Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,765
Reaction score
86,447
Niaje wadau?

Hili tukio nililishuhudia kwa macho yangu wala sio stori..

Ilikuwa ni jijini mwanza mwaka 2006 tukiwa kwenye gari tunatoka kwenye harusi usiku kama saa nane hivi ama saa tisa usiku.

Tulitoka harusini salama salimini safari ilikuwa ndefu kidogo lkn tulipokaribia kufika gari tuliokuwa tumepanda iliishiwa mafuta!

Dereva akaipaki gari pembeni mtu mmoja akashuka kukimbilia petroli ilikuwa ni maeneo ya ghana kwa wakazi wa mwanza nadhani mnapapata.

Wakati tukisubiri petroli huku wengine wakiwa wameshuka wakibalizi ghafla tuliona mwanga wa kijani umetanda pote!

Kucheki juu niliona kitu hicho kikitoa mwanga huo huku kikienda juu kwa kasi na mwanga huo ulidumu kwa sekunde kama sita hivi na kile kilichotoa mwanga huo kilipotelea angani!

Kusema kweli mapigo ya moyo yalinienda mbiombio..Watu walisema ni satelite lkn hawakuwa na uhakika.

Kutokana na utoto nliokuwa nao sikuhoji sana lkn sasa nimelifikiria tukio lile nimekosa majibu pia nimejaribu ku google ni satelite gani ilirushwa mwaka huo but no..

Kama ni satelite ni lini Afrika ama tanzania tumeirusha huko angani mwaka 2006...? but nothing!

Wadau kama kuna alieshuhudia tukio lile na anajua ni nini kile kilichotokea anijuze maana kichwa kinanikeleketa kutaka kujua ni nini kile..?

Hata leo nimekuwa nikiwauliza na kuwakumbusha tuliokuwa nao siku ile lkn jibu walitoa ni satelite! Hivi satelite ikiwa inarushwa ndo hutokea vile..?

Na tatizo jengine nililoliona hapa ni kuwa sisi waafrika sio wafuatiliaji wa mambo kiundani.. (But not all).

Wadau ni hivyo tu kama kuna anaejua anijuze and that is all...!

Karibuni
 
Muendelezo kidogo...

Kama ni satelite ni lini Afrika ama tanzania tumeirusha huko angani mwaka 2006...? but nothing!
wadau kama kuna alieshuhudia tukio lile na anajua ni nini kile kilichotokea anijuze maana kichwa kinanikeleketa kutaka kujua ni nini kile..?
Hata leo nimekuwa nikiwauliza na kuwakumbusha tuliokuwa nao siku ile lkn jibu walitoa ni satelite!
Hivi satelite ikiwa inarushwa ndo hutokea vile..?
Na tatizo jengine nililoliona hapa ni kuwa sisi waafrika sio wafuatiliaji wa mambo kiundani.. (But not all).

Wadau ni hivyo tu kama kuna anaejua anijuze and that is all...!
Karibuni
 
Watanzania wengi wako kama hao ndugu zako
yaani kitu hawakijui lakini wanakipasisha kuwa ni kitu fulani baasi
hawataki hata kujisumbua tena kujiuliza

ndo maana Africa iko hivi ya mwisho duniani

Haiwezi kuwa Satelite labda ni UFO na UFO maana yake ni 'unidentified flying objects'

labda wadau wengine watakusaidia Kiranga Nyani Ngabu
 
Nimejikuta nashauku sana ya kujua ni nini kile nilichokiona lkn dah! inaonekana kama kunaugumu coz ya teknolojia yetu...
 
Naomba unayetaka kumjibu jiulize, kwa nini kama hao wenye arusi walijua wangeenda mbali hivyo, mbona hawakuweka mafuta ya kutosha?
Kama ni vipi, kwa nini mwanga huu utokee ghafla na kupotea?
Nadhani, kuisha mafuta ilikuwa ndio The only chance ya ujumbe flan kufikishwa kwa walengwa. Kuna kaujumbe hapo
 
Nimejikuta nashauku sana ya kujua ni nini kile nilichokiona lkn dah! inaonekana kama kunaugumu coz ya teknolojia yetu...

Sasa itakuwa vigumu sisi kutambua maana hatukuona
1. Kilikuwa na ukubwa gani
2. Kilikuwa na mlio/mshindo gani
3.kilitokea mlipokuwa au kilipitia hapo na kilienda vertically upward au horizontally
 
kuhusu ukubwa ni ngumu kudetermine coz kilikuwa juu sana hivyo kwa chini yake ndo ilionekana mwanga ule wa kijani.
kuhusu mlio ulikuwa wa kawaida tu sema tuliogopa coz ilikuwa ni ghafla na kilikuwa kinaenda juu ndo kikapotele.
 
Itakuwa ni risasi maana uck inatoa mwanga na watu wengi hupiga wakielekeza mtutu juu kuogopa madhara
 
Niaje wadau?

Hili tukio nililishuhudia kwa macho yangu wala sio stori..

Ilikuwa ni jijini mwanza mwaka 2006 tukiwa kwenye gari tunatoka kwenye harusi usiku kama saa nane hivi ama saa tisa usiku.

Tulitoka harusini salama salimini safari ilikuwa ndefu kidogo lkn tulipokaribia kufika gari tuliokuwa tumepanda iliishiwa mafuta!

Dereva akaipaki gari pembeni mtu mmoja akashuka kukimbilia petroli ilikuwa ni maeneo ya ghana kwa wakazi wa mwanza nadhani mnapapata.

Wakati tukisubiri petroli huku wengine wakiwa wameshuka wakibalizi ghafla tuliona mwanga wa kijani umetanda pote!

Kucheki juu niliona kitu hicho kikitoa mwanga huo huku kikienda juu kwa kasi na mwanga huo ulidumu kwa sekunde kama sita hivi na kile kilichotoa mwanga huo kilipotelea angani!

Kusema kweli mapigo ya moyo yalinienda mbiombio..Watu walisema ni satelite lkn hawakuwa na uhakika.

Kutokana na utoto nliokuwa nao sikuhoji sana lkn sasa nimelifikiria tukio lile nimekosa majibu pia nimejaribu ku google ni satelite gani ilirushwa mwaka huo but no..

Kama ni satelite ni lini Afrika ama tanzania tumeirusha huko angani mwaka 2006...? but nothing!

Wadau kama kuna alieshuhudia tukio lile na anajua ni nini kile kilichotokea anijuze maana kichwa kinanikeleketa kutaka kujua ni nini kile..?

Hata leo nimekuwa nikiwauliza na kuwakumbusha tuliokuwa nao siku ile lkn jibu walitoa ni satelite! Hivi satelite ikiwa inarushwa ndo hutokea vile..?

Na tatizo jengine nililoliona hapa ni kuwa sisi waafrika sio wafuatiliaji wa mambo kiundani.. (But not all).

Wadau ni hivyo tu kama kuna anaejua anijuze and that is all...!

Karibuni
hao wachawi walikuwa wanaenda kusikiliza siri za mungu
 
Umesema ulikuwa mdogo,... Kuna uwezekano ulikuwa umelala kwa uchovu wa harusi, na hAyo uliyoyaona ni ndoto...achana nayo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom