Niliahidi kuja Tz...mh! nilioyaona!

Mazee ina maana muda wote hujui matatizo ya umeme bongo? Au ndiyo nyie type za kukaa miaka miwili Albania huko tayari unasema "Nimesahau Kiswahili" ?
Jamani members mbona hamuamini? Napenda swahili pia. Tatizo hamuamin mtu akizungumza kiswahili...!Nipo Canada .
 
Si ajabu na mbwembwe zote hizi unatokea Zaire au Sudani, anyway au pakistan lakini unataka kila mtu ajue kuwa umepanda ndege haya syco tumejua tayari
Utakua dogo tu! Age hizi hamna logic hata kidogo. Umeona kuparamia ndege ujiko?Acheni utoto...mimi naishi huku ninayo familia pia ndugu zangu twaishi huku. We vipi yakhe!!!
 
Waacheni wabwate, wengine safari ndio wanaanza na walikuwa hawana ndoto hata za kutoka kijijini kwao. Kwa hiyo hata the basics of netiquette na decorum hawajui.Unasoma thread unaona kabisa huyu mtu katoka chini ya jiwe. Wewe unasafiri unaenda mpaka bongo ndiyo unajua kuna tatizo la umeme? Huna utashi au internet?Au ndiyo kutukoga tu siye wengine kina Kakamiye?
Kiranga! Pole mwanaJF!Umeumia sana moyo wako. Hili kwangu ni jambo jepesi ila bado hujakua na hujayapata.Utafahamu ni jambo la kawaida.Mungu akusaidie unifahamu .Maana wabongo mambo yenu yanafanana sijui ajili gani?
 
​............................Maendeleo ya kweli huletwa na wazalendo wa nchi.
 
Heri ninyi mlio bahatika kuzikimbia shida na matatizo ya Tanzania. Ukweli hali ya nchi si nzuri hata kidogo..
Lakini naamini hukosi walau binamu aliobaki kama si watanzania wenzenu ambao nao pia hawazipendi shida kama ninyi..

Mkumbuke kwamba Tanzania haiwezi kujengwa na CCM, CHADEMA au CUF bali watanzania wenyewe. Diaspora mnayo nafasi kubwa ya kutukomboa kupitia yale mliyojifunza huko mliko.

Sina wivu na maisha yeny na siwalaumu kwa mliyoyachagua bali nawashawishi muache kutucheka, na mtumie uwezo wenu wa kitaaluma au kifedha kuwekeza nyumbani. Matatizo ya nchi yetu si ya kufanyia mzaha na ole kwa anayefanya hivyo.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Great Thinker Amechangia!! wabongo wengi wana wivu na wenzao walioko mbele ... hahaha!
 
Preta !Matatizo nimeyataja...nilikua naja kwa matayarisho ya kuanzisha uzalishaji. Nimerejea labda watakuja wenzangu mara nyingine.Nimewakilisha ahadi nilio ahadi humu kwa wana JF.

Kweli una matatizo sana.Ulitaka kuanza kuzalisha nini? Binadamu, wanyama au nini?
Hueleweki na ndio maana hukuweza kuelewa hata maelekezo kidogo uliyopatiwa na hao washkaji wako.Ina maana hata ku tune redio ulishindwa? Magazeti ulikuwa husomi online kwani?
Au lengo lako ni kutaka tujue uko majuu??..ACHA MISIFA YA KIJINGA WEWE!
 
Kweli una matatizo sana.Ulitaka kuanza kuzalisha nini? Binadamu, wanyama au nini?Hueleweki na ndio maana hukuweza kuelewa hata maelekezo kidogo uliyopatiwa na hao washkaji wako.Ina maana hata ku tune redio ulishindwa? Magazeti ulikuwa husomi online kwani?Au lengo lako ni kutaka tujue uko majuu??..ACHA MISIFA YA KIJINGA WEWE!
hilo lijamaa haliko nje wala nini,si ajabu ukakuta liko hukoo mererani linafanya kazi ya ulinzi..
 
