Sijivunii wazazi wangu

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
4,156
7,416
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
 
Mwanetu weka akilini wewe sio wa Kwanza na kila unaye muona anaishi na kucheka usifikiri amekua ktk njia mkeka watu wamevuja damu Sana mioyoni ila Kuna mwisho kulingana na maamuzi utakayo chukua.

Kuna wale wamekuzwa kwa matusi na vipigo visivyo na likizo ... Wameishi Kama waasi kwenye nyumba walizo zaliwa ila maamuzi yameleta faraja.
Pigana usiendeleze uliyopitia wewe toka kwa wazazi.
Usipojitahidi kuyachukulia sehemu ya mapito ukayafanya ndio maisha yako.
Spika na Turubai ntatoa bure.
#Jikaze Mwanetu🏅
 
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na anajali jinsi wanavyolelewa (Zaburi 127:3, 34:11; Mithali 23:13-14). Wakati Mungu anatupa zawadi, pia anatoa maagizo ya wazi kuhusu matumizi yao.

Maeneo kadhaa katika Maandiko hutoa maagizo maalum kwa wazazi kuhusu jinsi ya kulea watoto wao. Waefeso 6:4 inasema, "Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana."

Kuna njia kadhaa ambazo wazazi wanaweza kuwachokoza watoto wao kwa hasira. Baadhi ya wazazi huweka viwango visivyowezekana ili mtoto akate tamaa ya kuitimiza kamwe. Wazazi wengine huwasumbua, huwadhihaki, au huwadhalilisha watoto wao kama njia ya adhabu, ambayo haina chochote bali huwachokoza kuwa hasira.

Ukinzani pia kunaweza kufanya hasira kwa kuwa mtoto hana uhakika kamwe juu ya matokeo ya matendo yake. Unafiki huwafanya watoto kukasirika wakati wazazi wanahitaji tabia kutoka kwa watoto ambayo wazazi hawajichagulii wenyewe.
 
5. Wewe ni matokeo ya starehe ya baba na mama yako.
4. Unahasira na vinyongo kwa wazazi wako.
3. Umasikini wa baba na mama yako haukuzuwii wewe kufanikiwa.
2. Usiingilie ugomvi na tofauti iliyopo kati ya baba na mama yako.
1. Dunia haitaki makasiriko, na hakuna aliyewahi kufanikiwa ama kufanya maamuzi sahihi akiwa mwenye hasira.
Mwisho nakushauri tu kwamba usiwalaumu wazazi wako na unapaswa kuwashukuru kwa kufanikiwa kukufukisha walau kidato cha nne.
Wapo wengi walio zaliwa na kutupwa.
Wapo walio lelewa na kutumikishwa.
Wapo walio someshwa hadi darasa la saba pekee.
Lakini wengi walitoboa na leo hawalalamiki tena hawana chuki kwa wazazi wao zaidi ya kumsgukuru Mungu na kuwa nguzo za mofano kwa wazazi wao.
 
Usimtukane wala kumtanzaga mama yako (eti singo mama)
Usimseme vibaya baba yako kwasababu bado anaishi kwa wazazi wake na hajafanikiwa kutoboa maisha.
Hao bado ni wazazi wako (haijalishi hata kama wangelikua vichaa)
Naelewa unazungumza nini mkuu na nilitegemea pia kukutana na maoni kama haya mimi hadi kufikia hatua naandika hivyo sio kwamba niliamka tuu mkuu, kuna wakati roho inaniuma alafu nikicheki still bado lawama nadondoshewa mimi tu sio kwao sio kwa ndugu zao kwamba siwazingatii wazazi wangu mkuu, kweli mimi niwe na uwezo nishindwe kumsaidia mzazi wangu!!!? Ni wazazi wangu ndiyo nawaheshimu sanasana na nawapenda sijawakosea heshima nimeweka wazi ili kueleza situation nzima ieleweke mkuu.
 
