UVCCM, tafadhali, jifunzeni siasa na muwe wastaarabu

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kuna chapisho langu Moja niliwahi kuhoji kwa Nini vijana wa CCM ni washari na Wana ujasiri uliopitiliza ( over confidence).

Kwa sababu ya yanayoendelea chini ya kapeti naomba kushauri ngazi za juu za CCM kuchunguza mienendo ya vijana wao, maana it is too much now.

Nimesema ngazi za juu kwa sababu, nataka kupata ushawishi kwamba ngazi za chini na hasa kuanzia wilaya, kushuka chini Hawa ndiyo waratibu wa mambo mabaya ambao hawa vijana wanafanya.

Hapa nyuma kidogo, Chadema walikuwa na maandamano yao. Of course, kama chama na kwa sababu ni siasa, ilibidi wafanye publicity. Waliweka bendera zao mahali mahali na vipeperushi.

Huwezi amini, kulikuwa na operation ya makusudi kabisa ya vijana wa CCM kuondoa matangazo na hata kushusha na kuondoka na bendera na vipeperushi, Tena wengine wanafanya hayo usiku wa manane na wakiwa na magari kibao.

Hata bila kuwagusa polisi (maana pia najiuliza huwa hawanusu uharifu au ?) Ni siasa gani hizi ambazo,Zina element zote za uharifu?

Kwa Nini kuchana bendera ya mwenzako, mtanzania mwenzako, ambaye chama chake kina fanya kazi zake kisheria?

Hivi kukatokea malipizi (reciprocity) kwa vyama vingine nao kulipiza kisasi , je hatuoni kwamba tutakuwa tunaunda magenge ya kisiasa ya uharifu?

Ushauri wangu, capacity na uwezo ulio ngazi za juu za CCM ushuke huku chini basi Ili tuone siasa safi na za kistaarabu.

Inashangaza vijana wa CCM, kujitwisha jukumu la kutetea chama chao vyovyoye hata kwa gharama ya fujo na kupiga watu wasiowaunga mkono.

Haki ya kupiga wenzao na kuwapora vitu inatoka wapi?

Na najiuliza kwa Nini vyombo vya Dola vinaacha uharifu unaenea kwa jina la kuogopa CCM? Come on ,which country is this where political hooliganism is tolerated?

CCM jingeeni vijana wenu uwezo wa kufanya siasa za masuala, na siyo siasa za nguvu na misuli ambayo itakuja baadae kujenga kisasi kwa wanaoonewa!

Tumejisifu mara nyingi kama nchi ambayo ilipata uhuru wake pasipo kumwaga damu (vita). Kwangu Mimi nashawishika kuamini kwamba hii ni misingi iliyowekwa mapema, yaani siasa za ushawishi na masuala ( politics of persuasion and issues).

Mbona hatujengi Sasa siasa zetu juu ya huo msingi? Why beating other people, in the name of converting them to follow you?

Kwa Nini hatufanyi siasa za hoja?

Nawashauri Tena vijana wa CCM waangalie na kujiepusha na ulevi wa chama chao kuwa madarakani.

Nimesema mara nyingi, "absolute power corrupts absolutely", tusiache nchi hii ambayo Rais wetu ana tu disciple juu ya 4R's. Ielekee mahali pasipo sahihi.

CCM youth wingers, manner up please!
 
Watakuja kupiga hoja yako bunduki weka kambi utaona. Ni watu fulani wenye kuamini kuwa ushindi ni kutumia nguvu yenye ulinzi nyuma yake.
 
Hayo wanayofanya vijana ww ccm Yana baraka zote za chama chao, vyombo vya Dola na serekali, kisha wakishaumiza na kufanyia uhalifu vyama vingine, utasikia viongozi wao wakitoka hadharani na kupotosha huku wakihubiri amani, wakati nyuma ya pazia wanafanya unyama wa wazi. Mbinu hizi wamezicopy iliyokuwa ulaya mashariki ya zamani, ndio wanazitumia hapa.
 
