Niko njia panda katika maamuzi yangu na wazazi wangu, wanataka nijiendeleze kielimu

Sep 18, 2023
14
20
Habari wanaJf, mimi ni kijana niliyehitimu kidato cha sita mwaka 2021 katika tahasusi ya HGL, baadae nikaanza biashara yangu ya mpesa, mwaka huo sikuomba chuo kutokana na matatizo ya kifamilia.

Mwaka jana nikaomba chuo course ya sheria ila nikakosa mkopo, nikaamua kujikita kwenye biashara yangu, hadi kufikia sasa nina branch ambayo kwa kiasi kidogo imekuwa maana nimeweka na bank wakala ingawa siyo zote

Changamoto inakuja kwa upande wa wazazi wanaotaka nisome degree kwa wakati huu maana wanaamini sana katika ajira, na mimi nina wasiwasi juu ya biashara yangu maana kwenye hizi kazi wafanyakazi usipowafuatilia ni mwezi mmoja umetoka kwenye road.

Nilikuwa naomba msaada kwa wanaJF ili nichanganye na zangu
 
Hongera sana kwa kujiajiri kama utaweza ungesoma open masomo kuliko kuwa fulltime student ukacha kuangalia biashara yako vizuri .
 
Ukimaliza chuo anakupa pesa ya ya uhakika ya mtaji au ndio kusoma kwa pata potea ?
 
Wazazi wengine bwana wanatutafutiaga dhambi ya kuwachukia bure, wakati Mungu kasema waheshimu wazazi wako. Mimi nahisi wanakuonea wivu na pesa unayoipata. Kuna baadhi ya wazazi Huwa wanaona mtoto akishapata pesa basi hatawaheshimu Tena.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Hakuna mzazi mwenye wivu na mwanae asa wakumzaa hiyo haipo na kama itakua bas huyo sio mzaz halisi. Ila hao wazaz wanaanin sana katika ajira kuliko kujiajiri. Wanaamin biashara mda wowote inaweza bumbulika mtu akafirisika ila wanasahau ajira ni kutawaliwa na serikali, kampuni, Taasia au mtu binafsi. Chamhim akae nao azungunze nao je support yao katika nyanja zote za biashara yake na kujiendeleza kielim watam support vip?
 
Back
Top Bottom