KABLA YA KUANDIKA COMMENT YAKO ZINGATIA KWAMBA HAKUNA ANAEPENDA KUWEKA WAZI BACKGROUND YAKE YA NYUMA IJULIKANE HASA KAMA SIO NZURI, UKIONA MTU ANAIWEKA WAZI MEAN KWAMBA IMEBIDI TU HAINA JINSI, SO NAANDIKA KUHUSU HAYO YOTE ILI WATU KUELEWA SITUATION NZIMA ILI UKITOA USHAURI MAYBE AU MAONI YAENDANE NA MAISHA YANGU KIUJUMLA. So, Kuandika kuhusu mama yangu kuwa single maza, Au baba kuishi kwa bibi yangu mean kwamba naiweka hivyo ili mjue situation nzima na sio kulaumu au kuwavunjia heshima maana nawaheshimu na kuwapenda sana ila jinsi walivyonitreat au wanavyonitreat hakufanyi nijivunie wao.
 
naelewa unazungumza nini mkuu na nilitegemea pia kukutana na maoni kama haya mimi hadi kufikia hatua naandika hivyo sio kwamba niliamka tuu mkuu, kuna wakati roho inaniuma alafu nikicheki still bado lawama nadondoshewa mimi tu sio kwao sio kwa ndugu zao kwamba siwazingatii wazazi wangu mkuu, kweli mimi niwe na uwezo nishindwe kumsaidia mzazi wangu!!!? Ni wazazi wangu ndiyo nawaheshimu sanasana na nawapenda sijawakosea heshima nimeweka wazi ili kueleza situation nzima ieleweke mkuu.
Nakushairi usipende kusikiliza sana maneno ya kuletewa kuhusu negatives stories za wazazi wako.

Anza kufanya/saidia kwa kiasi lakini usipungukiwe.

Kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wako ni wajibu ukingali bado unaishi, lakini kuwasaidia ukingali unanung'unika nisawa na bure kabisa (bora usiwasaidie hadi pale utakapo ona umefanikiwa na kutosheka).
 
KABLA YA KUANDIKA COMMENT YAKO ZINGATIA KWAMBA HAKUNA ANAEPENDA KUWEKA WAZI BACKGROUND YAKE YA NYUMA IJULIKANE HASA KAMA SIO NZURI, UKIONA MTU ANAIWEKA WAZI MEAN KWAMBA IMEBIDI TU HAINA JINSI, SO NAANDIKA KUHUSU HAYO YOTE ILI WATU KUELEWA SITUATION NZIMA ILI UKITOA USHAURI MAYBE AU MAONI YAENDANE NA MAISHA YANGU KIUJUMLA.
Kama ni backgrounds, wapo watoto walio fiwa na wazazi wakingali wadogo.

Wapo watoto walio zaliwa na kisha wakauzwa utumwani.

Wapo watoto walio zaliwa na kisha wakateswa.

Nakadhalika nakadhalika.... Haya yote unayo yaandika ninahakina ni sababu ya hasira tu kijana.

Mimi nafikiri haya umeyaandika ili upate kuuponya moyo na kupunguza maumivu.
 
Kama ni backgrounds, wapo watoto walio fiwa na wazazi wakingali wadogo.
Wapo watoto walio zaliwa na kisha wakauzwa utumwani...
Mkuu unajua kwenye maisha mtu akieleza hisia zake za kuumia usilinganishe na za mtu mwingine watu tunatofautiana mioyo so, lengo la huu uzi wangu ilikuwa ni kutua ya moyoni mwangu sio kutoa ya moyo wa mwingine, sijasema mimi nina situation mbaya kuliko wengine ila kwa kiasi changu hapo imefika nimeona niandike humu maana nobody knows me, nobody knows my parents pia.

So inabaki kama slogan ya Jf isemavyo "A place where we dare to talk" ila ahsante kwa maoni yako pia ya kujaribu kuonesha kwamba hii issue ni ndogo sana kwako inanipa moyo pia.
 
Back
Top Bottom