Nikiwa kama mwana Simba SC naiomba Kamati ya Maadili ya TFF iwafungie Chama na Sakho

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,134
110,489
Mimi ni mwanamichezo, mwana Simba SC lia lia na napenda utani na utani wetu wa Simba na Yanga ila sipendi na sifurahii upumbavu (Upan'gang'a) pale ukitokea.

Nitamshangaa na nitawashangaa pia kuona wana Simba SC wenzangu wakinichukia kwa hili na hata kutoniunga mkono kama kweli wana Spirit of a Sportsmanship ambayo GENTAMYCINE imenitawala mno.

Na nasikitika kuona kuwa zaidi ya mara mbili mchezaji Clatous Chama amefanya tukio hilo hilo ila Uongozi wa Simba SC wala haujamchukulia hatua kali za kinidhamu.

Nimeendelea kushangaa zaidi kuona hata mchezaji Pape Sakho naye siku za karibuni amekuwa ni mtu wa kucheza rafu za kijinga, lakini hata jana alipomkanyaga vibaya mchezaji wa Mtibwa Sugar FC hadi leo hii uongozi wangu wa Simba SC haujamchukulia hatua yoyote ile.

Najua kuna watu watahoji kuwa ninajuaje kama Uongozi wa Simba SC haujawachukulia hizo hatua za kinidhamu?

Jibu ni kwamba GENTAMYCINE 75% ya wachezaji wazawa wa Simba SC na Yanga SC ni wana (marafiki) na wamenihakikishia kuwa si Inonga au Chama au Sakho ambao ameitwa kwa uongozi na kuonywa au hata kufungwa ili heshima iwepo na maadili yafuatwe kwa ustawi wa soka (mpira) hapa Tanzania na duniani kote.

Ninaomba hawa wafungiwe haraka.
 
Kwa Chama nafikiri tuko pamoja na Safari hii Tff hawamuachi labda kama hawatalipata tukio vizuri.ya Sacko nayo haikua nzuri lakini angalau mtu hakua chini.
 
Mimi ni mwanamichezo, mwana Simba SC lia lia na napenda utani na utani wetu wa Simba na Yanga ila sipendi na sifurahii upumbavu (Upan'gang'a) pale ukitokea...
Faulo ya Chama niliianzishia Uzi siku ileile ya Mechi na Azam nikaonekana adui wa timu. Lakini narudia CHAMA AACHE KUJIFANYA MJANJA IPO SIKU ATAIGHARIMU TIMU.
 
Back
Top Bottom