Members JF!
Habari.
Nashukuru niliomba maelekezo ya kujua magazeti ya kusoma pia stations za kupata habari.
Ila nilishindwa hata kuitumia phone yangu so nimeshindwa kuwasiliana kipindi nlichokuepo huko Bongo.
Ni kwetu kuna jamaa zangu wengi lakini si vibaya kusema''nawashukuru'' kwa yote mlionielekeza lakini nilikaa huko siku 3 nkarejea na maswali mengi.
1-Nimekuja muda si muafaka?
2-Matatizo kama ndio hayo uhakika wa maendeleo itakuaje? Maana umeme wa uhakika shida na vitu vingi vinahitaji umeme ...bara bara jams ,maji hakuna uhakika ...
Nimesikitika zaidi nilipanga kuonana na members ana kwa ana.
Nilikua muoga maana sikuwa na bodyguard.
Ahsanteni.
Ndevu mbovu;
To some extent, nimejifunza namna unavyopata shida ku-cope na maisha uliyokuwa nayo ambayo uliyaacha hapa kwenu Tanzania,... yes, unaenda na wakati,...mabadiliko.
Kwa upande mwingine nimejifunza ni namna gani ulivyo comfortable na hii situation ya shida zilizokushinda wewe hapa, kwa wengine ambao wanaendele nazo mpaka mda huu "
vinahitaji umeme ...bara bara jams ,maji hakuna uhakika ..."
. As such siyo kwmba unalalmikia maendeleya nchi kuwa unaguswa na hali iliyopo, ila unatamba na kuifurahia kimoyomoyo kwa wale tunaoendelea kui-face. Hata hivyo tungeliweza kukuonea huruma sana kama tungegundua kuwa huko uliko pengine unabeba maboksi, ni mkata nyasi au ni loiterer ambaye ukiambiwa f**k* you inabidi useme ahsante, la unaweza ukapigwa risasi. ".........................HAKUNA UMASKINI MKUBWA DUNINAI KAMA UMASIKINI WA MAWAZO,.. J.K. NYERERE
 
Members JF!
Habari.
Nashukuru niliomba maelekezo ya kujua magazeti ya kusoma pia stations za kupata habari.
Ila nilishindwa hata kuitumia phone yangu so nimeshindwa kuwasiliana kipindi nlichokuepo huko Bongo.
Ni kwetu kuna jamaa zangu wengi lakini si vibaya kusema''nawashukuru'' kwa yote mlionielekeza lakini nilikaa huko siku 3 nkarejea na maswali mengi.
1-Nimekuja muda si muafaka?
2-Matatizo kama ndio hayo uhakika wa maendeleo itakuaje? Maana umeme wa uhakika shida na vitu vingi vinahitaji umeme ...bara bara jams ,maji hakuna uhakika ...
Nimesikitika zaidi nilipanga kuonana na members ana kwa ana.
Nilikua muoga maana sikuwa na bodyguard.
Ahsanteni.

wewe ni mzaliwa wa wapi
 
DUh Hizi ni type za kina Jack pemba. Analinganisha matatizo anayoyaona masaki na yale ya canada. Sasa sijui ungefika alikozaliwa babu yake( Hope hakuzaliwa aghakhan) Ungeandika nini.

But mungu hakunyimi yote mkuu wengine huku kigoma tunafariika badala ya kuamshwa na alarm ya simu na saa ni sauti za ndege wa asubuhi ndo alarm yetu. umeme kwetu ni favour na maisha yanakwenda na kuna wanacada wengi wanakuja huku Ulizia hifadhi ya Gombe. kujifunza maisha ya kigumu na wanafurahia.
 
Ndevu Mbili yupo sawa kw kiasi flani. Bongo maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha, ishu ya umeme na maji ni cha mtoto. Usiombe uuguliwe halafu umechacha, hospitali za serikali hazina dawa wala vipimo hivyo watu inabidi tukimbilie kwa babu Samunge ndio tumaini lililo bakia.

Maisha haya hadi lini?
 
Kweli una matatizo sana.Ulitaka kuanza kuzalisha nini? Binadamu, wanyama au nini?Hueleweki na ndio maana hukuweza kuelewa hata maelekezo kidogo uliyopatiwa na hao washkaji wako.Ina maana hata ku tune redio ulishindwa? Magazeti ulikuwa husomi online kwani?Au lengo lako ni kutaka tujue uko majuu??..ACHA MISIFA YA KIJINGA WEWE!
Jina lako peke yake lina maanisha ulivyo!Umezoea kuchangia uzi ...kama hujaelewa wapo walioelewa. Vizuri ungeuliza kama alivyo fanywA mwenzio kuuliza. Lini mtastaarabika Jamani? Hujui majukumu yangu...so isi lazima kuwepo muda wote na search net kujua Tz ikoje? Ndio maana niliuliza humu na members walinsaidia zana ...ndio vile nimewajuza.Bado hujakua pikok.
 
Ndevu Mbili yupo sawa kw kiasi flani. Bongo maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha, ishu ya umeme na maji ni cha mtoto. Usiombe uuguliwe halafu umechacha, hospitali za serikali hazina dawa wala vipimo hivyo watu inabidi tukimbilie kwa babu Samunge ndio tumaini lililo bakia.Maisha haya hadi lini?
Nmerurahi umenifaham member!Bado wenzetu wahitaji waelImishwe sasa! Wapo wanaamin ukiwa huku uzungumze kizungu muda wote! Ha ha ha !.
 
Shosti, klorokwini wameshaidaka hii thread bado aje Lizzy & co, basi hii thread is dead and buried.
Hata haina thamani ya kuchakachuliwa na mimi!!Kusiwe na maswali wala comment maana sitojibu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom