Hakuna shida mkuuSmart911 kama majina yanataka kufanana hiviš¤¦
Hakuna shida mkuuSmart911 kama majina yanataka kufanana hiviš¤¦
Sawa mkuu nimekuelewa.Jifijirie wewe, hivi unadhani hawakuona Microfinance uchwara kwa hiyo crown wanawapa hadi milioni 8 cash ndani ya dk chache mpaka waje kwako?
Kuna makini unaandaliwa kitu kizito utapigwa nacho kichwani hutaamini, nachokiona umeitamani crown, fanya hivi kahakikishe kama hiyo gari haina msala, kama ipo safi anza kuitumia vizuri uhakikishe ipo kwenye hali nzuri mda wote, watakapokuja utawapa gari yao, watakupa chako, wakiikataa unawaongezea hela unaendelea kuitumia
Asante kwa ushauri mkuu.We kachukue chako hiyo gari achana nayo warudishie au waambie kabisa unauza chenchi yao wape.
Otherwise watakusumbua maisha yote hao watu.

Kuhusu kuikodisha, hapana mkuu. Vyombo vya moto vina unforeseen risks nyingi sana. Inawezwa ikagongwa huko nikakosa pa kutokea.Kwasababu unashida na pesa yako na jamaa hawapatikani nakushauri kaingalie traffic Kama Ina msala, ikiwa fresh buni biashara rahisi tu ili hiyo gari ianze kukuingizia pesa. Fanya mpango hata uikodishe kwa mtu anayehitaji ili iingize pesa, jamaa wakirudi dai hela yako bila riba mmalizane. Mpaka hapo itakuwa imekupa faida kiasi
Mkuu, iko hivi, ile 3M niliyowapatia waliitumia kuwapatia askari ili kesi isiende Mahakamani. Yaani jambo liishie polisi. Kwahiyo hawana kesi yoyote.Watuhumiwa wa kesi ya Magendoo anakuletea Gari yake iwe kama Bond na wew kama wakili ukakubali kwa mkataba unajua kama kesi ikiwashinda pamoja na kuhonga kwao Polisi watakuja kuibeba hiyo gari kiulaini sanaa...! So wew kuwa mpole mfatilie kujua hao jamaa wako wapi kwanza ukishajua na maendeleo ya kesi yao hapo ndo utaweza kuamua kwa usahihi otherwise utaingia matatizoni...
Asante sana mkuu.Hiyo gari nayo itakuwa ya magendo.
Ni muda tu na wewe utakamatwa.
Hao ni wahuni tu.
Hata kuipaki kwako bado ni hatari.
Waite waje kuchukua gari yao.
Pesa hesabu tu hasara au ajali kazini.
Ila pole.
Ok nashukuru sana mkuu.endelea kutumia gari. siku wakija wape gari yao kisha chukua vijisenti vyako. huwezi kujua umafia wao ni wa kiwanga gani
Jiulize swali la Muhimu. Angekuwa Yesu angefanya nini?



we mwamba umewaza nini aisee?Niko makini zaidi ya unavyofikiri mkuu.Ogopa mfanyabiashara wa magendo, na hapo walikamatwa walikuwa tu hawajatoa maelekezo wanafahamianaga vizuri kuanzia polisi, TRA, na mamlaka zooote, jichanganye upotee gafla
No problem mkuu.Play your cards well
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.
Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.
Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.
Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.
Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!
Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!
Naombeni ushauri.
Ndio kakaMzee umesomea sheria nini? Nakuelewa vizuri hapo kwenye law of contract act.
, mimi ni Wakili.Vumilia vumilia kwanza mzee kula raundi kwanza bilashaka itakuwa ni zile wa vijana wa kimini mjini


Ok pamoja sana Kaka umetishaNdio kaka, mimi ni Wakili.
Utajimilikisha vipi huna mkataba wa mauzino,na wewe hujasajiliwa kutoka mikopo?Hata mimi sitaki magari ya watu mkuu, vitu vinabeba roho. So siwezi kujua ni kwanini wameniachia hili gari jipya kirahisi namna hii.
Aidha, kuhusu utaratibu wa kujimilikisha hilo gari ni rahisi sana, tena kwa utaratibu halali kabisa wa Kisheria, kuna kitu umechanganya ndio maana umezungumza kuhusu usajili, mimi siko huko mkuu.
Shida yangu kubwa ni hela yangu irudi kwenye biashara zangu.
Kutumia Crown kubebea tofali ni sawa na kula kuku mchemsho na muhogo mbichiKwani gari imekaa ndani kama picha?
Anza kuizungukia na kuifanyia biashara. Bebea hata matofali.
In case wakija hela watakupa, wasipokuja unakua umerudisha hela yako
Kutumia Crown kubebea tofali ni sawa na kula kuku mchemsho na muhogo mbichi

