Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,554
9,531
Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana
 
Niliisha shuhudia enzi za jiwe, mwenye nyumba alikuwa akitamka, kwamba kama yeye ana miliki nyumba na maisha anayaona magumu, je mpangaji wake??
Akawaambia wapangaj, wale anaowadai watamlipa watakapopata kodi yake kwa sasa watafute na maisha yaendelee, haimaaish wakae bure ila aliwaondolea presha ya kodi
 
Mkuu au alikuwa anakuhisi kuwa ni kibaka flani?Yani Kodi Nampa na visabuni vya rushwa anapata halafu aniletee hizo?Mm nisingemsumbua hata mke wangu ningemgongea dirisha lake afungue yeye la sivyo anipe funguo yangu ya geti.Yani Nimekasirika utadhani hii sio chai
 
Back
Top Bottom