Westchester college haipo USA, ila ipo Westchester county college au huitwa community college ambavyo hutoa wahitimu wa certificate na associate degree elimu ambayo kwa tanzania unaweza kulinganisha na deploma au certificate. Westchest ni county iliyoko kaskazini ya jiji la NY, ni kupandisha kidogo tu toka vile vitongoji vya vijana wa born city waanzilishi wa miondoka ya Ragge aka wana Bron..... Mara kadhaa umeonyesha kwenye CV yako kwamba ulisoma community college iliyoko westchester ni nje kidogo tu ya jiji la NY ambako kulikuwa na nyumba ya balozi wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa nadhani wameitelekeza siku hizi na kununua nyingine. Hivi vyuo vingine vimemea kwa ajili ya kugombea nafasi chamani?
Hivi vyuo vingine vya Marekani naone vimeongezeka safari hii ulipoandaa CV ya kugombea nafasi chama cha mapinduzi. Inaweza kutia shaka kidogo na degree ulizoanika hapa kwenye CV yako wakati awali hukuweka kitu kama hicho kwenye CV yako. Kwangu mimi CV haina maana kwa mtu iwepo uwezo wake hana. Cha msingi uwezo ndio chanda cha dhahabu, kwani wengi wana elimu lakini wameishia kuhangaika kama mimi huku wakikodolea utitiri wa vyeti vyao vya uhitimu walivyovitundika majumbani na kuwa kama magazeti ya kuziba nyufa ukutani (to paper the cracks).