Nini simu? Mimi nishavunjiwa TV inchi 52, laptop, kabati la vyombo na vyombo vyake, sofa lether zilichanwa chanwa na wembe, sigth mirrors, nguo na viatu kuchomwa Moto na hasala luluki. Kisa mchumba alikuta alikuta kitenge magetoni. Akapaniki Sana. Nilikuwa nimetoka kidogo kumsindikiza sister alikuja kunitembelea ila yeye sikumwambia. Kurudi nikakuta geto limekuwa torabora. Kumuuliza ananijia juu na kunikwida na kuanza kulalamika nimefikia hatua ya kuingizwa made zangu ndani. Kisa kitenge.
Nikamwambia subiri. Nikampigia sista akarudi maana hakufika mbali. Nikamwambia umesahau kitenge chako na ndio kimeleta dhahma yote hii. Akapigwa butwaa. Nilichofanya nikamwambia yule mchumba ingia kwenye ndinga tukaongee. Nikaenda nae mpka kwao nikamshusha na kumwambia asinitafute Tena. Hakukubali ila baada ya miezi kadhaa akakubali matokeo.