Nilikosa amani yote kwa kusumbuliwa na wachawi, nilikuwa nalala alfajiri huku nanunua betri ya tochi kila siku, nilihama nyumba

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Hawa wanga mbaki kuwasikiaga tu na kama huamini hawa watu wapo basi ni dhahiri wewe si mkristo wala muislamu maana haya mambo yapo kwenye vitabu vyote, na hata kwa mila zetu waafrika hawa wanajulikana kwa kuwa miiba katika maisha ya watu enzi na enzi,

Ni mwaka 2014 ndio kwa mara ya kwanza maishani mwangu nawajua wanga, ilikuwa ni Arusha nimepanga chumba pande za Lemara mitaa ile karibu na mabwawa ya maji taka, ni zile nyumba zilizopo karibu na reli, sikuwahi kabisa kudhania kwamba wachawi wapo A-town, nilihofia vibaka ila suala la uchawi sikuwahi hata kulifikiria,

Basi siku ya siku wakati nikiwa naingia kulala ile navuta usingizi nasikia nyuma ya ukuta kuna kitu kama nondo inakwaruza ukuta kwa nguvu sana, Dah! nikadhani ni wahuni wa Kijenge wamekuja kusaka riziki wanataka kuingia kwa kutoboa ukuta, nilichukua silaha yangu bomba la chuma nikasema ataeingia kupenyeza bichwa au mkono namtia adabu, ghafla nikasikia kicheko cha kike heee heehehe juu ta dali, wazeee!! nilipatwa na wazimu, pakatulia na sikuweza kulala hadi saa 12 asubuhi,, kesho yake naenda kucheki nyuma ya ukuta nakuta hakuna chochote wala hakuna mchubuo hata wa wembe kwenye rangi ya ukuta, nilienda chumbani nikajilaza chali kitandani naiangalia silingi bodi kwa takribani saa zima nawaza hivi inawezekanaje, ndipo hapo nikaona nachezewa, ni rasmi sasa nilianza kuwa naweweseka nisie na amani, nilienda mjini kununua tochi inayotumia zile betri kubwa na kila siku ilikuwa lazima 500 initoke ya battery, niliogopa kulala gizani hasa ukizimgatia nao Tanesco hawatabiriki.

Usiku unaofata niliacha tochi inawaka huku nimezima taa, saa saba ukuta ukaanza kusagwa tena, tena na tena hadi saa nane, ilikuwa ninaishi chumba cha mwisho kabisa nikamstua jamaa wa chumba cha pili nae anasema kweli kuna kitu kinaendelea, na mpangaji mwengine wa chumba cha tatu alikuwa ni binti nikamwambia vipi huko nae hivyo hivyo, sema muda huu kidogo tuliweza kugawana hofu ikawna nafuu maana nilidhani ni mimi tu.

Another day nahisi baada ya siku 5 huku nikiendelea na utaratibu wa kulala na tochi tena hio siku Tanesco wamekata umeme, basi mida ya saa nane imefika ni kama mchanga unamwagwa kwenye bati kwa dakika 3 mfululizo, nilitoka nje mimi na tochi langu kumurika huko kwenye bati lakini hamna kitu, nilihisi kuchanganyikiwa, wale wengine nilishawakita nje wametoka, tulikaa hapo nje kama saa hivi kila mtu akarudi kwake, ile tunarudi kuna vicheko vya kebehi vilidumu kwa dakika hivi vinapause na kuplay haraka harala, mimi huku nikiwa na uoga ulioambatana na hasira nilijikuta natoa tusi nahisi kila mtu alisikia. nikajikaza ivo ivo kujaribu kuonyesha siogopi japo kiukweli moyo ulikuwa unadunda sana na jasho.

Yule binti kesho yake alimleta mwenzake wawe wanalala wote hapo, itakuwa ni rafiki yake alimweleza hivyo ili kupunguza uoga wa kulala peke yake.

