Leo katika pita pita zangu nikakutana na mdada mmoja mtaani. Huyu dada tumeshawahi kutana mara nyingi, mi najua anafanya kazi gani ila ya alikuwa hajui kazi yangu.
Nikamweleza kuwa nina maongezi naye, akanipa namba yake ili nimtafute jioni. Ilipofika jioni nikamtafuta tukaenda pub moja tukaagiza vinywaji na nyama choma.
Tukiendelea kunywa akaniuliza nafanya kazi gani? Nikamwambia mi muuzaji wa duka la mhindi. Si akaanza kujishaua, oooh... Unajua kuna mtu nataka nimuwahi aliahidi kunipa hela leo..!., na sababu zingine kibao! Aakiwa anaendelea kujishaua kuna jamaa anayenifahamu akatukuta pale.
Katika kunisalimia akataja Dr. Nyalotsi vipi? Kusikia hivyo nikaona mdada kabadirika, akaagiza na kinywaji kingine na kuniuliza, mbona hukunambia kuwa wewe ni dr? Nikamjibu nilitaka nijue kama utavutiwa na mimi kwanza.. Bahati nzuri na simu yangu ikaita kuna jamaa yangu alikuwa zamu, alihitaji nimsaidie.
Lakini bado najiuliza, kukiwa hakuna uhakika wa hela hupendwi? Ina maana ni money for service? Duh, kazi tunayo..!