Ayenda M
Member
- Jan 4, 2018
- 97
- 132
Maisha yetu binadamu yamezungukwa na mambo mengi sana. Kuna wakati kwenye maisha ukweli na uongo huamua kujitenga ili maisha halisi yajidhihilishe.
Ni kawaida ya wanadamu wote hasa waafrika kudevelop ego hasa pale wanapoona wao ni wa muhimu sehemu fulani. Sijui nani alituloga sisi ngozi nyeusi.
Huwa tuna imani kuwa kwa kuwa tunafanya kazi fulani, hakuna wa kuifanya kazi ile kuliko sisi au karibu na uwezo wetu. Hapana, tuache kuvimba... kuna mamilioni ya watu wanasubiri uchomolewe waoneshe ubora wao hata kuliko wewe.
Juzi nimeona stori ya Chama na Simba. Nikacheka. Kwa nini nilicheka na naendelea kucheka kila nikisoma makala za baadhi ya wachambuzi wetu wa Bongo.
Miaka ya hivi karibu hasa kipindi cha usajili Chama amekuwa akiichezesha Simba SC kama anavyotaka yeye. Anaisumbua kweli kweli Simba na maneno ya hapa na pale! Kipjndi chote hicho, Simba kama taasisi haijawahi kufanya maamuzi ya tofauti.
Ila Juzi imeamua kutoka na kufanya walichofanya. Simba SC imemchoka Chama, Chama hajaichoka Simba bali alitikisa kiberiti kuona. Show ilianza Chama siku hizi anacheza kifather sana. Anaonesha hana tena ile kiu ya mafanikio na kuipambania Simba SC.
Naamini chini ya Benchikha, Uongozi umuache Chama aondoke. Waishi maisha mengine bila Chama. Na inawezekana.
Walikuwepo akina Kichuya kona, Okwi na Kagere.... tuachane na wazee wetu akina Zamoyoni na wengine waliopita ila Simba bado ipo na itaendelea kupita.
Chama hataki kuiheshimu Simba Sc na ni muda sahihi wamuache aende haijalishi anaenda wapi. Simba iachane na Chama haraka sana kwa mstakabari wa mafanikio yake ya baadae.
Ahsante.