Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,331
- 7,885
Pole sana kaka. Yaani pole nyingi nimeumia kweli utafikiri tumetoka tumbo moja... Naamini kwa muda wote huo ulikuwa umeshaanza kumsahau lakini baada ya kuskia hili tukio la yeye kuolewa ndio ikaamsha maumivu upya mpaka kufikia hatua ya kuandika huu uzi.Habarini
Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.
mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.
Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.
Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.
siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.
sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango
Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.
baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.
baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu
baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.
Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.
ewe maisha nilikukosea nini?
Nachelea kusema huu uzi utakupa ahueni kubwa sana na kama ulikuwa huna hamu ya kula basi leo utakula.
Nachokuomba usije ukathubutu kufuatilia tena habari zake tena, maana chochote kinachompa furaha upande wako wewe itakuwa ni maumivu. Hii ni kawaida kwa binadamu karibu wote tuko hivyo, kuwatakia mabaya waliotukosea na ikiwa tofauti basi tunaumia.
Huwa naamini binadamu yoyote ambaye bado hajakata punzi, Basi anaweza akaishi na furaha regardless his/her physicality.
Cha msingi tu tafuta mfumo mzuri wa maisha unaoendana na hali uliyonayo utakao ku-keep busy kiakili kiasi kwamba haitakuwa rahisi kwa wewe kufikiria mikasa mibaya iliyowahi kukukumba huko nyuma.
Halafu hii mikasa imekuwa mingi Sana siku hizi... Aisee Kuna haja ya sisi wanaume kupeana seminar namna ya kuishi na hawa viumbe nyakati hizi hili matukio kama haya yasiendelee kutokea.
Wanawake wa Leo sio Kama mama zetu.
Women are no longer the way they used to be back in old days.
Gone are the days when men give the huge sacrifices for women's interest and women reciprocate by being loyal and treat men like Kings.
Now days things are way different, you treat your woman like a queen, she treats you like trash in return.
Wanawake wana kitu kimoja kinaitwa natural state of hypergamy, na ndicho kilichoku-cost wewe na wenzako wengi sana.
Kuna siku nitakizungumzia kwa mapana jinsi gani ya kukitambua kwa haraka na kufanya maamuzi sahihi kabla hujawa muhanga.
Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