Palikuwa kimya wiki hivi na niliacha kutumia tochi mi nikaona tochi ni kupoteza pesa ntalala kama kawaida japo nilikuwa naogopa ila kadri siku zinaenda nazoea zoea kibishi,

Jumamosi flan imefika hio, saa saba wakalianzisha, hivi sijui ni watu au ngombe zilikuwa zinakimbia huko darini, yani ni ile unahisi vishindo kabisa, nilisikia wengine milango wanafungua wanatoka nje mimi nilibaki ndani humo na wala sikuamka ila moyo unapiga sana , uvumilivu ulinishinda nikawatolea tusi "ku*an*a zenu hamnitishi kitu, wa*enge nyinyi hamnitishi, malizeni mrudi kufi**na na mafisi) ila kamoyo kadunda hapo acha tu.

Kesho yake nikaingia kulala naona wengine saa 8 wanantumia mesej vipi huko, najaribu kusikia kwa karibu naona hakuna kitu, nikaona hawa washanifanya kiziwi, basi nikapiga mziki kwenye simu pale nasikia, mimi nikawajibu huku kimya, asubuhi ndo wananiambia jana walikuwa wanakwangua ukuta,

Baada ya wiki hivi tena niliambiwa wamerudia kukwangua ukuta, ehhh sasa mbona mimi nilikuwa sisikii! nikaona hawa watu wabaya sasa huenda watakuwa wanaingia kimya kimya chumbani kwangu, niliogopa sana.

Nilihama hio nyumba siku hio hio kuelekea Njiro huko Container jamaa yangu dalali nilimtafuta aliniambia kuna mwanafunzi anauza chumba imebaki miezi mitatu nimfidie kwa bei ya discount, nililala gesti usiku huo, kesho yake yule mwanafunzi alipohamisha vitu ndio nikarudi kuchukua vitu vyote na kirikuu nikahama moja kwa moja.

wakati mikiki miki hiyo ikiendelea wenzangu walikuwa washaanza kujiongeza kuweka visu kwenye ndoo ya maji lakini wapi, kuchoma zile nyanya pori ndulele sindano wanaweka kwa kona lakini wapi, walilala hadi na mifupa ya nguruwe lakini wapi. naskia watu wa mtaani hapo walililatua ila sijui ilikuwa kwa namna ipi.

Ushauri

1.uchawi uko kila mkoa, tusikariri kwamba ni mikoa flani tu.

2. Kama kauwezo kapo epuka kukaa uswahilini. hapo nilipoishi kimtindo ni uswahilin.

3. Sali kavla ya kulala, enzi hizo nilikuwa nalala kama ng'ombe, nilikuwa sisali kabisaaa!!
 
Unawaambia Nini wakishua watoto wa daslam

Wanaosema uchawi haupo
1684320116854.jpg
 
Unawaambia Nini wakishua watoto wa daslam

Wanaosema uchawi haupoView attachment 2631750
uchawi hauonekani kirahisi kama kwenye muvi zinazotungwa na ma director ambao wanatengeneza picha tunayoiona kwenye muvi inayotokana na mawazo yao na kuaminisha wengine wauone kwa jinsi wanavyofikiri.

Kiuhalisia ni tofauti kabisa, watu wengi wamekariri wachawi wanapaa na ufagio sababu wameona kwenye muvi za harry potter ila yote yale yalikuwa mawazo ya mtu moja director,
 
Mkuu nafikiri hayo yanakuwa ni maroho machafu, nina experience hiyo nilivyokuwa naishi bado kwa wazazi tukiwa tumepanga nyumba moja hivi, hivyo hivyo unavyoeleza na mimi nilikuwa napata hofu sana.

Kuna siku nililala gesti moja mtwara mjini nikasikia kwa nje kama kelele za mtu anakunja makaratasi, kuchungulia dirishani hakuna kitu. Nafikiri haya mambo yapo sana uswahilini na huenda yanakuwa ni majini au kitu kama hicho.

Ukijitia ujasiri katika Mungu Mkuu hayawezi kukutia hofu na labda kufanya maombi ya kuondoa hali hiyo.
 
