Nilichokula ni nini (Fumbo)

umetaja neno kula,si neno la masihala,
bali lina makabila,na viko vingi vyakula,
watoto wasivyokula, kwa masharti ya mila,
wakubwa wanachokula,hicho ndicho umekila.

ukipanda daladala,kuenda mwananyamala
utamuona hawala,mpenzi wa Abdalla,
atakiri Abdala,huyo amekwisha mla,
utamu pasi badala,japo mtu si chakula.

yamkini yako kula,ni sawa na Abdala,
wala kwa kugalagala,kama muwa wa mbagala,
chapa ntu umekula,tena ni pale mahala,
wakubwa wanapopala,ndipo wapate kulala.
 
jamani asanteni sana wote mliotunga utenzi,
kwa kweli mmenichanganya, hii ni fani wanaoiweza wachache, mfano wa vijana ni kina Juma Nature,
Nifanyeje nianze na mimi?
 
Mwanakijiji acha utani
Kwa staili unayoghani
Ulichokula mdomoni
Hukifahamu moyoni?
Au ulikula ndotoni
Uliyoota Ukweni?

Mi sitaki uliza sana
Wala sitaki elewa upana
Umeongea ya maana
Ajuaye maulana
Wazee na vijana
Tumepemnda ulivochana
Na asiejua maana
Usimwambie maana

Kula vilivo vema
Vibaya mpe neema
Vikiwa vichungu tema
Au mtupie rehema

Kuna wapendao vya kuchechema
Ila vikiwa vichungu watema
Watakula hata ya BIMA
mwsho watuacha twahema
 
natamani wangetia timu hapa ebbynature, xpasta na mgombea ubunge, nawaapia pasingekalika hapa!

hongera wote mlio mabingwa wa mistari................
 
Hivi Mwanakijiji hicho chakula ulikula au uliliwa?

Sharti nijuavyo, kula ni kwa kinywa
na wewe usemavyo, ni kama umeliwa
na ili iwe ndivyo, ujuwe umeliwa
Maana halisi ya kula, ni kwa kupitia kinywa

Mwaweza kustaajabu, ni vipi ninafikiri
Lakini si maajabu, hivyo mimi nakiri
Nyie mlio jaribu, nadhani mwaweza kiri
Maana halisi ya kula, ni kwa kupitia kinywa

Wasema kilikuwa moto, mkono hukuungua
tena si cha kitoto, wakubwa hukigunia
hapo uliota ndoto, eti hutaki changia
Maana halisi ya kula, ni kwa kupitia kinywa

Mi naona uliliwa, maana we uliingia
Aliyefaidi kajaliwa, kimya kajitulizia
Wewe ulie onjeshwa, tungo ukakitungia
Maana halisi ya kula, ni kwa kupitia kinywa
 
Nduguzo twafa na njaa, wewe kicheko cha haja
Wenzako tuna balaa, wewe ndugu unafuja
Sisi twapata vichaa, wewe wala kwa mrija,
Mla jana kala nini, kula mla mla leo

Kula mla mla leo, mla jana kala nini
Ukila hupati cheo, huwezi tamba mjini
Mlaji hunywa vileo, hufaidi mtimani
Endelea kutafuna, ukishiba tugawie

Ukishiba tugawie, na sisi tufurahie
Uje utupe na sie, tutafune tujilie
Chakula tukisifie, tule kama siesie
Unapopata kizuri, kula na sisi nduguzo

Kula na sisi nduguzo, tupige vigelegele
Hata kama ni uozo, uliosazwa na wale
Tutakula kwa gumzo, kijijini tutawale
Hakina ugwadu chacho, unapowapa wenzio


Unapowapa wenzio, Baraka huja kwa shere
Tajifunga mitandio, tule tushibe tuhare
Atapokuja bandio, akute tumekisare
Ukitunyima tunyime, hatutachoka kuomba

Hatutachoka kuomba, nasisi tukisugue
Tukile hadi kulamba, hamu hadi itutue
Sasa twapiga jalamba, twaruka kama ngurue
Hamu haiwezi kwisha, hadi na sisi tuguse

Hadi na sisi tuguse, msosi tushikeshike
Ukitunyima tususe, kaya iparaganyike
Sisi ndugu wa manzese, mtaa wa mbuzi jike
Kama chakula kichache, usingepiga mirimo

Usingepiga mirimo, tusingetoka udenda
Hata sisi nao tumo, tunataka hiyo tenda
Tukila tucheze sumo, mchezo tunaopenda
Wewe ni ndugu wa damu, ulacho sisi halali

Kaditama wa tamati, nimefika kiringeni
Tena nimevua shati, ninasubiri resheni
Ndugu nimejidhatiti, nikimege magegoni
Nataka msosi huo, nipe nami nifaidi.