Unaowashauri wawafunze hekima na ustaarabu ndiyo haohao wanaowatuma wafanye fujo na wanawalipa fedha au madaraka.Muulize Queen Sendiga alivyokuwa anafanyiwa fujo wakati wa kampeni za uchaguzi 2020 na hao watu na anawafahamu.
 
In my opinion...

A few years ago, CHADEMA and other political parties made a commitment to the public to do everything in their power to ensure thatbthis country remains Ungoverned.

The environmet, rather, the atmosphere fostered within these political factions was one of negativity and hostility. Now, we see a call for UVCCM to cease actions such as the removal of flyers and Flags.

Isn't it clear that these behaviours are a direct result of the conditions established by the Opposition parties?
 
Are sure this was established by opposition parties?
 
Huwezi amini, kulikuwa na operation ya makusudi kabisa ya vijana wa CCM kuondoa matangazo na hata kushusha na kuondoka na bendera na vipeperushi, Tena wengine wanafanya hayo usiku wa manane na wakiwa na magari kibao.
Magaidi hao. Sio wanasiasa.....ni Hamas na hawashauriki
 
In my opinion...

A few years ago, CHADEMA and other political parties made a commitment to the public to do everything in their power to ensure thatbthis country remains Ungoverned.

The environmet, rather, the atmosphere fostered within these political factions was one of negativity and hostility. Now, we see a call for UVCCM to cease actions such as the removal of flyers and Flags.

Isn't it clear that these behaviours are a direct result of the conditions established by the Opposition parties?
Who are these UVCCM Mr syllogist? Are they constitutional law enforcers to combating of crimes, suppose there is any?
Do the powers you assume to be upon them, enshrined in any of our law books?

Let me keep my reservations, however, the real problem vests in the so called " power arrogance". And as I cited before" absolute power corrupts absolutely".

I kindly beseeech these wingers to manner up and start having the country in their minds and abstain completely from sycophancy.
 
#UVVCCM ni wapiga mapambio na wasio na akili timamu.
Ahsante.
Ccm ipo 5th cycle hawa ndo machawa wanaosubili kama fisi mkono udondoke watie mdomon

4th cycle hii inagusa wilaya angalau ngazi hii wanapata vimaokoto , ila pia ndo ngazi inawatu wanaojificha ndani ya kivuli cha ccm fanya ufisadi, na wizi

3third cycle hii ni sawa na 4th cycle ila kinachoongezeka ni Maokoto na ubunifu mkubwa wa wizi na ufisadi

2nd cycle hapa ndo watu wanaanza tafuna keki ya taifa , hapa kuna madili ya kila aina, ufisadi ,upigaji iko karibu sana na inner cycle , hapa wazee wote waliwhi shika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama utawakuta hapa, mfano Makamba senior n.k

Inner cycle , hawa ndo top , kuanzi mwenyekiti , na mlolongo mzima, hapa kuna kazi ,hakuna alieko hapa ni maskini , ukitaka umaskini ni wewe mwenyewe tu,

MSHANGAO

Unakuta mtu / kijana yupo huko cycle 5,6,.............
Ndo unajifanya anakijua chama , maneno mengi ila daily kusubili elfu 20, kofia ,kanga na t-shert ,

Wengi ndo utawakuta ndani ya mitandao ya kijamii kwa kumwaga sifa za kijinga kwa Mwenyekiti wao ,kuchafua wapinzani , wengine kushindwa kuelewa kwamba mtu yeyote anaweza kufanikiwa vizuri bila hata kua ndani ya ccm, hawa hawana imani kwamba kunamafanikio nje ya ccm, hawana imani kwamba unaweza pata kazi nzuri bila kutokua mwana ccm

MWISHO
Siku sio nyingi Machawa wote watachomwa moto
 
Back
Top Bottom