Mkuu nafikiri hayo yanakuwa ni maroho machafu, nina experience hiyo nilivyokuwa naishi bado kwa wazazi tukiwa tumepanga nyumba moja hivi, hivyo hivyo unavyoeleza na mimi nilikuwa napata hofu sana. Kuna siku nililala gesti moja mtwara mjini nikasikia kwa nje kama kelele za mtu anakunja makaratasi, kuchungulia dirishani hakuna kitu. Nafikiri haya mambo yapo sana uswahilini na huenda yanakuwa ni majini au kitu kama hicho.

Ukijitia ujasiri katika Mungu Mkuu hayawezi kukutia hofu na labda kufanya maombi ya kuondoa hali hiyo.
Ni kweli, huko nilikoenda kupanga kulikuwa uswahilini kimtindo. kamtaa kamejaa wameru na warangi.

Sema mtihani huwa ni siku ya kwanza, yani saikolojia inaharibika kabisa utapanic na kuweweseka sana na hata usingizi utakata kabisa.

Ila nilichojifunza kadri siku zinaenda kama una ujasiri utazoea tu, mimi kwa sasa hali hii hata ije kujirudia siwezi kupaniki, nadhani na hawa wakulungwa lengo lao huwa ni kukuwewesesha, ukikaza moyo ukiwa huna mda nao lengo lao la kukutisha linafeli wanaona ni kupoteza muda tu kuja kwako,

Ila kuomba nako muhimu sana sambamba na kufanya maamuzi mazuri sehemu za kuishi kama kauwezo kapo hama uswahilini.
 
Ukienda sehemu zingine ambazo unahisi kuna mambo ya uchawi wewe tafuta mafuta original ya mzeituni usiku paka utanishukuru baadae.. hayo mafuta ni anti-witchcraft
 
Uchawi upo.. kama hayo mambo ya kumwaga mchanga juu ya bati yapo kila mkoa. Kuna mikoa unasikia vishindo watu wanakimbia wanazunguka nyumba, nyingine kishindo katikati ya nyumba halaf unafuatiwa na ukimya usio wa kawaida, nyingine vicheko.

Nyingine unasikia mtu anatembea mpaka kitandani mwako halaf kimya.. nyingine unanyolewa live na asubuhi unakuta huna nywele, nyingine wanakunya..

Nyingine unalala umeoga vizuri, lakin asubuhi unajikuta una udongo wa shambani au tope..mambo ya kisengerema mengi tu
 
yanaproduce positive energy kwenye mwili na kupambana na negative energies zote za kiroho.. niligundua nilipokuwa na misafara na watumishi mbalimbali wa Mungu wale wanaoenda kuhubiri injili vijijini wengi huyatumia haya NB: Nunua yale original achana na yale ya mwamposa.
 
yanaproduce positive energy kwenye mwili na kupambana na negative energies zote za kiroho.. niligundua nilipokuwa na misafara na watumishi mbalimbali wa Mungu wale wanaoenda kuhubiri injili vijijini wengi huyatumia haya NB: Nunua yale original achana na yale ya mwamposa.

Yani nayanunua bila kuweka chchte na kuanza kuyapaka.

Ina maana hayo mafuta nkipaka usiku mchawi hanigusi
 
Yani nayanunua bila kuweka chchte na kuanza kuyapaka.

Ina maana hayo mafuta nkipaka usiku mchawi hanigusi
Huweki kitu chochote unapaka kama yalivyo niliwahi kuyatumia tulienda kijiji kimoja mpakani mwa Mtwara msumbiji kuhubiri injili tuliambiwa hicho kijiji ni nyoko sana kwenye uchawi ila tulifika tukafanya huduma tukasepa bila kudhurika. ila nimeulizia bei za hayo mafuta original ni gharama sana kudadeki kuanzia 75K na kuendelea ila yana nguvu ya ajabu sana.
 
Back
Top Bottom