wengi wetu makosa yetu wengi hawayafahamu na hatuja yaandikia threads hapa jf.
Alafu nanyi akinadada, ebu hata mmoja basi ampende jamaa mleta mada maana yupo singo na mwamba anaonekana ni mwenye upendo wa dhati kabisa. Hana wenge kama akina mimi...🤸🤸
 
Mkuu pole saaan. Ulicho andika hapa ni funzo hata kwetu sisi ambao bado hatujaingia kweny mahusiano. Usikate tamaa huu ni mda mwafaka wa ww kuomba toba kwa mumba wako naamini atafanya njia pasipo na njia. Pia msameh huyo mwanamke kutoka moyoni maan hata mungu hatoweza kukubariki na kufanya njia kwako ile hali umebeba watu moyoni mwako. Ilo ni pito yu na kumbuka hakuna jaribio ninalo kuja kwetu ambalo ni kubwa kiasi kwamba tutashindwa kulifuka. Trust in god and forgive baada ya ww kufanya hvyoo trust me utaona Baraka zake mungu zitakavyo kumiminikia. Samehe kwanza mkuu wangu
asante ndugu naomba Mungu anipe nguvu ya kusamehe na kushaau kwani inaniwia vigumu sana kusamehe nimejitahidi ila nashindwa
 
Kwakua hili umelitambua, basi samehe (najua ni ngumu kusahau) kisha anza maisha mapya kana kwamba ndio unaanza moja.
Usiangalie kwamba una ulemavu, bali jitazame kama binaadam. Na usipoteze muda wako kumfikiria huyo binti alieku jeruhi maana utaongeza tatizo la sonona ndani yako.
Nina hakika utakuja kumpata atakae kupenda kwa dhati, kikubwa ni kuomba uzima na afya njema.
asante ndugu yangu Mungu anisaidie nisamehe
 
Daaahh mapenzi haya jaman.......nimuhimu Sanaa mtu kujifunza mapema namna ya kuruhusu mapenzi yasikutawale......na hii imenipa nguvu kuendelea kuwa hii tabia yako ya mim kuonekana sipo romantic na Wala sijui kujali...

Natamkiwa hii kauli karibu kwa kila mwanamke ninae kuwa nae kwnye mahusiano...!!
Haikua hivi mwanzo.....nilianza kuwa hivi baada ya kugundua mapenzi yanaweza kuniharibia maisha yangu Kama nikiendekeza kuyaabudu.

Hata mke wangu asije tegemea kwamba love yangu kwake itavuka beyond 70%......never....!!!

Mwanamke hata umpende vipi!! Umjali vipi!!! Kitandani umfanye kwa mastyl yote tena kwa rate ya 1hr/bao........bado itafika tu time atakuletea pigo za usaliti na dharau...

Na tangu niutrain ubongo na moyo wangu kuwa hivi,,,,,,imekuwa very easy to let it go......!!!
Yani nikishaona tu mwanamke kaanza kubadilika vitabia, majibu ya hivyo, misunderstanding, dharau, poor communication.....basi fasta sana napiga u-turn na kuendelea kula maisha katika njia zingine.
Na Cha ajabu ni kwamba hii imekua Kama dawa katika mahusiano yangu.....wengi wao wamekua wakijirudi baada ya kugundua wananiletea ujinga wakitegemea ntateseka kumbe holaahhhh.......

That is my principle!!!

Pole Sanaa ndugu yangu kwa yalio kukuta....Mungu akasimame na ww
 
Back
Top Bottom