 
Chakula nilichokula, nakisifia kitamu!
Nimekula bila hila, kimeniondoa hamu,
Cha jirani sitokula, changu chanitosha hamu,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Sikukipika kwa moto, kwani kimekwisha wiva,
Ndani kina jotojoto, chakula hicho si mbeva,
Si chakula cha watoto, si chakula cha mandava,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilijihisi nayeya, pale nikikirarua,
Pale nilipochoveya, kwenye mchuzi murua,
Nilihisi napepeya, utamu kunizingua,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilichokula si kuku, si ng’ombe wala si bata,
Msijeanza kushuku, majina mkaniita,
Wakijiji kala chuku, ametiliwa limbwata,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilichokula si embe, fenesi au nanasi,
Sio ugali wa sembe, au samaki mkisi,
Si tambi wala si pombe, msidhani nawatusi,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nimekula kwa kuguna, nikala kikimya kimya,
N’kang’ata n’katafuna, na pia nikamung’unya,
Mwenzenu nikajichana, miye ninawatambiya,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Chini nikabingirika, utamu kuninogeya,
Na jasho likanitoka, huku nikichekeleya,
Pumzi ikinitoka, kama ninaogeleya,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Sikitaki cha jirani, cha kwangu chatosheleza,
Kinanitosha shambani, na hata Uingereza,
Hata huko Marekani, changu tumbo chanijaza,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nawauliza wenzangu, na wapishi majikoni,
Mmekula kama changu, chakula hiki ni nini,
Nawauliza Marangu, Kitete na Turiani,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Beti miye nazifunga, miye naondoka humu,
Meza yangu naipanga, nile chakula kitamu,
Komeo nimelifunga, sitaki katishwa hamu,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?
Ulichokula si pono,wala Nguruwe mnono
hata kama una mshono,utakula kwa jivuno
ukikipapasa kwa mkono,utakula kwa wiano
Ulichokula kitamu,wallahi chanipa hamu
 
Chakula nilichokula, nakisifia kitamu!
Nimekula bila hila, kimeniondoa hamu,
Cha jirani sitokula, changu chanitosha hamu,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Sikukipika kwa moto, kwani kimekwisha wiva,
Ndani kina jotojoto, chakula hicho si mbeva,
Si chakula cha watoto, si chakula cha mandava,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilijihisi nayeya, pale nikikirarua,
Pale nilipochoveya, kwenye mchuzi murua,
Nilihisi napepeya, utamu kunizingua,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilichokula si kuku, si ng’ombe wala si bata,
Msijeanza kushuku, majina mkaniita,
Wakijiji kala chuku, ametiliwa limbwata,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nilichokula si embe, fenesi au nanasi,
Sio ugali wa sembe, au samaki mkisi,
Si tambi wala si pombe, msidhani nawatusi,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nimekula kwa kuguna, nikala kikimya kimya,
N’kang’ata n’katafuna, na pia nikamung’unya,
Mwenzenu nikajichana, miye ninawatambiya,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Chini nikabingirika, utamu kuninogeya,
Na jasho likanitoka, huku nikichekeleya,
Pumzi ikinitoka, kama ninaogeleya,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Sikitaki cha jirani, cha kwangu chatosheleza,
Kinanitosha shambani, na hata Uingereza,
Hata huko Marekani, changu tumbo chanijaza,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Nawauliza wenzangu, na wapishi majikoni,
Mmekula kama changu, chakula hiki ni nini,
Nawauliza Marangu, Kitete na Turiani,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?

Beti miye nazifunga, miye naondoka humu,
Meza yangu naipanga, nile chakula kitamu,
Komeo nimelifunga, sitaki katishwa hamu,
Nilichokula kitamu, nilichokula nini?


ulichokula umwazi, ndio maana hunyamazi,
tena sema kwakificho, wasisikie paparazi,
utamu hauna kificho, wanaojua wazazi,
ulichokula ndicho, hicho chaitwa umwazi.
 
wakijiji twaomba rudi, utupe tena uhondo
jukwaa lawa baridi, twakosa zako ndondondo
chakula sile zaidi, ukapasuka utumbo
chakula unachokula, kisituletee karaha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom